Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,524
- 8,171
Kiongozi wa wamasai waliohamia Ngorongoro wamelalamikia Serikali kutotimiza ahadi zake huku wananchi hao wakiwa wamevunja maboma yao Ngorongoro na kuhamia Msomera.
Wananchi hao 136 wamesema zoezi hilo limezungukwa na udanganyifu, wamemtaka Rais Samia kufuatilia zoezi hilo kwa kuna watendaji wake wasio waaminifu.
Wananchi hao wamesema wasipotendewa haki zao wanakusudia kurudi Ngorongoro.
Akijibu malalamiko hayo, mkuu wa wilaya ya Handeni, Albert Msando amesema Serikali imetimiza ahadi zake kwa wananchi wote waliohamia Msomera na mpaka sasa wamepokea kaya 1600 ambayo ina watu 6,700 ikiwemo fidia, motisha ya nyumba, motisha ya shilingi milioni 10 na shamba kwaajili ya kilimo.
Amesema kilichotokea kwa wanaodai wengi ni wategemezi kwani anayelipwa fidia ni mkuu wa kaya/boma. Kwa familia ambayo baba ana wake watatu analipwa mkuu wa kaya tu, wanaodai wengi ni wake wa mkuu wa kaya au mtoto wa mwenye boma ambayo haikuwa ahadi ya Serikali.