Jenga gorofa moja kwa gharama nafuu

Wengi wanaogopa sana kujenga ghorofa wakizani labda mpaka uwe na pesa nyingi ndio ujenge. Ukiamua hakuna kinachoshindikana, kama umeweza kujenga nyumba ya chini,jua una uwezo pia wa kujenga ghorofa. Fanya yafuatayo kutimiza ndoto zako:-
  • Weka kwenye michoro wazo la nyumba yako (jichoree mwenyewe unavyotaka)
  • Tafuta injinia akuandalie BOQ (idadi ya matirio yatakayotumika),michoro, na ramani
  • Tafuta kibali cha ujenzi- itategemea na eneo uliopo
  • Anza kununua mawe, kokoto nyeusi, mchanga, matofari ya kuanzia, nondo. simenti-kwa ajili ya msingi
  • Nenda maeneo yanapojengwa magorofa, na umchukue fundi unayemuona anapiga kazi
  • Ingia makubaliano na huyo fundi-akupatie gharama ya msingi, ikiwezekana mkubaliane kwa siku.
  • Anza kazi ya msingi.
  • Weka rafu/ zege kwenye msingi
  • Anza kupandisha nguzo na tofali kwa awamu awamu kutokana na mzunguko wako wa pesa- unaweza kumtumia yule fundi wa mwanzo au ukatafuta mwingine
  • Ukifika kwenye lenta-inabidi upumzike
  • Anza kukusanya nondo,kokoto nyeusi, simenti,misumari
  • Angalia pa kukodi 'plate' au 'marine board',kwa siku gharama yake huwa ni sh. 400/= kwa moja, pia kukodi mirunda, mbao; inategemea na sehemu ulipo.
  • Mwite fundi kwa kazi ya 'slab'- hapa ndipo huwa pagumu sana kwenye ghorofa
  • Akishamaliza slab, pumzika utafute nguvu
  • Endelea na ujenzi wa juu
  • Paua mjengo wako
  • Endelea na hatua zingine za 'finishing'
  • Baada ya hapo jipongeze....kwa kutembelea mbuga za wanyama
Ni busara kumtafuta engineer yeye ndio akasimamia kazi yako..na yeye ndio unaweza muachia jukumu la kukutafutia fundi mzuri..client wengi hawana uelewa na ujenzi hivyo wanapaswa kuongozwa na wataalamu ujenzi.

Michoro huwa inaandaliwa na Architect, Quantity surveyor anaada gharama za ujenzi..then Engineers wana design ( Msingi, beams Nguzo, Slabs, Ngazi etc....Ujenzi wa ghorofa ni tofauti na nyumba yakawaida....

Msingi unatakiwa uwe imara kuishikilia nyumba...na aina ya msingi unakuwa selected kwa kuangalia aina ya udongo uliopo ( soil testing lazima ifanyike) yote haya hufanyika ilikujua ni aina gani ya msingi utatakiwa kujengwa.....

Ukijenga bila utaratibu ni kuweka hela yako at risk
 
Natamani Kuja Kujenga Ghorofa Hata Ya Flow Moja Ila Iwe Standard Sio Ili mradi....
Changamoto niliyo nayo ni nitaanzia wapi?kwa sababu wanatoa conditions gani ili upewe building permit ya ghorofa
 
Tafuta mtaalamu wa michoro na ramani, inaweza isizidi laki 2; baada ya hapo nenda halmashauri/manispaa kwa ajili ya kibali, haitazidi laki 2.. baada ya hapo nunua malighafi
 
Ni vizuri pia kuwa na nyumba ya ndoto yako, ingawa changamoto huwa bei ya malighafi; mfano mimi nondo nilikuwa nachukulia kiwandani ili kupunguza gharama, unakuwa unauziwa kwa tani.
Mkuu nondo ulinunulia kiwanda gani
 
Siku mie namwaga slab mifuko 116 ya cement inondoka mbele ya macho yangu ndio nilipojua haya maghorofa yote ni kujijaza upepo tuu unless ni for business.

Bora ujilie mbususu tuu kwenye nyumba yako ya chini ya mil100. Muhimu kuwe na kipupwe vyumba vyote na maji yanatoka kwa presha basi.
Mkuu naomba makisio ya Nondo za kumwaga jamvi baada ya kupandisha kuta kozi 10 na kufunga linta
 
Siku mie namwaga slab mifuko 116 ya cement inondoka mbele ya macho yangu ndio nilipojua haya maghorofa yote ni kujijaza upepo tuu unless ni for business.

Bora ujilie mbususu tuu kwenye nyumba yako ya chini ya mil100. Muhimu kuwe na kipupwe vyumba vyote na maji yanatoka kwa presha basi.
Mkuu hiyo 116 ni slab ya mita skwea ngapi
 
Wengi wanaogopa sana kujenga ghorofa wakizani labda mpaka uwe na pesa nyingi ndio ujenge. Ukiamua hakuna kinachoshindikana, kama umeweza kujenga nyumba ya chini,jua una uwezo pia wa kujenga ghorofa. Fanya yafuatayo kutimiza ndoto zako:-
  • Weka kwenye michoro wazo la nyumba yako (jichoree mwenyewe unavyotaka)
  • Tafuta injinia akuandalie BOQ (idadi ya matirio yatakayotumika),michoro, na ramani
  • Tafuta kibali cha ujenzi- itategemea na eneo uliopo
  • Anza kununua mawe, kokoto nyeusi, mchanga, matofari ya kuanzia, nondo. simenti-kwa ajili ya msingi
  • Nenda maeneo yanapojengwa magorofa, na umchukue fundi unayemuona anapiga kazi
  • Ingia makubaliano na huyo fundi-akupatie gharama ya msingi, ikiwezekana mkubaliane kwa siku.
  • Anza kazi ya msingi.
  • Weka rafu/ zege kwenye msingi
  • Anza kupandisha nguzo na tofali kwa awamu awamu kutokana na mzunguko wako wa pesa- unaweza kumtumia yule fundi wa mwanzo au ukatafuta mwingine
  • Ukifika kwenye lenta-inabidi upumzike
  • Anza kukusanya nondo,kokoto nyeusi, simenti,misumari
  • Angalia pa kukodi 'plate' au 'marine board',kwa siku gharama yake huwa ni sh. 400/= kwa moja, pia kukodi mirunda, mbao; inategemea na sehemu ulipo.
  • Mwite fundi kwa kazi ya 'slab'- hapa ndipo huwa pagumu sana kwenye ghorofa
  • Akishamaliza slab, pumzika utafute nguvu
  • Endelea na ujenzi wa juu
  • Paua mjengo wako
  • Endelea na hatua zingine za 'finishing'
  • Baada ya hapo jipongeze....kwa kutembelea mbuga za wanyama
Dah, hiyo Item ya mwisho umenifurahisha sana. Nitaitendea kazi Mkuu.
 
Kumbe ilikuwa kubwa, nafikiri 50msq inakuwa ahueni
OKW BOBAN SUNZU hii slabu ya SQM 50 itakuwa na nini na nini kimfano (yaan bedroom ngapi, balcony? kwa mfano) na je umemaanisha eneo lote mpaka ukuta/kuta zinapopita ama? ni pasipo kuta? sure upo sahihi kwa ghorofa ukiweza kupunguza idadi ya SQM pia utapunguza gharama tatizo ni hapo ni kwa namna gani utapunguza hizo SQM na bado kwa mfano G1 upate let say 3 master bed rooms, balcony
 
7c71a5b23c8140e2ea186b0fd229346d.jpg

Asante mkuu
Idea ni isizidi SQM 50. Kuwe na minsitting room ft 10X8ft, bedroom ft 12Xft 14, dressing room ft 10X ft 6, bathroom ft 5X ft 6, staircase na balcony(au isiwepo kabisa. Pasiwe na mambo mengi. Imagine kitu kama hicho hapo juu
c.c mzabzab
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom