DOKEZO Wastaafu wa TAZARA tunasotea stahiki zetu huu Mwaka wa 20, Rais Samia tusaidie

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Serikali ya CCM inafahamika vyema kihistoria kwa dhuluma dhidi ya hela za wastaafu. Ilianza tabia hii tokea enzi za utawala wa awamu ya kwanza.

Tulishuhudia kilio cha wazee wa iliyokuwa EAC ya awali. Wakati wenzao wa nchi za Kenya na Uganda wakilipwa mafao yao tena ndani ya wakati, wastaafu wa Tanzania wao waliambulia patupu. Licha ya kufuatilia kwa miaka nenda rudi waliishia kupewa porojo tu.

Angalia madeni yaliyokithiri na yasiyolipika ya serikali katika mifuko ya hifadhi za jamii. Mifuko hii imegeuzwa na serikali kuwa kama shamba la bibi pale inapokabiliwa na uhaba wa fedha za kuiendesha na kufanya anasa.

Angalia suala zima la kikokotoo. Wakati watawala wakijilipa mafao ya kukufuru, wastaafu wengine wanalipwa mafao kiduchu tena kupitia michakato iliyojaa mlolongo mkubwa.

Hawa wazee wanaolalamika hii leo, waliwahi kuwa vijana katika miaka yao ya kutesa. Walipita barabani huku wakiringa na kujidai kuwa wao na CCM ni damu damu, na tena wapo tayari kukilinda kwa gharama yoyote na hata kukifia chama chao.

Sasa leo kiko wapi! Walisaliti mapambano ya kutaka kuleta mageuzi, sasa hivi wanatafuta huruma kutoka kwa watesi wao walewale wa siku zote. Hali inajirudia hata katika nyakati za sasa, wakati watu makini wanapaza sauti zao, za kutaka katiba mpya, kuna watu wenye vichwa vigumu wakiwemo chawa maarufu ambao wanafahamika vyema hata ndani ya mitandao karibu yote ya kijamii, kwa makusudi wanajitoa ufahamu na kujifanya haelewi dhuluma inayofanywa na watawala, huku wakileta kejeli na dhihaka dhidi ya takwa hili nyeti na la wakati.

Wao pia ni wastaafu watarajiwa. Na itafika muda nao watakuja kuwa na kilio hiki hiki kama cha wenzao. Utakuja wakati ambapo watawala mafisi maji wa CCM watakuwa wakijilipa mabilioni ya fedha na wenzi wao, pamoja watoto wao, wao watakuwa wanalia na kusaga meno.

My friend, shetani hana rafiki. Tambua kuwa kila kitu kina gharama zake, iwe mbaya ama nzuri, Lakini uamuzi unao wewe mwenyewe ili kuweza kulipia hiyo gharama. Fanya uamuzi sahihi hii leo, mwaka huu wa 2024 ama mwaka kesho 2025, mchague shetani na mtesi wako ili muyajenge pamoja nae, ama la, chagua kesho yako iliyokuwa bora wewe mwenyewe pamoja na watoto zako
Hapo hujasemea Kikokotooo
 
Wazee wa jumuiya ya Africa mashariki wanakufa tu mmoja mmoja mpaka leo hawajalipwa.
wale walilipwa tena kwa awamu mbili. Mimi ninao shemegi zangu wawili na wote walilipwa.

Lakini wale walipiga mikwara ya uhakika ndiyo wakalipwa. Sijui kama unakumbuka ilifikia mpaka wengine kulala barabarani ndiyo serikali ikachukuwa hatua.

Sasa hao wa TAZARA wakijifanya wastaarabu watakufa na ustaarabu wao. Hatua ya kwanza ni kueleza masikitiko yao kwenye vyombo vya habari na hii ndiyo itamfikia Raisi kwa urahisi zaidi kuliko kulalamika pembeni.
 
Yeyote mwenye ufahamu asaidie kunijibu.

Nini kitasababisha pesa ya wastaafu isitolewe kwa kipindi chote hichi?

Kwa miaka 20 yote serikali ilikua inajibu nini?

Nilikua bado mdogo kufuatilia vitu ila nakumbuka kuna wazee walilala barabarani kudai mafao yao. Sijajua walikua ni TAZARA ama la
 
wale walilipwa tena kwa awamu mbili. Mimi ninao shemegi zangu wawili na wote walilipwa.

Lakini wale walipiga mikwara ya uhakika ndiyo wakalipwa. Sijui kama unakumbuka ilifikia mpaka wengine kulala barabarani ndiyo serikali ikachukuwa hatua.

Sasa hao wa TAZARA wakijifanya wastaarabu watakufa na ustaarabu wao. Hatua ya kwanza ni kueleza masikitiko yao kwenye vyombo vya habari na hii ndiyo itamfikia Raisi kwa urahisi zaidi kuliko kulalamika pembeni.
Usiandike kitu usichokijuwa, Mkapa aliwalipa flat rate ya nauli million 3 na mabosi mpaka million 15.

Hawajalipwa haki zao mpaka sasa wamefunga kesi Kwa serikali ya Uingereza na wameshinda.

Kinachoendelea NI process ya serikali ya Uingereza kuwalipa.
 
kwanza nipende kutoa shukran zangu kwa rais wetu Samia S. Hassan. ulipo andika CCM nimeishia kusoma. na bado
 
Usiandike kitu usichokijuwa, Mkapa aliwalipa flat rate ya nauli million 3 na mabosi mpaka million 15.

Hawajalipwa haki zao mpaka sasa wamefunga kesi Kwa serikali ya Uingereza na wameshinda.

Kinachoendelea NI process ya serikali ya Uingereza kuwalipa.
siyo kweli na wewe, mimi ninao shemegi zangu wawili walikuwa wafanyakazi wa railways na walilipwa kwa awamu mbili ndiyo mana nilijua. Na walipokuwa wanashughulikia issues zao walikuwa wanafikia nyumbani kwetu.

Labda kuna wale ambao hawakuwa na documents za uajiri (wenyewe wamekufa wanaodai ni warithi) ndiyo ilikuwa matatizo sana kuhusu malipo.

Na walipokuwa hawajalipwa walikuwa wanalala mpaka mabarabarani na maandamao kibao, mbona sasa kimya?
 
Bora nikuignore tu, nenda Keko Masantula alhamisi vikao vinafanyikia hapo.
 
Kama upo sehemu ukipata nafasi ya kuchota we chota shauri yako hawanaga shukran hawa jamaa.
 
Mzazi wangu ni mmoja wa Wazee ambao wamestaafu utumishi katika Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), mzee wangu na wenzake wengi waliostaafu Mwaka 2004, 2005 na 2006 hawajalipwa stahiki zao licha ya kufanya jitihada kubwa ya kushughulikia.

Naandika andiko hili kwa maelekezo ya Mzee wangu ambapo anachokisema ndicho nakiandika...

Mimi na Wazee wenzangu tupo zaidi ya 180 tumefanya jitihada kubwa tangu wakati huo hadi leo ikiwa ni takribani miaka 20 bila mafanikio huku Serikali ikituzungusha.

Wazee wachache ambao wana ndugu kwenye nafasi za juu Serikalini wao walifanikiwa kupata msaada na wakalipwa.

Waliolipwa walikuwa na ndugu au jamaa katika nafasi za Uwaziri na nyinginezo lakini sisi huku ambao naweza kusema ‘hatujuani na Wakubwa’ tumeambulia patupu bado tunateseka kufuatilia.

Kuna wenzangu kadhaa wameshapoteza maisha bila kupata stahiki zao, familia zao zimepambana nazo hazijafanikiwa.

Uhakiki wa madai yetu ulishafanyika na Serikali ikathibitisha tangu kipindi cha Rais Jakaya Kikwete hadi cha hayati Magufuli, ambapo tulionana hadi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikathibitishwa kuwa tunatakiwa kulipwa lakini hilo halijatekelezeka.

Suala letu lilifika hadi Mahakamani tukashinda shauri, baada ya hapo tukaonana na Waziri Mkuu kuwasilisha malalamiko yetu, akatusikiliza na akatukabidhi kwa maafisa wake washughulikie lakini tangu wakati huo danadana zimekuwa nyingi.

Wengi wetu wanaendelea kuteseka, wengine wanaumwa, jasho letu tulilolitoa kwa ajili ya Taifa linapotea, tunamasononeko, familia zetu zinamasononeko dhidi ya Serikali yetu kwa hiki kinachoendelea.

Mara kadhaa nimewashawishi wenzangu twenden kwenye Vyombo vya Habari kueleza changamoto zetu, hawataki kwa kuwa wengi wetu ni Wazee wa CCM na wakereketwa hasa, wenzangu wanaamini tukisema kwa Waandishi tunaweza kukiharibia chama, jambo ambalo mimi napingana nalo kwa kuwa ukimya wetu ndio anguko letu hadi tunakufa.

Taarifa zilizopo ni kuwa fedha tunazotakiwa kulipwa zipo Hazina na kuna wakati inadaiwa zimekuwa zikitoka na kurejea, kwa maana zinaingia katika matumizi mengine kisha zinarejeshwa.

Tumejuaje hilo? Harakati hizi za kwenda huku na huku zimetuwezesha kukutana na baadhi ya watu wa karibu na Mamlaka za juu wa Serikali ambao wanajua sakata hilo na wamekuwa wakitudokeza kuhusu hilo, kama ni kweli au la hilo sina uhakika.

Sisi Wastaafu wengi tuna hali mbaya sana kiuchumi, wengi tupo Dar na wengine wapo mikoa tofauti, tumeenda huku na huku bila mafanikio, yaani kwa ufupi tunatapatapa na imekuwa kawaida kuombaomba nauli kwa watu tofauti, ni aibu lakini hatuna jinsi.

Inaniuma sana kuona Watanzania tuliopambana kwa nguvu zetu zote kwa ajili ya Taifahiki haya ndio matunda.

Tumaini letu pekee limebaki kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwani kauli yake inaweza kuwa na nguvu ya kuweza kutusaidia kupata haki yetu.
Huu mtindo wa kila mtu mwenye shida ''kusali sala ya Taifa'' na kumalizia kwa kibwagizo cha ''tumaini letu pekee liko kwa Samia'' hautawasaidia enyi wabongo. Huyu ''mungu'' wenu mnayemlilia ndiye ameifikisha nchi hapa ilipo. Tegemeo pekee ni kuingana na wanaodai katiba mpya ili nchi iwe na mabadiliko.
 
Mzazi wangu ni mmoja wa Wazee ambao wamestaafu utumishi katika Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), mzee wangu na wenzake wengi waliostaafu Mwaka 2004, 2005 na 2006 hawajalipwa stahiki zao licha ya kufanya jitihada kubwa ya kushughulikia.

Naandika andiko hili kwa maelekezo ya Mzee wangu ambapo anachokisema ndicho nakiandika...

Mimi na Wazee wenzangu tupo zaidi ya 180 tumefanya jitihada kubwa tangu wakati huo hadi leo ikiwa ni takribani miaka 20 bila mafanikio huku Serikali ikituzungusha.

Wazee wachache ambao wana ndugu kwenye nafasi za juu Serikalini wao walifanikiwa kupata msaada na wakalipwa.

Waliolipwa walikuwa na ndugu au jamaa katika nafasi za Uwaziri na nyinginezo lakini sisi huku ambao naweza kusema ‘hatujuani na Wakubwa’ tumeambulia patupu bado tunateseka kufuatilia.

Kuna wenzangu kadhaa wameshapoteza maisha bila kupata stahiki zao, familia zao zimepambana nazo hazijafanikiwa.

Uhakiki wa madai yetu ulishafanyika na Serikali ikathibitisha tangu kipindi cha Rais Jakaya Kikwete hadi cha hayati Magufuli, ambapo tulionana hadi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikathibitishwa kuwa tunatakiwa kulipwa lakini hilo halijatekelezeka.

Suala letu lilifika hadi Mahakamani tukashinda shauri, baada ya hapo tukaonana na Waziri Mkuu kuwasilisha malalamiko yetu, akatusikiliza na akatukabidhi kwa maafisa wake washughulikie lakini tangu wakati huo danadana zimekuwa nyingi.

Wengi wetu wanaendelea kuteseka, wengine wanaumwa, jasho letu tulilolitoa kwa ajili ya Taifa linapotea, tunamasononeko, familia zetu zinamasononeko dhidi ya Serikali yetu kwa hiki kinachoendelea.

Mara kadhaa nimewashawishi wenzangu twenden kwenye Vyombo vya Habari kueleza changamoto zetu, hawataki kwa kuwa wengi wetu ni Wazee wa CCM na wakereketwa hasa, wenzangu wanaamini tukisema kwa Waandishi tunaweza kukiharibia chama, jambo ambalo mimi napingana nalo kwa kuwa ukimya wetu ndio anguko letu hadi tunakufa.

Taarifa zilizopo ni kuwa fedha tunazotakiwa kulipwa zipo Hazina na kuna wakati inadaiwa zimekuwa zikitoka na kurejea, kwa maana zinaingia katika matumizi mengine kisha zinarejeshwa.

Tumejuaje hilo? Harakati hizi za kwenda huku na huku zimetuwezesha kukutana na baadhi ya watu wa karibu na Mamlaka za juu wa Serikali ambao wanajua sakata hilo na wamekuwa wakitudokeza kuhusu hilo, kama ni kweli au la hilo sina uhakika.

Sisi Wastaafu wengi tuna hali mbaya sana kiuchumi, wengi tupo Dar na wengine wapo mikoa tofauti, tumeenda huku na huku bila mafanikio, yaani kwa ufupi tunatapatapa na imekuwa kawaida kuombaomba nauli kwa watu tofauti, ni aibu lakini hatuna jinsi.

Inaniuma sana kuona Watanzania tuliopambana kwa nguvu zetu zote kwa ajili ya Taifahiki haya ndio matunda.

Tumaini letu pekee limebaki kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwani kauli yake inaweza kuwa na nguvu ya kuweza kutusaidia kupata haki yetu.
Mbona kama mtoto wa mstaafu hivi umeandika uzi kwa machungu sana
 
Back
Top Bottom