SoC04 Serikali iwekeze nguvu katika sekta ya Kilimo ili kupunguza ukosefu wa ajira

Tanzania Tuitakayo competition threads

jastin22

New Member
May 2, 2024
3
0
Kilimo ni moja ya sehemu ya ukuaji wa nchi na ni moja kati ya sekta iliyo ajili watu wengi katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea kama Marekani.

Serikali ya Tanzania inahitaji kuwekeza nguvu katika sekta hii ili kupunguza ukosefu ya ajira hasa kwa vijana maana idadi ya vijana wenye ukosefu wa ajira ni wengi ukilinganisha na wenye ajira hiyo kama itapewa kipaumbele ni sekta ambayo itakuwa na manufaa kwa miaka ijayo.

Zifuatazo ni faida za kuwekeza katika kilimo.
Kupunguza athari za mfumuko wa bei kwa upande wa mazao,kama ni shuhuda mwaka uliopita mazao ya mahindi yalifika mbaka shilingi elfu ishirini ni kutokana na uhaba wa huduma hiyo kama kungekuwa kuna wingi wa zao hilo mambo yangekuwa kama wakati huu bei zipo chini sana.

Kukidhi soko la ndani na soko la nje, bidhaa nyingi hutokana katika kilimo kama mafuta ya kula hutoka katika zao la alizeti na asilimia kubwa ya mafuta huagizwa nje ya inchi kama zao la alizeti tunge kuwekea mkazo tungekuwa hatuhitaji kuagiza nje ya nchi.

Kuongeza ajira, kwa sasa uhitaji wa ajira ni mkumbwa na hakuna muafaka wa wapi vijana wapi wafanye kazi huwezi kuona changamoto tena.

Kutatua changamoto ya ukosefu wa malighafi kwa viwanda, mwaka huu tumeshuhudia baadhi ya viwanda kusimama uzalishaji kama sukari kwa kukosa malighafi za kuzalisha sukari miwa na kusababisha kitengo cha sukari kuagiza sukari nje ya nchi ili kupunguza uhaba wa sukari nchi kama kungekuwa kuna wingi wa malighafi haungetokea mfumuko wa bei kwa upande wa sukari.

Pia kuna hasara kwenda katika kilimo biashara kwani kunaweza kusababisha uharibifu wa mazingira kama hakutakuwa na sera maalumu
 
Kilimo, kilichoitwa uti wa mgongo wa Taifa kina uwezekano wa kuliinua taifa.

Tunahitaji kufanya kitu kidooogo tu kama ulivyogusia kwenye mahindi na alizeti nacho ni SOKO LA UHAKIKA.

Kijana, muwekezaji, mwananchi na yeyote yule atavutiwa kiotomati pale atakapoona kuna 'dili'. Na ili ionekane hivyo ni pale atakapoamini ku a soko la uhakika la bidhaa zake.

Tulime na tuuze ndani na nje bila ukiritimba, kilimo kitaajiri watu wengi mnoooo.
 
Tatizo ni masoko mkuu sio, serikali haitaki tuuze nje.
 
Tatizo ni masoko mkuu sio, serikali haitaki tuuze nje.
Yaaani

Wajiulize mbona sie bidhaa za nje tunauziwa sana.

Hawaoni kwamba hizo bidhaa ndio kama mazao ya 'kilimo' cha viwanda vya hizo nchi!

Tutaendeleaje sasa kama hakuna tunachozalisha na kuuza nje? Na tunachoweza sanansana ndio hicho bidhaa za kilimo.

Tujitafakari kama nchi
 
Back
Top Bottom