Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 943
- 4,457
Nimesoma kitu kinachoitwa usafirishaji haramu wa binadamu huko Duniani na mbinu zinazotumiwa. Takwimu zinaonyesha kwamba hii biashara ni kubwa labda namba tatu baada ya biashara ya silaha na madawa ya kulevya.
Nimejikuta kusoma kutokana na kuona ndani ya wiki mbili zimekamatwa V8 tatu nchini zikiwa na wahamiaji haramu ambao ukiwaangalia kwenye picha unaona wamedhoofu sana.
Taarifa zinaonyesha kwamba Duniani biashara hii inafanywa na viongozi wa umma na kisiasa. Inafanywa na matajiri wakubwa ambao kabla ya kufanya haya ukikuta kutengeneza network nzuri na wanasiasa waliopo madarakani kuepusha mkono wa sheria.
Tanzania kwa hali hii inayoendelea ni Ishara kwamba wanasiasa wanatafuta fedha za uchaguzi 2025. Katika hali hii hakuna mwanasiasa atakayekamatwa na vyombo vya dola then hao waliomkamata wakabaki salama. Ukijitia kukamata lazima aidha uondolewe kwenye kiti au usimamishwe kazi.
Mimi siyo mtabiri ila kwa ukamataji unaofanywa na Polisi na Uhamiaji siku si nyingi utasikia viongozi wa taasisi hizi kwenye mikoa na makao makuu wametambuliwa. Watatumbuliwa kwa sababu wanaosafirisha hawa wahalifu ni wabunge, ni mawaziri, madiwani, watendaji wa vijiji, wafadhili wa vyama vya siasa nk.
Dalili hizi zimeonekana Duniani kote ambapo mfumo wa serikali umeruhusu wenye fedha kupanga safu ya utawala wanayotaka.
Tumeona namna ambavyo wanaopambana na madawa wanatumbuliwa kila siku; siyo kwamba wanakosea ila wanaingilia anga za wenyewe. Na mimi pia niwaandae kisaikologia viongozi wa polisi kwenye root zote zinazotumiwa na hawa viongozi kupitisha magendo yao kwamba wajiandae kutumbuliwa.
Niwatake waliopo makao makuu ya hizi taasisi kujiandaa kisaikolojia kwani muda si muda usishangae fedha ikapenya bungeni wabunge wakaanza kupiga kelele kwanini hawa watu wanakamatwa Morogoro, Manyara, Iringa, Dodoma, Mbeya.......utasikia kwanini wasizuiliwe huko mipakani na wataconculude viongozi wameshindwa kazi waondolewe.
IGP na Mkuu wa Uhamiaji msikubali kudhibitiwa na wahalifu hawa wanaowaza matumbo yao. Pelekeni kikosi wanapoingilia Tanga, Kilimanjaro , Arusha na huko Mara mkalinde mpaka. Bora wawapige Majungu mtumbuliwe kwa kuwadhibiti kuliko kuogopa kudhibiti.
Mwisho; tuambieni hizi V8 mlizokamata zimesajiliwa kwa majina gani? Msipowataja hao wamiliki mnawafanya wengine nao kuendelea kutumia malori na mashangingi kushamirisha uhalifu huu. Kwanini hakuna mmiliki wa V8 aliyekamatwa na kuhojiwa hadi sasa?