Ndoa hizi zitatuua Jamani!

shuka chini

Senior Member
Feb 27, 2024
196
517
Ndoa hizi zitatuua.Jamani ipo hivi .Mimi ni mme mwenye mke mmoja na mtoto mmoja.Mke huyu tumetoka nae mbali tulianza nae mwaka 2008. Changamoto aliyo nayo ni kelele na wivu uliopitiliza yani sina amani ndani akianza kuongea hamalizi .

Kiufupi tabia yangu niyakawaida sichepuki sana. Sasa juzi hapa kafanya kituko nimetoka mapema asubuhi kumbe huku nyuma kafanya vurugu kwa majirani yupo mama mmoja ni msimbe sasa mke wangu anahofia kuwa natembea nae .

Kiukweli huyu mama hata sijawahi kumtongoza ila mke wangu anamuhofia bure.Hili jambo linanipakero sana.

Mungu kajaria tumejenga sasa kila siku ananitisha kwamba tutauza nyumba tugawane.
Vurugu ikizidi sana hii ndoa itakuja kufa bora kuanza upya kuliko kuishi bila amani.

Hivi wadau mnaishije na aina hii ya wanawake. Ninachangamoto sana yani hapa nimekaa juu ya jiwe kijiweni nawaza namna ya kurudi nyumbani maana nikifika tu ni kelele.
Nawasilisha wakuu.
 
Ndoa hizi zitatuua.Jamani ipo hivi .Mimi ni mme mwenye mke mmoja na mtoto mmoja.Mke huyu tumetoka nae mbali tulianza nae enzi tunasoma mwaka 2008 kipindi hicho nipo kidato cha tatu yeye kidato cha kwanza.
Changamoto aliyo nayo ni kelele na wivu uliopitiliza yani sina amani ndani akianza kuongea hamalizi .

Nimeshapiga sana mpaka basi kiufupi tabia yangu niyakawaida sichepuki sana. Sasa juzi hapa kafanya kituko nimetoka mapema asubuhi kumbe huku nyuma kafanya vurugu kwa majirani yupo mama mmoja ni msimbe sasa mke wangu anahofia kuwa natembea nae .

Kiukweli huyu mama hata sijawahi kumtongoza ila mke wangu anamuhofia bure.Hili jambo linanipakero sana.

Mungu kajaria tumejenga sasa kila siku ananitisha kwamba tutauza nyumba tugawane.
Vurugu ikizidi sana hii ndoa itakuja kufa bora kuanza upya kuliko kuishi bila amani.

Hivi wadau mnaishije na aina hii ya wanawake. Ninachangamoto sana yani hapa nimekaa juu ya jiwe kijiweni nawaza namna ya kurudi nyumbani maana nikifika tu ni kelele.
Nawasilisha wakuu.
Ndoa ni ya Me wenye uanaume tu na Ke wema wala si Wavulana, zingatia "uanaume".

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Pole sana. Ndoa imekuwa jehanamu kwa wengi, ila na wewe tayari umekubaliana na hali, mkeo kashakusoma madhaifu yako na kubadilisha hio kitu inahitaji wewe mwenyewe ubadilike ndo na yeye afuate. Sijui nini chanzo ila kama unataka amani inabidi uianzishe wewe, only you can change it, jifanye mjinga kW muda, usimkaripie wala kumjibu huo ndo uanamme sio kukimbia na kulialia. Kutafta mwanamke mwingine utazingua, kama mmedumu toka 2008 means mnajuana vizuri, work it through bro.
 
Back
Top Bottom