Nitasikitika sana kuona ndugu zangu wakiacha Salaa kisa Simba na Al Ahly

Leo ni siku ya ijumaa, al hamdu liLlah nimesali pamoja na waislamu wenzangu, nasubiri muda wa iftar ufike kisha sala ya ISHAA then TARAWEEH inshaa Allah

Ila nitasikitika sana sana Ndugu zangu Waislamu wale ambao sala kwao sio muhimu ila Mpira kwao ndio kipaumbele na muhimu kuliko sala.

Je! Mpira ndio utakuingizeni peponi! Hivi unaachaje kusali na kukimbilia mambo ya kidunia, ya kipumbavu yasiyokua na maana! Unaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu aliekuumbeni na akawapa rizki badala yake mnakimbilia mpira, kweli!

Nawausia, pamoja na kuiusia nafsi yangu twendeni msikitini, mambo ya kwa mkapa achaneni nayo, na wale wanaosali sala ya ishaa na kutoka bila kusali TARAWEEH kisa mambo ya dunia/mpira kwa kweli tutaenda kuulizwa.

Kwanza mpira ni Haram, na uharam wake mnaujua.

Assalaam alaikum warahmatullah
Ujui kuwa simba na yanga ni dini yao
 
"Ya Kaisari Muachie Kaisari,,Na ya Mungu Mpe Mungu"hao hae waliokuletea na kukukaririsha hizo Tarawee zako wanamiliki timu za mipira,,,na wapo watashuhudia kandanda leo na Wana uwezo wa kiakili hadi kimali kushinda wewe mwalimu wa masjidi ambae wanakutumia kueneza utamaduni wao
hah !
 
p_6832124121384522232757_0_5e7075bc9850341bc4dd7edf10dd5eca-jpg.2528770.jpg
 
Back
Top Bottom