Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,317
- 113,946
Nimeona ona humu JF baadhi ya watu wanadai kuwa eti kipindi cha Rais Magufuli watu ambao hivi sasa wanamkosoa Rais Samia, hawakuthubutu kumpinga hadharani kama ambavyo wanampinga huyu mama yao.
Hilo si kweli. Rais Magufuli alipingwa sana na watu. Tena watu wa kada zote.
Kudai kuwa hawa wanaomkosoa Samia hivi sasa enzi za Magufuli walikuwa kimya, huko ni kulazimisha uongo na ni kujisahaulisha kiumakusudi tu.
Magufuli alipingwa na CCM wenzake na alipingwa hata na wabeba maboksi maskini kama mimi na ushahidi upo [risiti zipo].
Kwa mfuatiliaji yeyote yule aliye makini na ambaye hasukumwi wala kuendeshwa na hisia, ukweli huo ni dhahiri kabisa.
Sasa hawa wajulikanao kama ‘chawa wa mama’ [weirdos] ni watu ambao hawatumii akili katika majadiliano yoyote yale yamhusuyo huyo mama yao.
Wao ni hisia tu kwa kwenda mbele. Huwezi kufanya nao majadiliano yoyote yale yaliyo ya maana.
Kwao kila kitu ni ‘whataboutism’ [sijui Kiswahili chake] tu.
Hawana kabisa hoja. Na hawawezi kabisa kujenga hoja.
Ukihoji chochote kuhusu Samia, wao jibu lao ni ‘what about Magufuli’.
No one is above criticism and no one is below praise.
And anybody can get it. That includes Samia as well.
Just suck it up, buttercups.