KERO Wanafunzi 150+ wa Chuo cha IFM hawajalipwa fedha zao za Boom kutoka Bodi ya Mkopo na uongozi upo kimya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Baadhi ya Wanafunzi zaidi ya 150 hadi 180 hadi leo hawajapatiwa fedha zao za ‘boom’ la Kwanza (Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), walicheleweshewa boom mpaka ikafika wakati wa kusaini boom la pili.

Wanafunzi wakasaini malipo ya fedha ya mara ya pili wakati yale ya awamu ya kwanza hawakupata, umeshapita mwaka sasa bado wanafuatilia boom lao bila mafanikio.

Mwanzo wanaambiwa “pesa hazipo” mara “wasubiri” mara wengine wanaambiwa “pesa zisha sainiwa” na wakati mwingine wanasema “pesa zishaingizwa kwenye account zao za bank” ila wahusika ambao ni Wanafunzi hawazioni.

Ninachokiona kinachoendelea kuna ujanja unafanywa na viongozi wanaohusika na mikopo ya Wanafunzi Chuo cha IFM Dar es Salaam.

Wanafunzi ambao hawajapata fedha hizo ni wale wa walioanza masomo kwa mwaka 2023/24, kiasi ambacho kila Mwanafunzi anastahili kupata ni Sh 600,000, wakusaini ndio maana wana haki ya kuhoji kinachoendelea.

Wamefuatilia hadi Bodi ya Mikopo, huko majibu yakatoka kuwa wao walishamalizana na Chuo hivyo ni jukumu la chuo na hasa Loan Officer, ambaye naye akiulizwa anatoa sababu kibao ambao hazieleweki kama nilivyosema hapo juu.
 
Back
Top Bottom