Tatizo la Typhoid na UTI zinayojirudia mara kwa mara. Je upi ni mdadala wa dawa za Hospitali au nini kufanyike ili kuondokana na tatizo?

Asante mkuu, Vipi shida yako iliisha jumla?
Sijawahi kupata tena typhoid na vibandani nakula kama kawaida,,, zamani ilikua nikila vitu vya njiani lazima typhoid iibuke ila tokea kipindi hiko sijawahi kupata na nakulaga sana wale pweza wa njiani na pilipili zao
 
Sijawahi kupata tena typhoid na vibandani nakula kama kawaida,,, zamani ilikua nikila vitu vya njiani lazima typhoid iibuke ila tokea kipindi hiko sijawahi kupata na nakulaga sana wale pweza wa njiani na pilipili zao
Dawa yenyewe unaopata hata jina pengine nikawa specific kwa wahaya Ili wajue nataka nini?
 
Asante mkuu, naona changamoto yangu ngumu kidogo. Maana nimejaribu kufuata taratibu zote lakini bado nasumbuka tuu.
 
Wakuu naanza kwa salamu zangu za dhati kwenu pia poleni na mihangaiko ya siku nzima ya leo.

Kabla sijaenda kwenye maada. Naanza kwa kusema kuwa najiona kuwa na bahati sana kuwa katika jamii ya siri kama hii ambapo kila mmoja ana ...
Umejuaje una Typhoid na UTI?

Usiseme nilienda nikapima na kuambiwa nina Typhoid na UTI. Mara nyingi hizo huwa ni hospital fix, ni propaganda.

Ulipataje Typhoid na UTI?
Typhoid ni ugonjwa wa kuambukiza kwa kula au kunywa chakula au maji yenye kinyesi cha kutosha cha mgonjwa wa Typhoid. Hivyo jawabu ni kuzingatia kanuni za afya.

UTI kwa mwanaume ni jambo lisilowezekana kirahisi unless una matatizo ya kimaumbile kwenye njia ya mkojo au unajamiiana bila kinga na mwanamke mwenye gono.
 
Wakuu naanza kwa salamu zangu za dhati kwenu pia poleni na mihangaiko ya siku nzima ya leo.

Kabla sijaenda kwenye maada. Naanza kwa kusema kuwa najiona kuwa na bahati sana kuwa katika jamii ya siri kama hii ambapo kila mmoja ana uhuru...
kwanza pole sana aise,

Lakini pili,
ni kwamba lipo tatizo la msingi ambalo unapaswa kulitibu kwanza hilo, ndipo haya mengine yanaweza tubika na kwisha kabisa. 🐒

vinginevyo hali hiyo itakutesa sana kwa muda mrefu na athari za dawa unazotumia mara kwa mara zikasababisha changamoto nyingine za kiafya 🐒

nyongeza ila si kwa umuhimu.

kwa wanaume wanao piga punyeto UTI huonekana dhahir shaihiri.
Ikiwa yupo anaepiga punyeto basi jua ni kwamba ana UTI kamili,
Nyeto na UTI ni mapacha 🐒
 
Maji ya kunywa chemsha au nunua water gurd ,swala la typhoid utasikia Kwa jirani ,usile hovyo mtaani Kwa mama lishe ama matunda
 
UTI jitahidi Kila unapomaliza kujamiina na mwenza wako ukimbilie chooni ukakojoe na kujisafisha .
alafu kingine ungetuambia hizo dalili unazosikia mpaka uhisi una UTI o Typhoid na kukimbilia kupima.
Hiyo typhoid uwa una Pima kwenye hsptl za level gani isije kuwa maabara za mtaani au dispensary maana typhoid sio Kila hsptl Ina kibari cha kuipima sijui kwa nini..?!na ukipimwa inachukua muda gani kupata majibu..??
 
Wakuu naanza kwa salamu zangu za dhati kwenu pia poleni na mihangaiko ya siku nzima ya leo.

Kabla sijaenda kwenye maada. Naanza kwa kusema kuwa najiona kuwa na bahati sana kuwa katika jamii ya siri kama hii ambapo kila mmoja ana uhuru wa kutoa mawazo yake bila kuhofia kutambulika katika jamii husika kitu ambacho kimafanya watu wawe huru sana kutoa mawazo na maoni yao ya siri juu ya maada mbalimbali.

Paso na kupoteza wakati wenu naomba nianze na kuelezea hili swala ambalo naliona kama kero kwangu.

Nimekuwa nikisumbuliwa na Typhoid na UTI ambazo zinarudi tena muda mfupi ( makadirio ya mwezi mmoja au miwili) baada ya kutumia dawa za hospitalini. Hii shida sikuwahi kuwa nayo nilipokuwa mtoto lakini ni haki ambayo imejitokeza nikiwa mkubwa. Nakumbuka nilipokuwa mtoto nilikuwa nakunywa hata maji ya bombani bila shida yeyote, lakini hali ilibadilika nilipojiunga na advance. Hali hii imekuwa endelevu mpaka imekuwa kero kwangu.

Nimetumia dawa karibia zote zinazohusiana na Typhoid na UTI. Baada ya kutumia kidogo napona lakini baadae naanza kupata dalili tena.

Nafikia kipindi naogopa pengine matumizi yaliyozidi ya dawa za hospitalini yataleta athari kwenye ini au figo.

Naomba kwa aneyejua dawa za asili Ili nipate kuwa natumia pengine zikanitatulia hili tatizo langu.

Natanguliza Shukrani zangu kwenu kwa usaidizi mtakaonipatia.
Mkuu hakuna dawa za Hospitali zitakzo weza kukutibu hayo maradhi ya UTI na Typhoid nitafute mimi kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako uguwa pole.
 
Back
Top Bottom