DOKEZO Shule ya Sekondari Longido ina Wanafunzi wengi kuliko idadi ya Mabweni na madarasa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mzazi na mhathirika wa haya yanayotokea, Shule ya Sekondari Longido iliyopo Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha, shule ina Wanafunzi wengi sana kupita kiwango.

Jumla ya Wanafunzi ni zaidi ya 2,000, idadi ambayo ni wengi kuliko idadi ya mabweni na madarasa yaliyopo.

Kwa kawaida darasa linatakiwa liwe na Wanafunzi 45 lakini kwa Longido imezidi.

Ni shule ya Kata lakini Wanafunzi wa Kata ya pale wamekuwa wakitafutiwa sababu za kufukuzwa shule kwa kigezo wanaotoka pale katani ni wakorofi.

Ofisi ya malezi inaongoza kunyanyasa Wanafunzi, kuwapiga na kuwatesa pamoja na kauli chafu wanazotolea Wazazi.

Pia miundombinu ya mabweni madarasa na hata dinning imechakaa sana.
 
Mwalimu hawezi kumtafutia mwanafunzi sababu ili amfukuze shule, waleeni watoto wenu vizuri ili waendane na taratibu za shule.

Tatizo wazazi wengi hawana nidhamu kutokea nyumbani na watoto wao nao vivyo hivyo.

Mwalimu anakuwa na kazi ya kumfundisha nidhamu mzazi na mtoto wake, na hapo ndio wazazi hulalama wamejibiwa vibaya na walimu wetu.
 
Mimi ni mzazi na mhathirika wa haya yanayotokea, Shule ya Sekondari Longido iliyopo Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha, shule ina Wanafunzi wengi sana kupita kiwango.

Jumla ya Wanafunzi ni zaidi ya 2,000, idadi ambayo ni wengi kuliko idadi ya mabweni na madarasa yaliyopo.

Kwa kawaida darasa linatakiwa liwe na Wanafunzi 45 lakini kwa Longido imezidi.

Ni shule ya Kata lakini Wanafunzi wa Kata ya pale wamekuwa wakitafutiwa sababu za kufukuzwa shule kwa kigezo wanaotoka pale katani ni wakorofi.

Ofisi ya malezi inaongoza kunyanyasa Wanafunzi, kuwapiga na kuwatesa pamoja na kauli chafu wanazotolea Wazazi.

Pia miundombinu ya mabweni madarasa na hata dinning imechakaa sana.
Tafuta pesa mwanao akasome shule bora na sio bora shule.Ni kawaida sana kwa shule za serikali kukuta wanafunzi hata mia 3 wapo darasa moja.
 
Ni vyema Sana jamii na serikali kwa ujumla kuchukua hatua katika kutatua kero hii kwa sababu Kila mmoja anapenda kupata elimu katika mazingira mazuri, huwezi kupata wasomi Bora ikiwa mazingira ya wanafunzi na miundombinu kwa ujumla ni mibovu. Suala la wanafunzi kutafutiwa makosa ili wafukuzwe ni vizuri Sana Kama serikali itachukua hatua stahiki kwa ajili ya kuondoa shida hii ikiwa ni pamoja na kufanya uchunguzi wa kutosha Kama ni kweli au la.
 
Back
Top Bottom