GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 5,183
- 7,010
Sitafuti kuwa mkamilifu kwenye Kiingereza, ila nimekataa kuwa chini ya "level" 5.
Kuhitimu Chuo Kikuu si tiketi ya kuongea lugha kwa ufasaha. Hata wazawa wa "English" kuna ambao bado wanajifunza, pamoja na kuwa ni watu wazima na wasomi.
Kwenye mtandao wa kijamii wa Kimataifa wa Quora, kuna swali limeulizwa hivi: HOW LONG DID IT TAKE YOU TO LEARN ENGLISH IN ORDER TO SPEAK IT FLUENTLY?
Kuna majibu tofauti kwa watu tofauti. Kuna waliosema miezi sita, wengine miaka miwili, wengine mwaka mmoja, wengine miaka minne, n.k.
Lakini jibu la huyu mtu limenigusa vilivyo!
Anaandika, "I'm 54 years old, native speaker, and I still have not learned to speak perfectly ..." - Daniel.
Inamaanisha Daniel angali akijifunza.
Ikiwa Daniel angali akijifinza, mimi ni nani nione aibu kujinoa zaidi?
Ona,
1. Kanizidi umri
2. Kiingereza ni lugha yake ya kwanza
3. Inawezekana, kanizidi pia na Elimu. Labda ana "Masters Degree", wakati mimi ningali na shahada moja.
"Kibongo bongo", kama wengine wasemavyo, ningeweza kuhesabiwa kuwa na mimi ninajua Kiingereza. Lakini kwa jinsi nijuavyo, bado sana. Lakini wiki sita (siyo miezi sita), naam, wiki sita kuanzia sasa, nitakuwa nimepiga hatua kubwa sana.
Nimeshapakua video kadhaa za kutumia kwa mazoezi.
Kama kuna mwenye wazo lo lote la kuboresha au la kuongezea, nitapokea kwa mikono miwili.
Nawakaribisha na wale wote wasioona aibu kujifunza tujumuike pamoja kujinoa katika hii lugha izungumzwayo na watu wengi zaidi duniani kuliko lugha nyingine yo yote ile.
Nikiishafikia viwango vya Kimataifa, nitaangalia kama nijinoe kidogo kwenye Kiswahili, au nijifunze lugha mpya kabisa, kati ya Kifaransa, Kihispaniola, Kiitaliano au Kijerumani.
Hata hivyo, kura inaweza kuiangukia Kifaransa.
It's never too late to start...
Nimeamua kuanza sasa, na sitasimama hadi nifike.