Tunachokishuhudia Kenya si maandamano ya amani bali ni vurugu na uhalifu

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,294
7,863
Maandamano ya tarehe 20/3 tulishuhudia maduka yakivunjwa na waandamanaji na kupora mali za watu, tumeshuhudia magari yakichomwa moto, matairi yakichomwa barabarani vurugu tupu.

Juzi trh 27/3, Tena tumeshuhudia makanisa na misikiti ikichomwa moto na waandamanaji, lakini pia shamba la Rais mstaafu likivamiwa na kupora mali.

Haya matatizo yote ya uharibifu wa mali za watub yamesababishwa na jeuri ya Raila na genge lake kwa kulazimisha maandamano yenye vurugu, endapo Raila asinge lazimisha maandamano hluharibifu usingentokea.

Tumeshuhudia wandamanaji wakiwa wamebena mapanga, marungu mawe na silaha za kijadi, sasa hayo ni maandamano ya kidemokrasia?

Wakenya lazima watambue kuwa maandamano yanayo fanywa na Raila sio ya amani kama anavyo dai bali yana lengo la kufanya vurugu na uhalifu kwa mali za raia.

Mali zilizo haribiwa sio za Rais mstaafu tu bali mali za raia wengine pia zimeharibiwa lakini pia msikiti na kanisa vimechomwa moto, gari la Polisi limechomwa moto.

Kama tatizo ni kupanda kwa gharama za maisha, Bunge la wananchi lipo kwenye kikao linao uwezo Wa kujadili hali hiyo na kuishauri Serikali Cha kufanya, sio mandamano ya vurugu.

Raila akatazwe kuitisha maandamano vinginevyo Kenya inataingia kwenye machafuko makubwa.
 
Ni maandamano ya amani ambayo serikali imejizatiti kuyavuruga:

Raila says protests still on, condemns ‘state’ violence

Tunachoshudia ni vurugu za serikali kama zile zetu zama za giza. Zama za wasiojulikana au zama za hawa ndugu wakiranda randa kama ma-tai:

Fr_7Zw0WcAAavRN.jpeg

Cc: Proved, Rabbon
 
Ni maandamano ya amani ambayo serikali imejizatiti kuyavuruga:

Raila says protests still on, condemns ‘state’ violence
Maandamano ya amani yenye lengo la kwenda kuvamia Ikulu?

Raila aliwahamasisha wandamanaji wakitoka kcc waelekee Ikulu na walipo zuiwa wakaanza kuvunja na kuchoma mali za watu, sasa kweli hiyo ndio demokrasia? Au vurugu?

Wameamua kuto kuzitii Sheria walizo zitunga wao wenyewe.

Bei ya sembe haiwezi kushuka kwa vurugu bali kupitia Bunge la wananchi.
 
Maandamano ya amani yenye lengo la kwenda kuvamia Ikulu?!!!

Raila aliwahamasisha wandamanaji wakitoka kcc waelekee Ikulu na walipo zuiwa wakaanza kuvunja na kuchoma mali za watu, sasa kweli hiyo ndio demokrasia? au vurugu?

Wameamua kuto kuzitii Sheria walizo zitunga wao wenyewe.

Bei ya sembe haiwezi kushuka kwa vurugu bali kupitia Bunge la wananchi.

Tofautisha kwenda ikulu na kuvamia ikulu mawili hayo ni mambo tofauti sana.

Zingatia kwenye nchi ya wananchi ikulu ni nyumba ya wananchi na kila mwenye jambo anaruhusiwa kulifikisha huko.

Tofautisha katiba za wananchi na katiba za walamba asali na wahuni zenye kushabikiwa na wale vijana wa hovyo.
 
Watu wanaandamana halafu wanaharibu miundo mbinu na Kuvunja maduka na kupora Mali za watu hapo inatakiwa atokee mtu mmoja kama Rambo ajitoe muhanga amwage risasi kama Elfu Kumi hivi ili hicho kizazi Cha fujo na vurugu kiishe nchi iwe shwari. Pumbavu kabisa. Vita Ikitokea Kenya hata Hicho chakula wanachosema kimepanda Bei halitakuwepo kabisa. Njaa itakua kubwa sana.

Amani haiji ila Kwa ncha ya upanga.
Nchi kama China au hata Marekani wasingekua na misimamo mikali kwenye baadhi ya mambo ungekuta Leo hii Marekani imegawanyika na kuwa vinchi vingi au China ingekua ni viande vipande na kuuana Kwa vita. Suala Raila kuvuruga nchi lisichukuliwe kirahisi. Huyo mtu ashughulikiwe ipasavyo.

Mtu anaitisha maandamano makubwa watu wataharibiwa Mali zao halafu wewe unatafuta umaarufu Kwa ajili ya maslahi yako. Hapana !! Lazima uchezee kichapo kikali na Mali zako kuwa za kwanza kuharibiwa kabisa.

Hivi mfano wanachama wa Ruto nao wakiamua kuandamana kupinga vurugu za Raila itakuaje. !!

Uchaguzi ulipita na Ruto ndio Rais basi aheshimiwe na sio vinginevyo.

Raila anajivunjia heshima
 
Ninakazia:

"Mr Odinga, who is expected to lead his third anti-government demonstration tomorrow, accused President Ruto and his deputy Rigathi Gachagua of sponsoring the invasion of “people’s lands and businesses”, but he did not provide evidence of his claims."

Hapo nini usichoelewa ndugu? Au hadi ukumbushwe kwa picha kuwahusu nduguzo hawa?

Fr_7Zw0WcAAavRN.jpeg

Kenya wako hapo sasa na watu wasiojulikana.

Hapo ndipo nasi tulikuwa.
 
Tofautisha kwenda ikulu na kuvamia ikulu mawili hayo ni mambo tofauti sana.

Zingatia kwenye nchi ya wananchi ikulu ni nyumba ya wananchi na kila mwenye jambo anaruhusiwa kulifikisha huko.

Tofautisha katiba za wananchi na katiba za walamba asali na wahuni zenye kushabikiwa na wale vijana wa hovyo.
Unatakiwa utofautisha unapo taka kwenda chooni na kwenda Ikulu.

hata kama Ikulu ni ya wananchi lakini huwezi kwenda kama unavyo kwenda chooni............

Katiba ya wananchi inapaswa iheshimiwe na wananchi wenyewe sio waramba asali.
 
Hao hawaendi chooni nfiyo maana wametoa taarifa ya ujio wao hata wewe unaijua
 
Tofautisha kwenda ikulu na kuvamia ikulu mawili hayo ni mambo tofauti sana.

Zingatia kwenye nchi ya wananchi ikulu ni nyumba ya wananchi na kila mwenye jambo anaruhusiwa kulifikisha huko.

Tofautisha katiba za wananchi na katiba za walamba asali na wahuni zenye kushabikiwa na wale vijana wa hovyo.
haipo hiyo duniani, uende ikulu kiholela tuuu??!!!?? haipo hiyo nchi ya kufikirika
 
Umeelewa utaratibu wa kwenda kwenye majengo ya umma unaoongelewa na Raila ambao uko kikatiba?

Jielekeze kwenye hoja badala ya kubambia bambia kwenye mada.
 
NDUGU YANGU wanasiasa wakiwa majukwaani wanajitahidi sana kudanganya wananchi, eti katiba inasema hivi, lakini nenda kwenye sheria pia zinasema vipi kuhusu usalama hasa wa rais, kuna nchi hapa majuzi rais alivamiwa ikulu na wananchi hakuna nchi itaruhusu jambo hilo litokee hata ikiwa na katiba nzuri vipi.
 
Back
Top Bottom