Kumuona nabii kiboko ya wachawi ni laki tano

Expensive life

JF-Expert Member
May 2, 2020
1,835
5,830
Kama haujawahi kukutana na matatizo basi unaweza kushangaa hili, watu wanamatatizo ndugu zangu.

Nina ndugu yangu ni mtoto mdogo tu kama unavyojua tena maisha ya vijijini mabinti huolewa mapema, umri wa miaka 25 tu anatesea na masuala ya uzazi.

Mume anataka mtoto, mimba akishika tumbo halikui kabisa, vipimo vinainyesha ana mimba lakini baada ya muda inapotelea mbali.

Kuna kipindi mimba ilikaa miezi 12 lakini baadae ikapotekea mbali, kutokana na kadhia ya mumewe binti akaanza kutafuta msaada kwa waganga huko kijijini nako akatoka patupu.

Akaamua kuja dar kwa dada yake kutafuta msaada zaidi, dada yake akampeleka kwa nabii kiboko ya wachawi, kufika pale wakaambiwa utaratibu wa kumuona nabii ni tsh. 500k.

Ikabidi warudi home kwa kuwa pesa hawana, bahati nzuri kuna siku nabii alitangaza bei ya ofa, yaani hiyo siku kumuona ni 100k, hii ikaleta unafuu kwa huyu dada kwenda kuonana na nabii.

Baada ya kuonana na nabii akamwambia umetupiwa majini watatu, hao ndio huwa wanakula mimba zako. Kuyatoa hayo majini yote aandae 3 million. Kutokana na kutokuwa na pesa shughuli iliishia hapo.
 
Huyu Nabii huwa namsikiliza usiku kwenye redio ya EFM, ana maigizo flani ya kufufua watu, kuna simu zinapigwa na wasikilizaji na kusema ndugu yao amefariki muda huo, so wanaomba msaada ili awasaidie, mara anawaambia roho ya ndugu yao bado ipo hapo ndani, anawapa maelekezo then unasikia wanasema marehemu kapiga chafya na kaamka 🤣🤣🤣🤣
 
Wapiga simu wanakuwa wapo nae hapo hapo studio mkuu.kuna pastor wa Kenya walimrecord yaani utashangaa.piga wewe hiyo simu uone
 
2 Timotheo 4:3-4
[3]Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;

[4]nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
 
Kama haujawahi kukutana na matatizo basi unaweza kushangaa hili, watu wanamatatizo ndugu zangu.

Nina ndugu yangu ni mtoto mdogo tu kama unavyojua tena maisha ya vijijini mabinti huolewa mapema, umri wa miaka 25 tu anatesea na masuala ya uzazi.

Mume anataka mtoto, mimba akishika tumbo halikui kabisa, vipimo vinainyesha ana mimba lakini baada ya muda inapotelea mbali.

Kuna kipindi mimba ilikaa miezi 12 lakini baadae ikapotekea mbali, kutokana na kadhia ya mumewe binti akaanza kutafuta msaada kwa waganga huko kijijini nako akatoka patupu.

Akaamua kuja dar kwa dada yake kutafuta msaada zaidi, dada yake akampeleka kwa nabii kiboko ya wachawi, kufika pale wakaambiwa utaratibu wa kumuona nabii ni tsh. 500k.

ikabidi warudi home kwa kuwa pesa hawana, bahati nzuri kuna siku nabii alitangaza bei ya ofa, yaani hiyo siku kumuona ni 100k, hii ikaleta unafuu kwa huyu dada kwenda kuonana na nabii.

Baada ya kuonana na nabii akamwambia umetupiwa majini watatu, hao ndio huwa wanakula mimba zako. Kuyatoa hayo majini yote aandae 3 million. Kutokana na kutokuwa na pesa shughuli iliishia hapo.
Mathayo 10:8 maombi ni bure ukiona unatozwa pesa ujue huyo siyo nabii bali ni mganga wa kienyeji aliyejivisha unabii feki.
 
Back
Top Bottom