Serikali: Watumiaji wa Intanet wafikia milioni 36.8

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,864
4,692
1715885389481.png
Serikali imesema kumekuwa na mafanikio makubwa ya sekta ya habari na Mawasiliano, pamoja na upatikanaji wa mawasiliano nchini, hivyo kuongeza idadi ya laini za simu, watumiaji wa intaneti na huduma za kutuma na kupokea fedha katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 .

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya wizara kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 Bungeni jijini Dodoma tarehe 16 Mei, 2024.

“Sekta hii imeendelea kukua ambapo takwimu zinaonesha kuwa laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka milioni 62.3 Mwezi Aprili, 2023 hadi kufikia laini milioni 72.5 Mwezi Aprili, 2024, sawa na ongezeko la asilimia 16.4...watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka milioni 33.1 Mwezi Aprili, 2023 hadi kufikia milioni 36.8 Mwezi Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 11.2”. Waziri Nape

Amebainisha kwamba katika kipindi hicho, pia watumiaji wa huduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtandao wa simu wameongezeka kutoka milioni 44.3 hadi kufikia milioni 53.0 mwezi Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 19.6..

Aidha, Waziri Nape amesema, idadi ya watoa huduma wa Miundombinu ya mawasiliano imefikia 25 ikilinganishwa na watoa huduma 23 waliokuwepo hadi Mwezi Aprili 2023, sawa na ongezeko la asilimia 8.7.
 
Watu tupo million 60 hafu watumiaji million 33.

Labda wanahesabia vifaa sio man to man.
 
Back
Top Bottom