Jay One
JF-Expert Member
- Nov 12, 2010
- 16,921
- 16,885
Rais wetu, Mama Samia, kwanza tukupe hongera sana kwa kazi kubwa na inayoonekana kwa Taifa letu, hakika kazi unaimudu na unaiweza kisawa sawa.
Rais tunakuomba pamoja na juhudi zako kubwa za kujenga nchi na kuwa hudumia wananchi wote ikiwemo wafanya kazi wa umma, nikupe siri, tupia jicho kali pale Utumishi Wizarani.
Yaani watumishi wa umma wako wanaumia sababu ya baadhi ya watendaji wabovu, wanaofanya kazi kwa mazoea, hawana muda kabisa kuhudumia watumishi wa umma, yaani wao kutwa nzima ni kufukuzana na vikao ili wapate posho za vikao.
Labda nitoe mfano hai, pale wizarani utakuta mtumishi anatakiwa kupewa barua labda ya promotion, Mkurugenzi husika atazunguka barua haandiki na itachukua hadi mwaka au miaka ili tu aandike barua kwa mtumishi ili iende kwa mwajiri ampe promotion mtumishi.
Yaani kazi hiyo ni kilio, watumishi wako wanalia ni shida, mkurugenzi anakuwa Mungu mtu, naomba ulizia hili utaambiwa nayokwambia Rais, tena hawajali chochote, tuma watu wako hapo Mtumba utaona madudu haya.
Mfano mwingine, utatuma barua ya kawaida Utumishi labda ya kufuatilia kubadili kada, labda umepata sifa fulani ya elimu, yaani ni miaka, sielewi Utumishi wako hivyo sababu gani?
Naomba Rais fuatilia kwa ukali, ulizia promotion za watu na watumishi waliopeleka malalamiko yao Utumishi, hata ufuatilie vipi, utakwama na hupati majibu yaani itachukua miaka.
Utumishi ni shida sana, Rais tunakuomba mno pita wizarani hapo, utakuta mengi ya watumishi wa umma hayafanyiwi kazi kwa miaka na viongozi uliowapa dhamana wapo na hii huleta chuki ya watumishi wa umma kwa serikali kumbe ni watu uliowapa dhamana wanakuangusha vibaya sana.