Utafiti wa Mwananchi ni matokeo ya ombwe la utafiti halisi wa maoni ya wananchi

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
38,019
46,841
Kabla ya utawala wa awamu ya tano kuingia madarakani kulikuwa na taasisi binafsi za utafiti zilizokuwa zinafanya utafiti wa masula ya kijamii kwa raia na kutoa matoke ya hapa na pale.

Waliokuwa wanafuatilia watazikumbuka Twaweza, IPSOS, Afrobarometer na REDET. Japo matokeo ya utafiti wa taasisi hizi yalikuwa yanashutumiwa vikali na wapinzani mara kadhaa lakini angalau vilikuwa ni vyombo bobezi katika eneo hilo la utafiti.

Baada ya awamu ya tano kuingia vyombo vyote hivyo vikapotelea mitini, ikabaki REDET ambayo ilikuwa ikifanya tafiti zilizokuwa na kila dalili ya upande mmoja. Likabaki ombwe kubwa la maoni ya wananchi kupitia utafiti halisi ambayo matokeo yake ni kama haya ya gazeti la Mwananchi kukurupuka na kuweka tafiti za mwendokasi zisizo kidhi vigezo.

Serikali ya CCM kwa nguvu kubwa ya kupitliza mlio nayo katika kudhibiti sekta ya habari, badala ya kuwashushia rungu mwananchi angalieni mlipojikwaa na sio mlipoangukia kwa manufaa ya taifa.

PIA SOMA
- Mwananchi waomba radhi baada ya wananchi wengi kupiga kura ya kutoridhishwa na sera za Uchumi za Rais Samia
 
Utafiti wa mwananchi hauna kosa lolote.ni ukweli mtupu.huyu mama Yao katuharibia nchi.alikuta sukari 1600kg lakini Kwa Sasa ni 5500/kg,petrol ilikuwa 1500/Lita lakini Kwa Sasa ni 3257 Kwa Lita,miradi mingi imesimama lakini yeye Kila kukicha anapaa hewani Kwa kutudanganya kuleta wawekezaji.
 
Kabla ya utawala wa awamu ya tano kuingia madarakani kulikuwa na taasisi binafsi za utafiti zilizokuwa zinafanya utafiti wa masula ya kijamii kwa raia na kutoa matoke ya hapa na pale.

Waliokuwa wanafuatilia watazikumbuka Twaweza, IPSOS, Afrobarometer na REDET. Japo matokeo ya utafiti wa taasisi hizi yalikuwa yanashutumiwa vikali na wapinzani mara kadhaa lakini angalau vilikuwa ni vyombo bobezi katika eneo hilo la utafiti.

Baada ya awamu ya tano kuingia vyombo vyote hivyo vikapotelea mitini, ikabaki REDET ambayo ilikuwa ikifanya tafiti zilizokuwa na kila dalili ya upande mmoja. Likabaki ombwe kubwa la maoni ya wananchi kupitia utafiti halisi ambayo matokeo yake ni kama haya ya gazeti la Mwananchi kukurupuka na kuweka tafiti za mwendokasi zisizo kidhi vigezo.

Serikali ya CCM kwa nguvu kubwa ya kupitliza mlio nayo katika kudhibiti sekta ya habari, badala ya kuwashushia rungu mwananchi angalieni mlipojikwaa na sio mlipoangukia kwa manufaa ya taifa.
But hayo ndo mayokeo, mbona mnayakataa? Juzi tu mmeyakubali matokeo ya uchaguzi😁😁😁😁😁
 
Back
Top Bottom