Wakati Marekani inaendelea kuilenga kampuni ya TikTok, TikTok inaendelea kuwa maarufu barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,022
1,046
1713852816526.png

Katika siku za karibuni Marekani imeendelea na mpango wake wa kuishambulia China na makampuni yake, baada ya wabunge na ikulu ya Marekani kusema wana wasiwasi kuwa kampuni inayomiliki App ya TikTok inahatarisha usalama wa Marekani na inaweza kutumiwa kufanya ushawishi kwenye uchaguzi wa Marekani. Hata hivyo kumekuwa na upinzani mkali kutoka kwa zaidi ya nusu wa Marekani ambao ni watumiaji wa app ya TikTok..

Wamarekani zaidi milioni 170 wamekuwa watumiaji wakubwa wa app ya TikTok, watumiaji hao wanatumia app hiyo kwa kufuatilia habari mbalimbali za kijamii, kuchangia video binafsi na wenzao, na wengine wanatumia app hiyo kwa mambo ya burudani, kutafuta habari na kujiingizia kipato.

Baada ya serikali ya Marekani kueleza nia yake ya kutaka kuipiga marufuku app hiyo, Wamarekani hao waliojua kuwa lengo hilo ni moja ya hatua ya serikali ya Marekani ni kudhibiti uhuru wao wa kutumia app hiyo, na sio maswala ya usalama kama wanasiasa walivyosema, walijitahidi kuwasiliana na kupinga nia ya wabunge wa Marekani kupiga marufuku app hiyo.

Kwa muda mrefu sasa sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano ya China imekuwa ikipiga hatua, na sio tu kuwa na manufaa ya mawasiliano, bali pia imekuwa ikiwanufaisha wale wanaotumia teknolojia hiyo kujiingizia kipato.

Lakini ukweli pia ni kuwa kutokana na China kuwa na gharama za chini za uzalishaji na uendeshaji wa miundombinu na mitandao ya kijamii, kunakuwa na changamoto kubwa kwa nchi nyingine kushindana na China, ndio maana baadhi ya nchi zinatumia kisingizio cha ‘usalama’ ili kukwepa ushindani.

Ukweli ni kwamba TikTok imepata umaarufu duniani kutokana na wahandisi wake, kujua vizuri matakwa ya wateja wake na kuwa na gharama za chini kwa wale wanaoitumia kibiashara na hata kuwa na gharama sifuri kwa wale wanaoitumia tu kwa burudani. Lakini pia kampuni ya TikTok imekuwa ikihimiza maendeleo ya matumizi salama ya mtandao wa internet kwa watumiaji

Ni hivi karibuni tu kampuni ya TikTok na Umoja wa Afrika walifanya mkutano na kufikia makubaliano ya kuhimiza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano barani Afrika.

Kwa bara la Afrika lenye idadi kubwa zaidi ya vijana duniani, kuwa na ushirikiano na kampuni ya TikTok, ni mwelekeo ambao uko duniani nzima, ndio maana kwa sasa tunaona app hiyo ina umaarufu mkubwa Afrika Kusini, Kenya, Nigeria, na Misri.

Umoja wa Afrika na TikTok wametangaza mpango wa pamoja wa usalama kwenye mtandao wa internet ili kuwawezesha vijana wa Afrika kuwa na maarifa na zana za kuwa kwenye mtandao wa internet kwa usalama, huku wakijitafutia fursa za kujiingizia kipato.

Kwenye taarifa iliyotolewa na pande hizo mbili, pande hizo zimesema mpango huo ulizinduliwa kwenye mkutano wa hivi karibuni wa TikTokSafer Internet Summit nchini Ghana, ambao si kama tu una lengo la kuwawezesha vijana wa Afrika bali pia wazazi na waelimishaji kuhusu usalama wa kidijitali.

Ukweli unaonesha kuwa suala la tiktok halihusiani na maswala ya usalama kama baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanavyojaribu kuiaminisha dunia, uhalisia ni kwamba linaonekana ni suala linalotumiwa na wanasiasa kwa maslahi.

Kama itakumbukwa aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump alipinga tiktok alipokuwa madarakani, lakini sasa amesema wazi kuwa kama atakuwa madarakani hataipinga app hiyo.
 
Mimi nikajua Ulaya

Ukataliwe USA ,ukubaliwe Africa halafu ujisifu?

Pamoja na mambo mengine,wao USA wana makampuni kinzani na Tik Tok kama Instagram, whatsapp, facebook. Kwahiyo pia yawezakuwa ni namna ya kuyalinda makampuni yao dhidi ya wapinzani
 
Mimi nikajua Ulaya

Ukataliwe USA ,ukubaliwe Africa halafu ujisifu?

Pamoja na mambo mengine,wao USA wana makampuni kinzani na Tik Tok kama Instagram, whatsapp, facebook. Kwahiyo pia yawezakuwa ni namna ya kuyalinda makampuni yao dhidi ya wapinzani
Pia ukumbuke makampuni kama Facebook na Instagram uko kwao Chinese hayatumiki. Wachina wapumbavu sana, wao hawataki vya magharibi lakini vyao wanataka watumie
 
Back
Top Bottom