Tofauti kati ya kesi za jinai na madai

Abdul S Naumanga

JF-Expert Member
Jan 28, 2024
204
310
millardayo-20240516-0002.jpg

Anayedaiwa kulala na kula Serena kisha kutokomea aachiliwa huru

Habari wana jamvi, awali ya yote nimesikitishwa sana na habari tajwa hapo juu👆 kwani nimejiuliza, je kama menager wa hoteli kubwa kama serena na team yake wameshindwa kung'amua tofauti iliyopo kati ya kesi za jinai na madai, sasa itakuaje kwa raia wenzangu wakawaida kabisa🤔? Japo suala hili nimewahi kuligusia katika Thread: Uelewa wa masuala ya kisheria ni mdogo sana Tanzania.. Lakini limenisukuma kuandika tena uzi huu ili uwe faida kwa umma juu ya tofauti kati ya aina mbili izi za kesi.
ANGALIZO
Taarifa zilizotolewa hapa zinakusudiwa kwa madhumuni ya elimu pekee na siyo ushauri wa kisheria. Juhudi zimefanyika kuhakikisha usahihi, lakini yaliyomo hayapaswi kutegemewa kama mbadala wa ushauri wa kitaalamu wa kisheria. Hivyo, ushauri kutoka kwa mtaalamu wa sheria mwenye sifa unapendekezwa kwa mwongozo zaidi.​

Tukianza na Kesi za jinai, hizi ni zile zinazohusisha makosa ambayo yameainishwa kisheria kuwa ni kinyume na maslahi ya jamii au nchi kwa ujumla. Makosa haya yanaweza kuwa ni pamoja na wizi, mauaji, ubakaji, na mengineyo.

Matokeo ya kesi za jinai mara nyingi ni adhabu kama vile kifungo jela, faini, au vyote viwili kwa pamoja. Japo sio mara zote ila mara nyingi kesi hizi huendeshwa na serikali kupitia ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) ambapo mwendesha mashtaka wa serikali anasimama kama mlalamikaji dhidi ya mtuhumiwa.

Mambo ya muhimu kuyafahamu kuhusu kesi za jinai ni pamoja na;​
  1. Asili na Madhumuni: Kesi za jinai zinahusu uvunjifu wa sheria za jinai, ambapo kitendo kinachodaiwa kufanywa ni kosa la jinai lililotajwa na sheria. Madhumuni ya kesi za jinai ni kulinda jamii dhidi ya tabia zinazovuruga amani na utulivu, na kutoa adhabu kwa wahalifu ili kuzuia makosa ya baadaye.​
  2. Wahusika wakuu: Mara nyingi mhusika mkuu ni serikali, inayowakilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) au vyombo vingine vya serikali kama polisi. Serikali inasimamia kesi dhidi ya mshtakiwa (mtuhumiwa) na mtendewa kosa (victim) atakua shaidi tu.​
  3. Mchakato wa Kesi: Kesi za jinai huanza na uchunguzi wa polisi, kukamatwa kwa mtuhumiwa, na mashtaka kupelekwa mahakamani. Mtuhumiwa anapopelekwa mahakamani, anashtakiwa kwa kosa maalum la jinai na kesi hufanyika kwa kuzingatia ushahidi uliokusanywa na upande wa mashtaka.​

View: https://youtu.be/EG_-qZMvd-0?si=oEZbAPpZI0ruvIWT
4. Kiwango cha Ushahidi: kiwango cha ushahidi katika kesi za jinai ni juu zaidi, ambapo upande wa mashtaka lazima uthibitishe kosa "pasi kuacha shaka yoyote ya kawaida" (beyond reasonable doubt).
5. Adhabu: Adhabu katika kesi za jinai inaweza kuwa kifungo gerezani, faini, huduma za jamii, au adhabu nyingine zilizotajwa kisheria kama vile kunyongwa kwa makosa makubwa kama mauaji.​

images (73).jpeg
Kwa upande mwingine, kesi za madai ni zile zinazohusiana na migogoro baina ya watu binafsi au taasisi ambapo upande mmoja unadai haki kutoka kwa mwingine. Hii inaweza kujumuisha masuala kama vile migogoro ya ardhi, mikataba, fidia za ajali, na kadhalika. Lengo la kesi za madai ni kupata haki au fidia kwa yule aliyeathirika. Kesi hizi zinaendeshwa na mlalamikaji binafsi, na siyo serikali.

Kama ilivyo kwenye jinai, hata kwenye madai ni muhimu kutambua yafuatayo;​
  1. Asili na Madhumuni: Kesi za madai zinahusu migogoro kati ya watu binafsi au vyombo vya kisheria kuhusu haki au wajibu wa kisheria. Madhumuni ni kutafuta haki na fidia kwa mtu aliyeathiriwa kutokana na kitendo cha mtu mwingine au chombo cha kisheria.​
  2. Wahusika wakuu: Wahusika wakuu ni mtu binafsi au taasisi inayodai kuathiriwa (mdai) na mtu binafsi au taasisi nyingine (mdaiwa).​
  3. Mchakato wa Kesi: Kesi za madai huanza kwa mdai kuwasilisha madai mahakamani dhidi ya mdaiwa. Mahakama husikiliza ushahidi kutoka pande zote mbili (mdai na mdaiwa) na kufanya uamuzi kulingana na ushahidi uliotolewa.​

View: https://youtu.be/YHw9KWnFaPQ?si=UV-xbGER4waDJX3G
4​
. Kiwango cha Ushahidi
: Kiwango vya ushahidi katika kesi za madai ni chini kuliko za jinai, ambapo mdai anatakiwa kuthibitisha madai yake "kwa mizani ya uwezekano" (balance of probabilities).​
5.​
Adhabu: Matokeo ya kesi za madai kwa kawaida ni fidia ya fedha kwa mdai, maagizo ya mahakama kama vile zuio (injunctions), au amri nyingine za kurejesha haki au kuzuia kitendo fulani.​

Kwahiyo, tofauti kuu kati ya kesi za jinai na madai ni nani anayeendesha kesi na lengo la kesi. Katika kesi za jinai, serikali ndiyo inaendesha kesi na lengo ni kuadhibu kwa kifungo au faini, wakati katika kesi za madai, mlalamikaji binafsi ndiye anayeendesha kesi na lengo ni kupata fidia au haki.​
 

Attachments

  • images (73).jpeg
    images (73).jpeg
    11.2 KB · Views: 2
  • Thanks
Reactions: K11
Hv mtumish (kiongoz) wa taasisi akiwa ametumia pesa ya taasisi kwa maslai yake huyu hushitakiwa ki jinai au madai?

Na kama jinai na unakuta amepigwa fain ya million 3 wakat alitumia zaid ya million 5 kwenye tĂ asisi hilo lipoje na kwann ata hyo faid ya million 2 haijarudishw kwenye taasisis husika(tasisi ni ya serikali inatoa huduma kwa jamii)
 
Hv mtumish (kiongoz) wa taasisi akiwa ametumia pesa ya taasisi kwa maslai yake huyu hushitakiwa ki jinai au madai?
Hii ni jinai ndugu, na kama ni mtumishi wa serikali apo anaweza kuwa na kosa zaidi ya moja. Inaweza kuwa wizi kinyume na kifungu namba 270 cha Kanuni za Adhabu (penal code) na atawajibika kwa kifungo cha miaka kumi na nne jela pale akutwapo na hatia
Screenshot_20240516-022511.jpg


Lakini pia inaweza kuwa kosa la matumizi mabaya ya madalaka kinyume na kifungu namba 96 cha Penal Code na iwapo atakutwa na hatia atawajibika kwa kifungo cha miaka mitatu jela.
Screenshot_20240516-022415.jpg


Mbali na hayo pia anaweza kushitakiwa kwa udanganyifu na uvunjaji uaminifu kinyume na kifungu namba 120 cha Penal Code na atawajibika kifungo cha miaka saba kama akikitwa na hatia.
Screenshot_20240516-022052.jpg

Na kama jinai na unakuta amepigwa fain ya million 3 wakat alitumia zaid ya million 5 kwenye tĂ asisi hilo lipoje na kwann ata hyo faid ya million 2 haijarudishw kwenye taasisis husika(tasisi ni ya serikali inatoa huduma kwa jamii)
Hapa sina jibu la uhakika la moja kwa moja, but for what I know adhabu ama hukumu katika jinai inaweza kuwa ya lazima ama hiari. Kwanza, ni muhimu kuelewa kwamba hukumu za lazima (mandatory sentences) ni zile ambazo mahakama haina budi kuzitoa kulingana na sheria iliyopo. Hii inamaanisha kwamba, mara tu mtu anapopatikana na hatia kwa kosa fulani, hakimu au jaji hana chaguo bali kutoa adhabu iliyowekwa kisheria bila kujali mazingira ya kipekee ya kesi hiyo au mtuhumiwa.

Kwa upande mwingine, hukumu za hiari (discretionary sentences) zinampa hakimu au jaji uhuru wa kutumia busara yake kulingana na mazingira ya kesi na sifa za mtuhumiwa. Hapa, mahakama inaweza kuzingatia mambo kama vile ushahidi uliotolewa, mazingira ya tendo la kosa, historia ya mtuhumiwa, na athari za kosa kwa jamii ili kuamua adhabu inayofaa.

Kwaio nadhani inawezekana io faini ilikua ni discretion ya hakimu au jaji kuamua hivyo, japo kwangu naona swala hili halijakaa sawa.​
 
Back
Top Bottom