UTAFITI: Makosa ya Lugha kupitia BBC SWAHILI

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,765
4,145
Kuanzia nafanya utafiti jinsi Lugha ya Kiswahili inavyaondikwa kimakosa katika mtandao wa bbc swahili

Mfano leo wameandika

Mamilioni ya watuwenye umri wa makamo wameongozwa kimakosa kuamini kuwa wao si wanene, kulinganana utafiti wa Kiitaliano ambao uliangalia mafuta ya mwili badala ya uzitounaohusiana na urefu.

Kutumia njia mpya ya kupunguza unene wa kupindukia kungetoapicha halisi ya nani ameathirika, watafiti wanasema.

Kwa umri, misuli hupungua na mafuta huongezeka karibu naviungo katika eneo la kiuno, mara nyingi bila mabadiliko katika uzito.

Changamoto nikupata zana ambayo inachunguza kwa urahisi unene.

Nimejitolea kufanya utafiti huu usiarasmi ili kulisaidia shirika kubwa la habari linavyoandika lugha adhmu ya kiswahili kimakosa.

Matokeo ya utafiti nitauachipisha hapa

UPDATE LEO 16/5/2024
WAPI WAMEKOSEA NA WALIKUWA WANATAKIWA WAANDIKE VIPI?

1. Putin akutana na Xi Jinping, vita vya Ukraine vyagubika ziara hiyo​

Kosa: Bila shaka, vita vya Ukraine huenda ikajadiliwa inaweza.
Usahihi: Bila ya shaka vita vya Ukrain ni miongoni mwa maswala yanaoweza kujadiliwa katika kikao hicho
Kosa: Wakati huo huo Xi anaweza kutafuta maelezo mafupi kutoka kwa Putin juu ya mkakati wa Urusi ni nini nchini Ukraine na labda pia hakikisho
Usahihi: wakati huo huo xi anaweza kupata maelezo mafupi kutoka kwa .........
 
Lugha ni tatizo sana ,kuna kuchapia kwa kutokujua au slip of the tongue.

Kinachokatazwa ni kubananga tu.
 
Kuanzia nafanya utafiti jinsi Lugha ya Kiswahili inavyaondikwa kimakosa katika mtandao wa bbc swahili

Mfano leo wameandika

Mamilioni ya watuwenye umri wa makamo wameongozwa kimakosa kuamini kuwa wao si wanene, kulinganana utafiti wa Kiitaliano ambao uliangalia mafuta ya mwili badala ya uzitounaohusiana na urefu.
Kwahio unaongelea hio typo au hata mtiririko wa maneno hauleti maana kwa haraka ? Kama ni typo basi mkuu all I can say is......
Nimejitolea kufanya utafiti huu usiarasmi ili kulisaidia shirika kubwa la habari linavyoandika lugha adhmu ya kiswahili kimakosa
Matokeo ya utafiti nitauachipisha hapa
A Pot calling a Kettle Black.....
 
Kiswahili cha Kenya hicho tuwe wapole ukimsikiliza yule mtoa taarifa za Congo DRC kutoka Goma nae anaongea Kiswahili cha Congo ya Mashariki.
 
Mtafiti mwenyewe unaandika lugha kimakosa, je, utawezaje kutafiti makosa ya wenzako?.

Mfano wa makosa katika uandishi wako:
i) Lugha badala ya lugha
ii) Aya ya kwanza haina nukta
iii) Umesahau nukta pacha baada ya aya ya kwanza
iv) watuwenye badala ya watu wenye
v) Usiarasmi badala ya usiyo rasmi
vi) Adhmu badala ya adhimu
vii) Hujaweka nukta kwenye sentesi ya mwisho.
 
Lugha ni tatizo sana ,kuna kuchapia kwa kutokujua au slip of the tongue.

Kinachokatazwa ni kubananga tu.
Kwa Taasisi kubwa hio sio excuse hawakatazwi kuajiri proof reader.., kukosea wote tunakosea kuacha kosa liendelee kuwepo inaonesha kukosa Umakini..., Sasa kama mtu anayenilisha Habari sio Makini inaweza pelekea kutokuamini anachonilisha....
 
Nilikuwa namsikiliza huyu daktari Mkongo anayeongelea athari za uvutaji sigara. Yeye anaita moyo roho. Kamaliza kuelezea mtangazaji hajaweka sawa kosa lolote la kilugha. Ila hawa ni VOA sio BBC
 
Kwahio unaongelea hio typo au hata mtiririko wa maneno hauleti maana kwa haraka ? Kama ni typo basi mkuu all I can say is......

A Pot calling a Kettle Black.....
Hakuna neno ''kwahio'' wala ''hio'' kwenye kiswahili. Shule za sasa ni janga kuu!
 
Kuanzia nafanya utafiti jinsi Lugha ya Kiswahili inavyaondikwa kimakosa katika mtandao wa bbc swahili...
Kwanini BBC wakati vyombo vyote vya habari viswahili vyao ni vibovu, na humu JF ndiyo usiseme(husiseme). Tatizo la kiswahili linaanzia shuleni ambako walimu hawajui(awajui) kiswahili, wizara ya elimu huwa(uwa) hawaoni tatizo kwenye kiswahili kibovu.
 
Hakuna neno ''kwahio'' wala ''hio'' kwenye kiswahili. Shule za sasa ni janga kuu!
Unaongelea hakuna hilo neno wakati nimeliweka na nimelitumia au ni nini maana ya neno ? na hapo nilipoandika nimeweka maneno typo, na all I can say..., au na hayo ni kiswahili au unadhani hapa naandika thesis au na mimi ni Broadcasting Company....
 
Mtafiti mwenyewe unaandika lugha kimakosa, je, utawezaje kutafiti makosa ya wenzako?.

Mfano wa makosa katika uandishi wako:
i) Lugha badala ya lugha
ii) Aya ya kwanza haina nukta
iii) Umesahau nukta pacha baada ya aya ya kwanza
iv) watuwenye badala ya watu wenye
v) Usiarasmi badala ya usiyo rasmi
vi) Adhmu badala ya adhimu
vii) Hujaweka nukta kwenye sentesi ya mwisho.
kuna typing errors na kuandika lugha isiofahamika. kwa mfano:
Ametangaza hayo baada ya kubaini kwa uhakika kuwa wawilikati yao walikuwa bado wanatafutwa pia nao waliaga dunia.

Chombo hiki kinachojulikana kama International ResidualMechanism for Criminal Tribunals (IRMCT) kilitangaza kwamba uchunguzi wake"ulipata ushahidi" kwambawaliokuwa wamesali wote wawili Ryandikayo na Charles Sikubwabowalifariki mwaka 1998.
 
BBC hawaandiki habari Kwa kiswahili, wao huandika habari Kwa kiingereza Kisha mashine zinabadili taharifa hiyo Kwenda lugha zote kuu Duniani, hapo tatizo lipo kwenye translators zao.
 
Back
Top Bottom