Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,013
156,444
NAFASI YA MKRISTO KATIKA VITA YA ISRAELI NA PALESTINA.

Shalom.
Juzi Palestina kupitia wanamgambo wa Hamas wameanzisha mashambulizi juu ya Israel, na inasemekana ni mashambulizi makubwa kuwahi kushambulia na kufanikiwa kuwaua Waisraeli zaidi ya 300 na wengine zaidi 100 kujeruhiwa, idadi hiyo inahofiwa kuongezeka. Waziri mkuu Benjamin Netanyahu ametangaza vita rasmi.

Kufikia jana Israel amejibu mapigo na kuishambulia Palestina na kufanikiwa kuwaua wapalestina zaidi ya 313 na wengine 2000 kujeruhiwa na idadi inahofiwa kuongezeka.

Sasa kutokana na matukio hayo kumekuwa na mvutano mkubwa wa watu katika mitandao ya kijamii na hata Duniani, kila mmoja akiongea lake. Lakini mivutano yote hiyo kwa sehemu kubwa imejaa udini ambao unaelemea upande wa imani ya mtu husika. Wengine wanaongea kisiasa n.k.

Nami pia kwa upande wangu naomba niongee kidogo kuhusu jambo hili, na mimi nitaongea tu kwa upande mmoja wa kikristo tu. Siongelei siasa wala historia leo ila nitaongea kwa upande wa nafasi ya Mkristo mgogoro huu.

Nimebahatika kupitia maoni mengi ya Wakristo na baadhi ya watumishi, wanafurahia Israel kujibu mapigo kwa Palestina kwa kile wanachodai kuwa Palestina ndiyo walioanza. Hivyo tunaiombea Israeli ikiwezekana wawachape wafilisti mpaka maji wayaite m-ma.

Leo nataka niondoe mtazamo huo mfu katika akili za wengi, Palestina kuna Wakristo kama sisi, yawezekana kuna walokole kule, Wasabato, Wakatoliki n.k unafikiri wale Wakristo wakule wanapoomba Mungu huwa wanaombaje? Je wanaiombea Israel iwapige wapalestina au Palestina iwapige Waisraeli? Ukilitambua hilo utaanza kunielewa.

Kristo alikufa msalabani kwa ajili ya Kanisa na si taifa la Israel, narudia Kristo alilifia kanisa na si taifa la Israel pale msalabani. Hivyo tambua kitu cha thamani kwa Kristo kwa sasa ni kanisa kuliko taifa lolote, yani kwake kanisa ni zaidi ya mataifa yote ulimwengu. Na zaidi ya yote kanisa ni mwili wake yeye mwenyewe, hivyo sote tu viungo katika mwili wake.

Kwa kulitambua hilo hilo Mkristo hakutakuwa kufurahia hii vita na vifo vinavyotokea huko Palestina, kama ambavyo waislamu wengi wanavyofuhia vifo vya huko Israeli. Mkristo anapaswa kuiombea Palestina kwa namna ya anavyoiombea Israel kwa sababu nchi zote zina ndugu zetu, yaani watoto wa Mungu ambao tunaungana nao katika mwili wa Kristo.

Wayahudi wengi kama ilivyo kwa wapalestina hawamtaki Kristo, wamemkataa, na kuweka sheria kali kwa ndugu zao wanaotamani kukata shauri, wengi wanajua Israeli ni nchi ya Kikristo lakini si kweli. Wakristo wengi hubaki katika andiko la kitabu cha

Hesabu 24:9
Aliinama, akalala mfano wa simba,
Na kama simba mke; ni nani atakayemstusha?
Na abarikiwe kila akubarikiye,
Na alaaniwe kila akulaaniye.

Tunaamini kwamba baraka zitapatikana kwa kuibariki Israeli hata katika machafuko, maana tutakapoilaani tutalaaniwa. Ndugu zangu baraka ya pekee ni kuwa na Kristo tuu, hatuna baraka nyingine iliyobakia. Sisi kanisa ni wakuu kuliko Israeli hivyo kazi yetu ni kuupatanisha ulimwengu na Mungu. Ulimwengu ni pamoja na Israeli wenyewe na Palestina, tutawaombea amani katika wakati kama huu na wokovu wa Mungu kwa sababu wengi wanaokufa hawana Yesu.

Hiyo ndiyo nafasi ya kanisa iliyobaki katika taifa la Israel, tuachane na Siasa na udini. Wote tunajua Palestina hawamuwezi myahudi na tunajua kinachotokea ni wapalestina kupigwa, ila mgogoro huu kwa kadri siku zinavyozidi huchochewa na itikadi kubwa ya udini na mwisho kuzidi kushika kasi Duniani. Mungu hafurahii mauaji.
 
Amani nawaachia!
 
Back
Top Bottom