Hivi wauza nafaka wote hapa Dar ni kweli wote huagiza nafaka mikoani au wengi wao hununua tu kwa wauzaji wakubwa wa jumla?

aBuwash

Senior Member
Dec 26, 2023
118
215
Habari wana jf natumai wote mko poa

Hii habari inanishangaza kila kila ninapoenda kununa labda mchele au maharage kila mfanyabiashar nikimuuliza hizi unachukulia wapi huwa wananiambia wanachukulia mikoani afu ukute ana gunia tano tu au kumi

Nimezunguka maduka mengi ila wengi wao wananiambia tu hivohivo sasa leo wanajf naomba tuelezane ukweli hili jambo ni sahihi. Au ndo basi wanaficha tu hawataki mteja ajue wankochukua mzigo wao kwa hapa dar

Na ni kweli wafanyabiashara wa nafaka wengi wa dar mizigo huchukua mikoani. Namaanish hawa wa kawaida achana na wale wakubwa

Na kama wanachukua mikoani wanamudu vipi usafiri, ushuru, nk wakat mitaji yao inaonekan midg yani 5M kushuka chini

Noamba tuwekane sawa hapa jamani.
 
Wengi wanachkua mizigo Tegeta, Manzese, Magomeni, Tandika, Mbagala rangi 3. Kwenye Maduka ya jumla ya Nafaka
 
Back
Top Bottom