johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 85,645
- 145,384
Waziri Nape anasema wanashauriana Serikalini ama kupunguza Kodi Kwenye Simu Janja au kuweka Kodi Kwenye Vitochi (viswaswadu) Ili Watu wote waweze kumiliki Simu Janja.
Huko tunakoelekea teknolojia ya Vitochi itapotea hivyo ni Bora kujihami mapema, amesisitiza Waziri wa Sayansi na Teknolojia mh Nape.
===
“Nadhani tunapoenda tunashawishiana serikalini kuangalia namna aidha ya kutoa kodi kwenye simu janja ili zishuke bei zaidi na ikiwezekana tuweke kodi kwenye vitochi (viswaswadu/ simu ndogo) kwa sababu hivi vitochi huko tunakoenda teknolojia yake itapotea, sasa tunaweza tukajikuta na vitochi vingi vikawa uchafu tu mtaani, kwa sababu Ulaya huwezi kutumia kitochi, haipo tena, sasa wameanza kuvitupa kuja bara la Afrika Kwa hiyo na sisi huku lazima tulinde bara letu, watu waendelee kupata huduma ila taratibu tuvisafishe zipatikane simu za kisasa (simu janja/ simu kubwa), vifaa vya kisasa na kompyuta za kisasa”
Nape Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema hayo leo, Jumatano ya tarehe 15 Mei 2024 wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha Good Morning cha Wasafi FM
Source: Jambo TV