Jina 'Machinga' chimbuko lake ni nini?

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,089
1,879
Habari kwenu wanajamii wote.

Nataka kujua na kwa faida ya wengine, hivi jina " Machinga lina asili gani? Kwanini Machinga awe na jina lake badala ya kuitwa tu mchuuzi au mjasiliamali?

Mwenye uelewa zaidi na asili ya jina "Machinga" atusaidie.
 
Habari kwenu wanajamii wote. Nataka kujua na kwa faida ya wengine, hivi jina " Machinga lina asili gani? Kwanini Machinga awe na jina lake badala ya kuitwa tu mchuuzi au mjasiliamali?
Mwenye uelewa zaidi na asili ya jina "Machinga" atusaidie🙏🙏🙏🙏
machinga lazima awe anatembea tembea sana ila machinga wa saivi wamekua wavivu wanakaa sehemu
 
Neno hilo asili yake ni kabila la Mchinga lipo huko kusini. Vijana wa kimachinga toka huko Lindi? walijipatia umaarufu Jijini Dar es salaam katikati ya miaka ya tisini kwa kufanya biashara ya kuchuuza vitu Kam vile nguo,urembo,viatu,vyombo,n.k kwa kutembea mitaani au kupanga pembezoni mwa barabara ndio maana wachuuzi wanaotembeza vitu na wale wanaopanga maeneo yasiyo rasmi wamepewa jina hilo

Sasa hivi hili neno linatimika Tz mzima kuwakilisha
 
Habari kwenu wanajamii wote.

Nataka kujua na kwa faida ya wengine, hivi jina " Machinga lina asili gani? Kwanini Machinga awe na jina lake badala ya kuitwa tu mchuuzi au mjasiliamali?

Mwenye uelewa zaidi na asili ya jina "Machinga" atusaidie.
Ilisha jadiliwa sana humu miaka ya nyuma.
 
-Marching guy=Anayetembea amebeba bidhaa akiziuza.
-Check line=mkatizo,mapishano ya barabara na reli/railwaycrossing.
Hence,matamshi ya kiswahili kuunganisha maneno.
-Marching guy=machinga
-Check line=chekeleni.
Need I write more?
Umenikumbusha enzi za mzungu ameenda Newala(huko mtwara),akachimba kisima maana maeneo ya Newala Kuna ukame sana.

Akakiita "New well",waswahili kwa kushindwa kutamka maneno ya kingereza wakaita "Newala".

Hadi Leo imekuwa Newala,na imekuwa wilaya sasa.
 
Ilisha jadiliwa sana humu miaka ya nyuma.
Ahsanteni sana kwa mchango wenu
 
Habari kwenu wanajamii wote.

Nataka kujua na kwa faida ya wengine, hivi jina " Machinga lina asili gani? Kwanini Machinga awe na jina lake badala ya kuitwa tu mchuuzi au mjasiliamali?

Mwenye uelewa zaidi na asili ya jina "Machinga" atusaidie.
Tafuta kitabu cha 'SAFARI YA CHINGA' kimeandika na Prof. Shani Omari
 
Neno hilo asili yake ni kabila la Mchinga lipo huko kusini. Vijana wa kimachinga toka huko Lindi? walijipatia umaarufu Jijini Dar es salaam katikati ya miaka ya tisini kwa kufanya biashara ya kuchuuza vitu Kam vile nguo,urembo,viatu,vyombo,n.k kwa kutembea mitaani au kupanga pembezoni mwa barabara ndio maana wachuuzi wanaotembeza vitu na wale wanaopanga maeneo yasiyo rasmi wamepewa jina hilo

Sasa hivi hili neno linatimika Tz mzima kuwakilisha
Huu ndiyo ukweli. Hayo mambo eti asili yake ni Marching - guy ni uzushi tu Wa kifesibuku.
 
Back
Top Bottom