- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Salaam,
Ndugu zangu kuna habari nimeona inasambaa kwa kasi Twitter ikidai kwamba Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limeshindwa kwenye kesi yake na IPTL -Independent Power Tanzania Limited.
Taarifa hiyo inadai TANESCO yashindwa kesi Marekani na kutakiwa kuilipa IPTL billioni 320!
Je kuna ukweli hapa?
Tazama mwenyewe:

- Tunachokijua
- JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa Taarifa hii imeibuliwa na ukurasa wa X (Zamani Twitter) ya Tanzania Abroad TV na kisha kuletwa na kuanza kusambaa kwenye mitandao mingine ya kijamii.
Je, ni kweli TANESCO wameshindwa kesi na wametozwa bilioni
JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa taarifa hii ni ya kweli lakini ilikuwa ni ya Septemba 19, 2016 ambapo ilitokana imetokana na uzi ulioletwa na Mwanachama wa JamiiForums aliyeitwa Jerrytz. Tazama picha hapa chini:
Aidha, JamiiForums imebaini kuwa ukurasa wa X (Zamani Twitter) ya Tanzania Abroad TV umeichukua mada hiyo ya Septemba 19, 2016 na kuifanya kama imetokea Agosti 16, 2023.
Zaidi ya hayo, taarifa hizi hazipatikani katika kurasa zote rasmi za TANESCO.
Hivyo, kutokana na vyanzo hivi, hoja inayodai TANESCO imeshindwa kesi siku za karibuni haina ukweli.