Waziri Mkuu Majaliwa ataka sheria kali ziundwe kukabiliana na Unyanyasaji wa Kijinsia

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,865
4,693
Serikali inatarajia kuweka sheria kali dhidi ya wanaofanya ukatili wa kijinsia kwenye Jamii ili kuondoa na kupungunguza wimbi la ukatili linaloendelea kwenye Jamii.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema hayo leo April 18,2024 wakati wa majibu ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Tunza Malapo aliyeitaka Serikali kupeleka muswada Bungeni wa kuongeza adhabu ama kubadili adhabu zitakazokidhi ili kuondoa matukio hayo.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema “kwakuwa nimekiri tatizo hilo lipo kwenye Jamii kwa baadhi ya maeneo hatua kali zinachukuliwa na inawezekana yanajirudia kwa baadhi ya maeneo ambayo yana sheria ambazo sheria zake sio kali sana kwasababu jambo hili ni mtambuka linagusa Wizara nyingi na kila Wizara inaweka sheria yake katika kukinga jambo hili”

“Tunapokea ushauri wa kufanya mapitio ya sheria hizi malengo yetu nu kuhakikisha Jamii inabaki kuwa salama na wale wote wanaotenda matendo yote ya ukatili wa kijinsia waendelee kuchukuliwa hatua kali na tunatamani jambo hili lionekane linakoma katika Jamii”
 
Back
Top Bottom