Nyerere Years

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,142
30,493
THE NYERERE YEARS

Nakifahamu kitabu hiki kuhusu marafiki wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

In Shaa Allah nitajaribu kuandika niyajuayo kutokana na majina ya hawa ambao ni rafiki zake na ndiyo waandishi wa kitabu hiki.

Bahati mbaya sana kuwa hawa waandishi Wazungu ukiwatoa wachache wanatambulikana katika kitabu hiki kama marafiki wa Nyerere.

Nimesema bahati mbaya kwa sababu hawa wakishatambulika kama ndiyo marafiki wa Nyerere hii itaondoa nafasi ya kuwajua marafiki wa kweli wa Mwalimu.

Urafiki si kitu chepesi.
Urafiki uko jirani sana na udugu kama vile usingizi na mauti.

Upo msemo, "Rafiki ndugu."

Katika hawa marafiki ndani ya kitabu hiki hakika sijamuona rafiki wa Nyerere kwa dhati ya nafsi mfano wa Kenneth Kaunda, Andrew Tibandebage, Hamza Mwapachu, Abdul Sykes, Amir Jamal na Dossa Aziz kwa kutaja majina machache.

Niyaonayo hapo ni majina ya watu waliojuana na Nyerere kwa sababu ya kukutananae akiwa mwanafunzi Uskochi na baadae Nyerere akajakuwa vile alivyokuwa.

Hii ndiyo ikawa sababu ya mtu kujinasibisha na yeye.

Vinginevyo tungesikia majina ya marafiki wengine wa Nyerere yakitajwa mfano wa Paul Bomani au Sheikh Issa Nasir Ismail wa Bagamoyo.

Kaunda ana haki ya kuwamo katika orodha ya marafiki wa Nyerere.

Amir Jamal ana haki kubwa sana ya kuwemo katika orodha ya marafiki wa Nyerere.

Amir Jamal amemjua Nyerere, mwalimu wa shule anaishi Pugu Mission na wakawa marafiki maisha yao yote.

John Iliffe yuko katika orodha ya marafiki wa Nyerere.

John Iliffe mwanahistoria bingwa wa historia ya Tanganyika na kama ilivyoandikwa kuwa ni rafiki wa Nyerere.

John Iliffe kwangu kimebaki kitendawili kizungumkuti vipi hakuweza kuandika historia ya Julius Nyerere rafiki yake?

Cranford Pratt alikuwa rafiki wa Nyerere lakini kimaslahi zaidi kwani yeye ndiye Mwalimu alimleta kutoka Canada kuanzisha Chuo Cha Kivukoni.

Yapo mengi ya kusema lakini tutosheke na haya.

Natamani kama na sisi kama walivyofanya Britain - Tanzania Society tungeandika kitabu kama hiki chao tukawataja marafiki wa kweli wa Julius Nyerere.

Lakini kwa kuhitimisha tujiulize wanahistoria wa Tanzania wanawajua marafiki wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere?

1715110693418.png

1715110944780.png

Attachments

  • 1715110301954.png
    1715110301954.png
    31.2 KB · Views: 4
  • Thanks
Reactions: vvm
THE NYERERE YEARS

Nakifahamu kitabu hiki kuhusu marafiki wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

In Shaa Allah nitajaribu kuandika niyajuayo kutokana na majina ya hawa ambao ni rafiki zake na ndiyo waandishi wa kitabu hiki.

Bahati mbaya sana kuwa hawa waandishi Wazungu ukiwatoa wachache wanatambulikana katika kitabu hiki kama marafiki wa Nyerere.

Nimesema bahati mbaya kwa sababu hawa wakishatambulika kama ndiyo marafiki wa Nyerere hii itaondoa nafasi ya kuwajua marafiki wa kweli wa Mwalimu.

Urafiki si kitu chepesi.
Urafiki uko jirani sana na udugu kama vile usingizi na mauti.

Upo msemo, "Rafiki ndugu."

Katika hawa marafiki ndani ya kitabu hiki hakika sijamuona rafiki wa Nyerere kwa dhati ya nafsi mfano wa Kenneth Kaunda, Andrew Tindegebage, Hamza Mwapachu, Abdul Sykes, Amir Jamal na Dossa Aziz kwa kutaja majina machache.

Niyaonayo hapo ni majina ya watu waliojuana na Nyerere kwa sababu ya kukutananae akiwa mwanafunzi Uskochi na baadae Nyerere akajakuwa vile alivyokuwa.

Hii ndiyo ikawa sababu ya mtu kujinasibisha na yeye.

Vinginevyo tungesikia majina ya marafiki wengine wa Nyerere yakitajwa mfano wa Paul Bomani au Sheikh Issa Nasir Ismail wa Bagamoyo.

Kaunda ana haki ya kuwamo katika orodha ya marafiki wa Nyerere.

Amir Jamal ana haki kubwa sana ya kuwemo katika orodha ya marafiki wa Nyerere.

Amir Jamal amemjua Nyerere, mwalimu wa shule anaishi Pugu Mission na wakawa marafiki maisha yao yote.

John Iliffe yuko katika orodha ya marafiki wa Nyerere.

John Iliffe mwanahistoria bingwa wa historia ya Tanganyika na kama ilivyoandikwa kuwa ni rafiki wa Nyerere.

John Iliffe kwangu kimebaki kitendawili kizungumkuti vipi hakuweza kuandika historia ya Julius Nyerere rafiki yake?

Cranford Pratt alikuwa rafiki wa Nyerere lakini kimaslahi zaidi kwani yeye ndiye Mwalimu alimleta kutoka Canada kuanzisha Chuo Cha Kivukoni.

Yapo mengi ya kusema lakini tutosheke na haya.

Natamani kama na sisi kama walivyofanya Britain - Tanzania Society tungeandika kitabu kama hiki chao tukawataja marafiki wa kweli wa Julius Nyerere.

Lakini kwa kuhitimisha tujiulize wanahistoria wa Tanzania wanawajua marafiki wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere?

Jina sahii ni Andrew Tibandebage.
 
Back
Top Bottom