DOKEZO Miundombinu ya Mkuranga ni mibovu, mvua inaongeza tatizo, Wananchi wa hali ya chini ndio tunaoteseka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
WhatsApp Image 2024-04-25 at 06.52.00_80766e2a.jpg

WhatsApp Image 2024-04-25 at 06.52.01_da67222b.jpg
Mwanzoni Miaka ya 2000 kila mvua iliponyesha wakati wa kuvuka Barabara tulikuwa tunalazimika kuvua viatu na kukunja nguo kisha tunavuka.

Miaka zaidi ya 20 baadaye hali tuliyoizoea kuvuka kwenye maji kila mvua inaponyesha ndio ileile.

Miundombinu yetu wakazi wa Mkuranga kwa asilimia kubwa ni mibovu, viongozi wengi ngazi ya mtaa na hata Mbunge wamekuwa wakitupa ahadi nyingi ambazo hazitekelezeki.

Mbunge wetu kila mara tumekuwa tukimwambia kuhusu hali hii lakini hatekeleze ahadi zake za maboresho, yeye amekuwa bize na masuala ya wakulima na wafugaji.

Tunakubali kuwa miundombinu ni mibovu lakini hizi mvua zinazonyesha zinathibitisha tu kuwa Wananchi wa Mkuranga maeneo ya njia za Lugwadu, Mkokozi kwenda Rungwadu, Mwandege Mitaa ya Kariakoo na Vicheji.

Upande wa Barbara zimekuwa zikikwanguliwa lakini haziwekwi mifereji ndio maana maji yanakosa pakupita na yanaingia kwenye Barabara hadi katika makazi ya watu.
 
Hatari sana,hapo sehemu gani mkuu?
 
Kwasasa pwani ndiyo inaongozwa kwakuwa na mawaziri!! Wambieni yote Kwa yote wakumbuke na ya nyumbani!!
 
Kwa kweli mbunge wetu kuna mahali unakosea maana tangu kipindi cha jua kali niliwahi kusema brbr ya kutoka mbande kwenda singbad mpaka kwako ulipozaliwa kuna siku watu hawatatoka ndani usipoboresha makalavati ya mto MZINGA ona sasa jana maji yamebomoa mpaka yale yalokuwepo
Natabiri siku sio nyingi watu wa mwanamnaya mipeko singbad watakaa kama wapo kisiwani
Halafu 2025 tutakupitisha tena na kukupigia makofi unafanya kazi nzuri
 
Back
Top Bottom