SHAIRI: Mpendwa ujitafute

MakaDik

JF-Expert Member
May 31, 2019
238
133
SHAIRI
MPENDWA UJITAFUTE

1.Ninapolileta somo, cha kwanza nawasabahi
Mi Mzee wa makamo, sikiliza nawasihi
Naufungua mdomo, naamini nimewahi
Mpendwa ujitafute, kwa sasa hupatikani

2.Yule tulomfahamu, tofauti na wa leo
Kawa kama mnywa damu, bora hata ya Farao
Watu wamekosa hamu, maswali kila uchwao
Mpendwa ujitafute kwa sasa hupatikani

3.Baba mama washangaa, mbegu imebadilika
Mtoto unachefua, wazazi wamekuchoka
Kila wanalokwambia, kwako wanaenda chaka
Mpendwa ujitafute kwa sasa hupatikani

4.Ulikuwa mtu mwema, wengi wakakukubali
Ukapatiwa heshima, ulikuwa unajali
Leo wapi umekwama, kila kona una zali
Mpendwa ujitafute kwa sasa hupatikani

5.ulipokuwa hewani, mambo yako yalitiki
Ujipime kwa mizani, wala usipige kiki
Ni wapi ulijilani, ukapoteza riziki
Mpendwa ujitafute kwa sasa hupatikani

6.Mpendwa ujitafute, kwa sasa hupatikani
Kwenye kweli ujikite, tafuta wewe ni nani
Kuuliza usisite, ikiwa haujioni
Mpendwa ujitafute kwa sasa hupatikani

7.unaitwa Dakitari, mchungaji na mwalimu
Una biashara nzuri, mkulima wa kudumu
Lakini una kiburi, watu wanakulaumu
Mpendwa ujitafute kwa sasa hupatikani

8.Fananisha hadhi yako, na heshima upewayo
Vyasadifu vitu vyako, au unapiga myayo
Inakuwa ni kituko, wakusifu kumbe siyo
Mpendwa ujitafute kwa sasa hupatikani

9.Yapo mambo mengi sana, Yafanyayo tusahau
Yanaigusa hazina, na kulipandisha dau
Mengine hayana maana, yafanya watudharau
Mpendwa ujitafute kwa sasa hupatikani

10.mfano ni sitarehe, hututoa kwenye chati
Ninakuwa hohehahe, hata kama nina suti
Mndali au mhehe, jaribu tukaze buti
Mpendwa ujitafute kwa sasa hupatikani

11.Jitafute uko wapi, pafanyapo wakushushe
Wakuone ni makapi, Kataa usichemshe
Kataa kuvaa nepi, kubwa zima wakuoshe
Mpendwa ujitafute kwa sasa hupatikani

12.wengine kuna sababu, zifanyazo wapotee
Ombi Mungu awajibu, Shetani asiwaboe
Mwovu asituadhibu, Mola na atuokoe
Nimalizie kusema wapendwa tujitafute
 
Shairi shule yetu

Shule yetu shule yetu ni nzuri twaipenda
Mwali weetu wa hesabuu kwakweeli twampenda
Hata inyeshe mvuaaa kwenye kipindi atakwendaa
Hata yajae mafurikoo bado kipindii kitakwendaa
 
Shairi shule yetu

Shule yetu shule yetu ni nzuri twaipenda
Mwali weetu wa hesabuu kwakweeli twampenda
Hata inyeshe mvuaaa kwenye kipindi atakwendaa
Hata yajae mafurikoo bado kipindii kitakwendaa
Na kengeeeele ikilia, bado chaaaaaki atashika
Wanafuuuunzi twaumia, bongo zeeeeetu zimechoka
Chipsi duuuuume zatujia, ubaoooooni kumeng'aka
Mwalimu wetu wa hesabu, lolote likukute....

😅😅😅😅
 
Shairi shule yetu

Shule yetu shule yetu ni nzuri twaipenda
Mwali weetu wa hesabuu kwakweeli twampenda
Hata inyeshe mvuaaa kwenye kipindi atakwendaa
Hata yajae mafurikoo bado kipindii kitakwendaa
1714685567245.png

1714685671313.png

1714685740997.png
 
Back
Top Bottom