TP Mazembe waomba kufundishwa football management na Yanga

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
16,216
25,002
“Tumepokea ugeni mzito kutoka moja ya Klabu kubwa Barani Afrika, TP Mazembe ya DR Congo ambao wamevutiwa na namna Klabu yetu ya Yanga inavyoendeshwa hivyo wamekuja hapa Tanzania kujifunza mambo mbalimbali kwenye Mfumo wetu wa Mabadiliko ya Uendeshaji" Simon Patrick, Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga SC.
---

Pia tutakuwa na makubaliano rasmi ya urafiki wa kushirikiana kati ya Klabu yetu ya Yanga na TP Mazembe ili kuweza kubadilisha ujuzi wa mambo mbalimbali ya kimpira yatakayoweza kuisaidia Klabu yetu.

Klabu kubwa kama TP Mazembe imesafiri kutoka DR Congo kuja hapa Jangwani kujifunza kwa kichwa chetu, Rais wetu Eng. Hersi Said halafu kuna watu wako nyumba ya 16 tu jirani hapo, wanapiga kelele kuwa hawana cha kujifunza kwa Yanga. Niwaambie tu, tutabeba Makombe hadi kila Mwanachama atakuwa anabeba la kuweka nyumbani kwake

#timuyawananchi
#daimambelenyumamwiko

Je Kuna ukweli kuwa Yanga ndio workshop ya soka hapa Afrika???
 
“Tunafuraha kubwa kufika hapa, ni heshima kubwa kwetu na tumefurahi kwa mapokezi mazuri mliyotupatia, tumekuja hapa kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Yanga na kutengeneza urafiki mzuri utakaoweza kuvisaidia vilabu vyetu hivi viwili bora Afrika Mashariki na kati hivi sasa" Frederic Kitengie, CEO TP Mazembe.

#timuyawananchi
#daimambelenyumamwiko
1715698400725.jpg
 
Kweli penye miti mingi hakuna wajenzi......

Simba management yao mbovu .....lkn hawataki kuomba kufundishwa na Yanga

Tp mazembe kutoka mbali .....ndio wameiona hii dhahabi adimu kuja kufundishwa na Yanga
 
Dah hao Tp nao mafala sasa unakuja kujifunza kwa mtu ulie mpita kimaendeleo ...au wameletwa na GSM.Kama kweli wamekuja kujifunza yanga itakua ni kichekesho.
TP Mazembe iliwagharimu muda gani kufikia maendeleo hayo ikiwa kama kampuni?

2021 GSM investment : 2023 Success = CAFCCL Final & 2024 CAFCL Quarter Final with consecutive NBC PL trophies 3 times, FA Cup 2021/2022 & 2022/2023 and continuing to chase FA Cup 2023/2024.

Big investment with a lot success in the short time period.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Back
Top Bottom