Rais Samia Atoa Ujumbe wa Eid Al Adh'haa, Awakumbuka Wenye Uhitaji

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,505
3,040
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za heri ya sikukuu ya Eid el Adh’haa kwa dua maalum akiwataka Watanzania kusherehekea kwa amani, umoja na upendo.

Ametuma salamu hizo leo Alhamisi Juni 29, 2023 kupitia kurasa za mitandao yake ya kijamii huku akiwahimiza Waislamu kutumia siku hii kuwakumbuka wale wote wenye uhitaji zaidi.

“Nawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Eid el Adh’haa. Tusheherekee siku hii njema kwa amani, umoja na upendo, tukiwakumbuka wale wote wenye uhitaji zaidi.

“Tutumie siku hii pia kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu azipokee ibada zetu, atusamehe makosa yetu, atuongoze katika mema, kweli na haki, tuendelee kuwa wamoja na atuepushe na yote yenye nia ya kutugawa. Eid el Adh’haa Mubarak,” ameandika Rais Samia.
 
Watanzania sote tu wahitaji wa kunufaika na rasilimali zetu.
Watanzania sote tunahitaji la kuona bandari yetu haitolewi sadaka kwa DP-World kwa IGA hii.
 
Na kwako pia mama,
Same to you
Mungu akulinde na warundi na wanyarwanda waliojipenyeza kupitia kanisa wakitaka kukutawala katika utawala wako, mama tumia mamlaka kama mtawala, nia yako ni njema, please usicheke na hawa mamluki, pita alimopita magu hakuna ataekuchezea, utakuja kunishukuru baadae
 
IMG_7396.jpg

IMG_7387.jpg

IMG_7381.jpg
 
Back
Top Bottom