KERO Changamoto ya barabara kutoka Mlalo - Lushoto kipindi hiki cha mvua

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Ibn Algherey

New Member
Nov 29, 2023
2
1
Kuna changamoto kubwa ya barabara inayotoka Mlalo mpaka Lushoto hususani katika kipindi hiki cha mvua barabara zina mashimo makubwa nyingine hazipitiki kabisa kwa sababu ya matope ni wiki ya pili sasa, hili tatizo linasababisha nauli kupanda na wananchi kuto mudu hizo gharama, nauli mwanzo ili kuwa 6000 sasa hivi 10000 mpaka 12000

Barabara hiyo pia anatumia mbunge wa jimbo la Mlalo ambae inasemekana pia ni mwenyekiti wa tanroad mkoa lakini jitihada zimekuwa ni ndogo sana za kutatua hii changamoto
 
Hapo mbunge akiona uzi ndio labda atastuka. Zaidi ya yote atasema wewe ni mpinzani
 
Hapo mbunge akiona uzi ndio labda atastuka. Zaidi ya yote atasema wewe ni mpinzani
Hiyo barabara imefungwa kwa sasa lakini hakuna kinacho endelea iko barabara ya mchepuko juzi ilitaka kuuwa watu kutokana na ufinyu wa hiyo barabara
 
Back
Top Bottom