SI KWELI Ukihisi harufu ya wali au mchele uwapo porini ni ishara kuwa Chatu yupo karibu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Habari,

Kumekuwa na hoja mtaani inadai kwamba ikitokea upo porini na ukahisi harufu ya wali au mchele unapaswa kuchukua tahadhari kwani ni ishara kuwa chatu yupo karibu na anatoa harufu hiyo kukuvuta.

Je, kuna ukweli kuhusu hoja hii? Tunaomba ufafanuzi.

1713444598154.png
 
Tunachokijua
Chatu ni aina mojawapo ya nyoka ambayo ni wakubwa kiumbo. Tofauti na aina nyingine za nyoka, chatu hawatoi sumu (ni nyoka wasio na sumu). Chatu wanaishi katika maeneo ya kitropiki ya Afrika na Asia. Wanaweza kupatikana katika misitu ya mvua, savanna na jangwa.

Kama alivyouliza mleta mada hii, kumekuwa na hoja ya kijamii inayodai kwamba Chatu chatu ana harufu ambayo anaitumia kuvutia mawindo yake. Baadhi ya simulizi zinadai na kutahadharisha kwamba uwapo porini na kusikia harufu ya wali au chakula basi unapaswa kukaa mbali kwani ni ishara kwamba Chatu yupo karibu. Hoja inayofanana na hii pia imewahi kuletwa ndani ya JamiiForums (Soma Hapa) ambapo Mwanachama Mshana Jr alikuwa akieleza namna ngozi ya Chatu ilivyo na nguvu ya kumpumbaza na kuvuta Mbwa kujipeleka mwenyewe.

Je kuna ukweli wowote kuhusu madai haya?

JamiiCheck imefuatilia madai haya kwa kufanya mawasiliano na Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA), Beatus Maganja na
Mhifadhi na Mkufunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Tito Lanoy ambao wote wanakubali kuwa nyoka anapojikoboa (kujivua) ngozi huwa kuwa na harufu fulani kama marashi lakini haifanani na wali.

akifafanua zaidi hoja hii, Beatus Maganga anaeleza kuwa hii inatokana na dhana za kijamii tu ambazo zimekuwa zikiaminika hivyo na kurithishwa katika vizazi na vizazi. Anasema:

Madai kuwa ukipita sehemu ukasikia harufu ya wali na kujua kwamba eneo hilo linahusiana na uwepo wa chatu au nyoka wakubwa si kweli.
Inawezekana wakati nyoka anajivua magamba huwa kuna harufu fulani labda watu watakuwa wanahusisha harufu hiyo na harufu ya wali lakini sidhani kama inatoa harufu ya moja kwa moja ya wali.
Kwa uzoefu wangu hiyo ni dhana tu na sio jambo la Kisayansi, ni stori tu zilizopita tangu enzi na enzi.
Kwa upande wake Tito Lanoy Mhifadhi na Mkufunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka anaeleza kuwa nyoka anapojikoboa ngozi yake hutoa harufu fulani isiyovutia 'Odor Smell' ambayo hutokana na majimaji anayotatoa wakati wa kujivua ngozi yake. Harufu hiyo hutofautiana kati ya nyoka mmoja na mwingine na huisha baada ya ngozi na majimaji hayo kukauka. Akifafanua zaidi hoja hii Tito Lanoy anasema:

Ni hivi inapofikia muda wa nyoka kujikoboa magamba yake kwa ajili ya kukua kuna majimaji ambayo yanakuwa kwenye magamba yake, yale majimaji huwa yanatoa harufu fulani ambayo hupotea baada ya kukauka. Na kuna mimea ambayo huwa na harufu hivyo mtu akisikia harufu ya mimea na akiona nyoka maeneo hayo anahisi ni harufu ya nyoka jambo ambalo sio kweli.
Harufu hiyo huwa ni mbaya na haifanani na wali kama inavyodaiwa. Maji hayo huitwa Lymphatic fluid ambayo nyoka hutoa na inamsaidia kutenganisha mwili wake na ngozi (Damis na Epidamis ya ngozi ya nyoka)ndiyo huwa na 'Odor smell' ambayo huisha kwa kadri ngozi hiyo inavyokauka lakini sio kwamba ukihisi harufu ya wali basi ni ishara kuwa nyoka yupo hapo.
1714210610851-png.2975198

Dhana hii inaweza kuwa imetokana na mtu aliyeona nyoka mahali labda akasikia harufu fulani na kudhani ni ya nyoka, hii dhana si ya kweli.

Mbwa na kumfuata Chatu mwenyewe
Tito Lanoy anaeleza kuwa suala Mbwa kudaiwa kumfuata chatu mwenyewe kuhusushwa na harufu sio sahihi. Mbwa humfuata chatu sababu chatu huweka mtego kwa kuchezesha mkia wake ambao humzubaisha na kumfanya Mbwa asogee mwenyewe.

1714210261593-png.2975190
Akisogeza karibu na mkia ndipo humvamia na kummeza. Kitendo hiki cha kutikisa mkia chatu hukitumia kama mbinu na uwezo wake wa kuwinda.

Hivyo, kutokaka na ufafanuzi huu kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya Wanyama JamiiCheck inaona hoja inayodai kuwa ukisikia harufu ya wali uwapo porini basi ni dalili kuwa Chatu yupo karibu haina ukweli.
Hiyo ni mitazamo ya kwenye jamii , maoni ya watu

~Lakini sayansi yenyewe je..?

Viumbe vidogo na vikubwa kwenye udongo (kama vile bakteria, minyoo); madini katika udongo (kama vile chuma, magnesiamu, phosphates); unyevu, maji na vitu vinavyooza kama vile majani, magome, wanyama waliokufa husababisha harufu tofauti za msitu

Moja ambayo inaweza kuwa ya mchele uliopikwa lakini kwa watu wengine wakapata harufu tofauti.

Aina ya harufu inayotolewa inategemea mambo kadhaa kama vile aina ya udongo, kitu kilichoozea ndani ya udongo
Bado maelezo yako hayajibu swali husika..!!
 
Hiii imani ipo sehemu nyingi. Hata mimi mara kadhaa nimeshapita maeneo nikasikia hiyo harufu ya wali. Kwangu mimi nadhani kuna mimea/miti ambayo huwa inatoa hiyo harufu. Nakumbuka kuna mmea mmoja huwa unatoa harufu ya maziwa ya mgando.
Angalau it makes sense. Kuna yale majani ukiyafikicha yanatoa harufu ya kinyesi..!! Enzi zetu za primary school, tulikuwa tunayafikicha na kuyarushia staff room..!! au ofisi ya mwalimu mkuu kabisaaa..!!
 
Ni kweli...chatu anakuwa anavua ngozi yake ya nje....lakini siyo kwamba anakuwa anakuvutia
 
Kuna siku katikati mapori huko turiani na muheza nikaskia hiyo harufu nilitoka mbio balaa mpaka kijiji kingine maana nilijua tu hii balaa.
 
Habari,

Kumekuwa na hoja mtaani inadai kwamba ikitokea upo porini na ukahisi harufu ya wali au mchele unapaswa kuchukua tahadhari kwani ni ishara kuwa chatu yupo karibu na anatoa harufu hiyo kukuvuta.

Je kuna ukweli kuhusu hoja hii? Tunaomba ufafanuzi
actually,
sio porini pekee, na sio kwa chatu pekeyake, hata nyoka wa aina nyingine, mathalani yupo ndani ya nyumba yako, akiwa amejikoboa magamba yake hunukia mithili ya mchele uliolowekwa au wali, na wakati huo hujaloweka wala kupika wali ndani kwako..

Ile harufu sio tu kwajili ya kuvutia wanyama wengine tu, bali pia ndio harufu yake baada ya kujivua gamba la zamani...

Na hiyo harufu inakujulisha au kuashiria eneo ulilopo kuna nyoka Jirani na wewe 🐒
 
actually,
sio porini pekee, na sio kwa chatu pekeyake, hata nyoka wa aina nyingine, mathalani yupo ndani ya nyumba yako, akiwa amejikoboa magamba yake hunukia mithili ya mchele uliolowekwa au wali, na wakati huo hujaloweka wala kupika wali ndani kwako..

Ile harufu sio tu kwajili ya kuvutia wanyama wengine tu, bali pia ndio harufu yake baada ya kujivua gamba la zamani...

Na hiyo harufu inakujulisha au kuashiria eneo ulilopo kuna nyoka Jirani na wewe 🐒
Mmmh ya kweli haya?
 
Huyo afisa pori kwa maelezo yake nae hajui. Pia kwa JF kuhitimisha kuwa sio kweli hawako sahihi. Wapo jamaa wachana mbao porini. Wanathibitisha kuwa ni nyoka huwa kavua gamba ndio unasikia hivyo.
 
Hajanishawishi kisayansi huyo mtu wa TAWA,waulizwe na watafiti wengine huyu kajibu kisiasa
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom