My true story of love: My girl left at the time i had never thought

Wow umefikia wapi sasa? Naye amejua hana ukimwi au? So kusema kuachwa solemba ndio utasema baadae?

Haya wai kabla hatujasahau una story hii.
 
nilikuwa naogopa kuandika story hii kwa kuhofia urefu wake kiasi kwamba watu wasingeisoma, wachache waliosoma na kuniomba niiendeleze inashiria wameisoma yote, wewe umenipa nguvu zaidi kiasi leo nimeindeleza tena japo sikuwa na muda nimejitahidi.

Nashukuru kuwa mmoja wa waliokupa moyo wa kuiendeleza story hii. Tupo wote mwanzo mwisho

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
I can imagine ulivyokuwa unajisikia, ulivyokuwa unasimuliwa jinsi mpenzi wako alivyokupenda na kutunza uaminifu wake kwako. Najiuliza kwa kweli nini kilitokea hadi mkatengana.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
1ST STORY

YALIKUWA NI MAPENZI YA SHULENI:

Nilimaliza o level na kumuacha msichana wangu akiendelea na masomo na mimi nikaenda kuendelea na masomo yangu baada ya kumaliza fm 4.

Umbali uliotutenganisha ulikuwa zaidi ya kilomita 1600 kama sijakosea. maana ni safari inayochukua masaa 14 mpaka 15 ama 16 ili kutuweka tena pamoja.

Likizo ilipofika nakumbuka mwezi wa nane wakati wa likizo nilikuwa na hamu sana ya kurejea nyumbani maana nilikuwa nime-m-miss sana my lovely girlfriend pamoja na kwamba tulikuwa tunawasiliana kwa simu za kuibiaibia maana shuleni kwake simu ilikuwa marufuku.

Ilikuwa safari ndefu ya siku karibia mbili kwa usafiri wa treni ndipo mida ya saa kumi alfajiri nikawa nimefika nyumbani.

FURAHA NA HAMU YANGU ILIISHA GHAFLA BAADA YA USIKU ULEULE NILIPOFIKA NA KUAMBIWA NA MARAFIKI ZANGU KUWA MPENZI WANGU TAYARI ALISHAMILIKIWA NA MWINGINE.

haiiiiiiiiiiii, haikuwa habari njema sana kwangu na niliumia zaidi na kusoneneka sana nisiamini kirahisi maneno yale.

mapema nikaamua kwenda kuongea na mpenzi wangu.

kwa wakati ule alikuwa anaishi mtaani amepanga chumba sikuona tena haja ya kusubiri mpaka jua lichomoze mana nilikuwa nimeumia tayari na nikataka kujua ukweli wakati uleule.

HATA HIVYO HAUKUWA UAMUZI MWEPESI KWANGU KWENDA KUMGONGEA USIKU HUKU AKIWA HANA TAARIFA KAMA NIMEKUJA NA NIKIWA SIJUI KAMA NITAMKUTA PEKE YAKE AMA NA JAMAA NILIYEAMBIWA AMESHAMMILIKI.

nilijiuliza mara mbilimbili na mwisho nikaona bora nimfate muda uleule.

Kwa kuwa haikuwa mbali toka nilipofikia na alipokuwa amepanga , safari yangu ilinichukua kama dakika nne ama tano hivi nikawa nimefika.

Kwa kuwa nyumba ile haikuwa na uzio basi nilizunguka nyuma ya dirisha lake na kugonga dirishani, kwanza mtoto ndo amelala fofofoh, mmmh nikahisi inawezekana vyumba vingine wakaamka alafu wanishangae kwa nini ninagonga dirisha la mtu mida ile, ila nikajikaza moyo. mara nikasikia mtu anajinyoooooosha taraaatibu kitandani kuashiria anaamka, ikawa kweli akaamka.

Nikamwambia afungue malango, ni mimi xxxx, jina langu halikusaidia kitu maana hakuamini kama ni mimi, akahoji mbona xxxx hayupo huku na sauti yake siyo hiyo?

Niliposikia anasema sauti yangu si yenyewe nikaona sasa hapa mziki umekuwa mnene, kimsingi sauti yangu ilikuwa imebadilika sana kutokana na kiswahili nilichokuwa naongea kutokana na utofauti wa lafudhi ya kiswahili kwa kila mikoa baada ya sipo huko huko yapata miezi sita.

Nikalazimika kutaja majina yangu yote manne labda anaweza kuamini kuwa ni mimi,maana sikuwa na njia nyingine ya kumfanya aamini kuwa ni mimi, nikamwambia ni mimi xxxx yyyy uuuu zzzz, bado hakuafiki maana majina yale yalikuwa yanajulikana kwa kila mtu na yeyote angeweza kuyatamka ili kumhadaa.

Nikiwa nimekataliwa kufunguliwa mlango na nikiwa nawaza kuondoka nikamalizie usingizi wangu geto, ghafla nikakumbuka jina moja ambalo kimsingi si jina langu ila lipo kwenye ukoo wetu ambalo niliwahi kumwelezea siku moja akawa amelifurahia sana kutokana na maana yake na akawa ananitania kwa kuniita jina hilo hata nilipomwambia si langu hakuacha kuniita maana ilikuwa sehemu ya utani wake kwangu,

ILI KUJIOKOA IKABIDI JINA LILE NILITUMIE MAANA HAKUNA ALIYEKUWA ANALIJUA ZAIDI YAKE, nikamwambia ndiyo mimi MMMM, hapo tayari kazi ikawa imekwisha baada ya yeye kuwa ameamini kuwa ni kweli mimi ndiye XXXX, hakusita tena kufungua mlango maana hata yeye hakuamini kama muda ule angeweza kumuona kipenzi wake baada ya kumkosa muda mrefu. nilijikaza nikaingia ndani.

Mpenzi wangu aliponiona baada ya kufungua na kunikumbantia, alikuwa mwenye furaha isiyoelezeka, huku mimi nikilazimisha furaha maana tayari moyoni nina maumivu na hicho ndiyo kilinipeleka ili nikajue ukweli,

Nilijikaza nisismuulize lakini uzalendo ulinishinda nikaamua kumuuliza juu ya huyo jamaa, jibu lake lilikuwa jepesi kuwa si kweli, nilimgombeza zaidi maana nilikuwa nimesimuliwa japo kwa ufupi, bado alisema si kweli,

Akili ikanicheza, nikaamini ghafla kuwa, kwa vyovyote vile kusingekosekana ushahidi wa barua ama kadi za love mule ndani toka kwa jamaa yake huyo.

Nikamuuliza, je humu hakuna ushahidi wowote unaoonesha huyo jamaa ni mpenzi wako?
jibu lake halikubadilika, akasema haupo.

Ikabidi nianze zoezi la kusearch mwenyewe, nikamwambia afungue begi lake huku sijamwambia ninatafuta nini, akafungua beg lake na kunikabidhi niangalie mwenyewe, nikamwambia apangue nguo moja baada ya nyingine ili nione kama hakuna kitu.
alifanya hivyo huku machozi yakimtoka, kila nilipomwangalia , huruma ikawa inanijia na kuhisi labda si kweli kama anavyosema.

Nguo zilikuwa nyingi, lakini toka nguo ya juu mpaka ya mwisho sikuona kitu,
janja yangu ikawa imefeli maana sikuona chochote kama nilivyofikiria kuwa ningeweza kumkamata kirahisi maana nilimshitukiza.

Wakati nikitafakari zoezi langu kushindwa, ghafla nikakumbuka kuwa hata kadi na barua zangu nilizowahi kumtumia sikuziona pia, kwa sababu nilimshitukiza, nikaamini kabisa kuwa kama ni kadi za mapenzi ama barua lazima atakuwa anaziweka sehemu moja.

Nikamuuliza, kadi zangu zote na barua nilizokuwa nakutumia ziko wapi? taratibu akafungua zip ya beg upande mwingine, nikajua humo ndo atakuwa kaweka kila kitu,nikwamambia atoe kila kilichomo mule ndani na anikabidhi, alifanya hivyo,

Nikaanza kukagua mwenyewe, nikakutana na kadi moja iliyotoka kwa mtu huyohuyo niliyeambiwa japo ilikuwa kadi ya urafiki wa kawaida lakini tayari nikawa nimepata ushahidi wa niliyoambiwa, nilimhoji ile kadi ni ya nini, akaniambia alimtumia kumuomba msamaha alipomtongoza wakakosana ndipo akamuomba msamaha, kimsingi kadi haikuwa na maneno yoyote ya kuomba msamaha kama ilivyochapishwa, nikamuuliza mbona hakuna sehemu unaombwa msamaha,

Aliichukua ile card na kuifungua nyuma kulikowa na maandishi ya wino wa bluu ambayo pamoja na mambo mengine nikaona ni kweli aliombwa msamaha, nikamuuliza , kwa nini kadi zangu hajazazichana wala kuzichoma moto? hili lilikuwa swali la mtego, akajibu hajachana wala kuchoma kadi zangu kwa kuwa ni za muhimu,

SIKUWA NA NAMNA ZAIDI YA KUAMINI KUWA HAIKUWA KWELI, LAKINI NILIENDELEA KUWA NA WASIWASI, NIKAMSAMEHE MUDA ULE NA MAMBO YAKAENDELEA.

NILIRUDI SHULE TENA.

HATA HIVYO LIKIZO YA MWEZI WA PILI MWAKA ULIOFUTA NILIRUDI TENA.
wakati huu akawa amehamishiwa boarding.

ILIKUWA JUMAMOSI YA PEKEE KESHO YAKE MARA TU NILIPOFIKA.

JUMAMOSI KULIKWA NA MICHEZO SHULENI.

Nilienda pia kushuhudia jioni ya jumamosi maana ilikuwa ni siku maalumu ya kuhitimisha finali ya sports and games ambazo huchukua wiki mbili za mashindano, muda mwingi nilikuwa nae pale shuleni tukiangalia wote michezo maana na mimi nilikuwa ni kama sehemu ya shule ile baada ya kukaa pale miaka yangu yote ya o level.

Wakati ule mkuu wa shule alikuwa amekuja mwingine na alikuwa amekuja na sheria kali zaidi kudhibiti aina yoyote ya mahusiano kwa wanafunzi, kimsingi alipiga marufuku hata mvulana kuonekana unakaa kwa kalibu na msichana ama kushikana mikono na adhabu ilikuwa moja tu suspension ama akiamua anafukuza kabisa shule.

Lakini kwangu sikuonekana kuogopa maana sikuwa tena mwanafunzi pale, kwa hiyo niliendelea kukaa na kuongea na my girl.

Tukaagana baada ya michezo kuisha nikarudi mtaani naye akaenda bwenini, jumapili ilipita salama.

Jumatatu nilikuwa na apointment na daddy maana alitaka nikamweleze mahitaji yangu ya shule maana nilikuwa napendelea zaidi kukaa geto kuliko kwa mzee, nikaenda mapema kwa mzee.

Ni ngumu kuelezea kilichotokea lakini nilipata hisia ghafla zisizo za kawaida, badala ya kukaa niongee na mzee, nikamwambia ningekuja baadae nikaondoka kuelekea geto.

Kabla sijafika geto, nikakutana na SHANGAZI YAKE DEMU WANGU, sikujua anatokea wapi maana hakuwa anakaa pale.

Sikujali sana, nikaendelea kwenda, ghafla nikakutana na mpenzi wangu akiwa ana mwanafunzi mwenzake amebeba jembe lakini ni nje kabisa ya eneo la shule, kifupi ni mtaani huku akiwa kavaa uniform za boarding, nilipoona jembe tu nikajua amepewa adhabu na mathalani kwa sababu alionekana akiongea na mimi siku ya jumamosi,

Nikamuuliza, umepwa adhabu? akajibu hapana nikamuuliza umepwa suspension? akasema hapana mikamuuliza umefukuzwa shule? akasema hapana.

ALL MY GUESS WERE OVER.

Nikamuuliza sasa nini tatizo? akasema HAPA NILIPO NDIO NAKUAGA NINAENDA KWETU DAR, it was shocking to me. nikamuuliza kwa nini hakuniambia jumamosi wakati nilikuwa naye, akasema hata yeyey hakujua maana amefatwa asubuhi na shangazi yake.

Nikahoji kwa nini anahamishwa shule, akasema nyumbani kwao wamesema shule siyo nzuri, nikamuuliza anaenda shule gani, akasema haikumbuki jina japo ameambiwa.

Daaaaaah sikuwa na jinsi na nilihisi kuumia, ukizingia mimi sikuwa na simu wala yeye hakuwa na simu, lakini kibaya zaidi kwao sikuwa napajua pamoja na kuniambia anapokaa lakini isingekuwa rahisi kumpata tena.

Nilimuaga kwa unyonge, nikarejea geto, nilipofika tu nikamkumta jamaa yangu, nikamwambia demu wangu ndo anarudi kwao dar, jamaa hakushituka sana.

Akaniuliza swali, UNAJUA KWA NINI AMEHAMISHWA HAPA? NIKASEMA SIJUI ILA KANIAMBIA KWAO WAMESMEA SHULE SIYO NZURI

Akanimbia YULE MSICHANA AMEATHIRIKA NA ANATUMIA VIDONGE VYA ARV NA NDIO SABABU YA KUMUONDOA SHULENI, wakati kichwa kikiwa kimepigwa butwaa, jamaa akaendelea kunipa ushahidi, akaniambia, yeye anafahamiana na shagazi yake kupitia mama yake maana waliwahi kufanya kazi pamoja.

akaniambia asubuhi ile ile muda almost mfupi tu amekutana na shangazi yake demu wangu akitokea shuleni, alipomsalimia akamwambia "natokea shuleni kumhamisha mdogo wako huwa ni mgonjwa tunamhamishia dar akakae karibu na huduma ya matibabu"

Jamaa kaendelea kunipa ushahidi zaidi, akasema yule jamaa ambaye niliambiwa aliwahi kummiliki hapo kabla wakati sipo ndiye aliyegundua kuwa yule msichana ana HIV baada ya kuona anatumia vidonge vya ARV na akaamua kumwacha ila stori ile aliwasimulia wenzake.

NILIKUWA KAMA NIMEPIGWA GANZI, MWILI ULIKOSA NGUVU GHAFLA NIKALALA KITANDANI HUKU SIJIELEWI TOKA ASUBUHI MPAKA JIONI HATA SIKULA.

Yakawa ndio maisha yangu ya mawazo na mateso huku nikikosa kabisa hamu ya kula, niliwaza mengi sana, bahati nzuri ijumaa ya wiki ileile msichana wangu alikuaj kuniaga rasimu maana jumapili ndiyo ilikuwa safari, sikutaka kumuuliza habari za ARV NA HIV, nilimuuliza kama anaumwa ugonjwa wowote akasema haumwi basi nikakaa tu jumapili ilifika akaondoka.

Mimi nikaonda sana huku nikujua sikuwa na namna na ikafika muda nikakubali kuwa basi nisingeweza kuibadili historia japo niliumia sana. na muda mwingi nilijihisi dalili za hiv zinaninyemelea.

Ilinichukua miezi miwili ya mawazo na kukonda. mwisho nilipooona na kuamini kuwa ni kweli kwa dalili za kukonda kupita kiasi na kuugua madonda mdomoni yaliyodumutakribani mwaka mmoja kuwa nilikuwa nimeathrika, nikaamua ni bora nikapime nijue niishije.

Nilienda angaza, kimbembe kikaanza, zilipoanza kutajwa dalili za hiv karibu karibu zote nilikuwa nazo.

1.kupungua uzito, nilikuwa nimekonda sana kuliko wakati mwingine wowte wa maisha yangu.

2.madonda mdomoni, tayari nilikuwa nayo tena yameshagoma kupona kama mwaka mzima.

3.miguu na mikono kupata ganzi, hapo ilikuwa kawaida tu kupata ganzi, zikaja njia za kuambukiza.

1.kiss, nilifanya sana.
2.sex, nilifanya pia

nilikuwa mpole na nikawa jasri maana tayari ninajua kwa dalili zile nilikuwa affected tayari.

itaendelea
.xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

MAMBO YA ANGAZA.

baada ya maelezo ya mpimaji na maswali yake kuniridhisha kuwa hakuna namna zaidi ya mimi kuwa nimeathirika.

akatoa nafasi kwa sisi kuuliza maswali.
kimsingi katika chumba kilichokuwa kimejaa waliokuja kupimwa HIV mimi nilionekana kama mtoto ama mdogo peke yangu maana wengi walikuwa wakubwa.

katika chumba kile hofu ilikuwa kubwa na ukimya ulikuwa umetawala kiasi cha hata mtu akidondosha sindano, sauti itasikika.

nikawa wa kwanza kunyosha mkono, kuashiria nilikuwa nina swali kwa mtoa ushauri nasaha, wakati huo wenzangu wakiniangalia kuona ninataka kuuliza nini.

LAKINI KABLA SIJANYOSHA MKONO KUTAKA KUULIZA SWALI NILIJIULIZA NA KUFIKIRIA YAFUATAYO KICHWANI NDANI YA SEKUNDE CHACHE SANA.

kwa kuwa mpenzi wangu nilimkuta bikra na kwa kuwa katika kipindi chote cha uhusiano wetu wakati sijamaliza o level alikuwa mwaminifu sana na niliamini kuwa kwa muda wote ule hakuwahi kunisaliti, na kwa kuwa wazazi wake wote wawili walifariki wakati yeye akiwa mdogo sana na ikawa inasemekana huenda chanzo cha kifo chao kilikuwa UKIMWI, na kwa kuwa dalili muhimu ya kuugua ukimwi ya vidonda mdomoni nilikuwa nayo hata kabla sijaenda form5 akili ilikuwa imeshanituma kuwa mpenzi wangu alizaliwa na wazazi waliokuwa wameathirika na hivyo alizaliwa akiwa na ukimwi,kwa sababu dalili ya ugonjwa wa vidonda mdomoni ilikuja mapema zaidi hata kabla sijaondoka na jamaa aliyesemekana kummiliki akiwa hata hajamtongoza, na kwa kuwa shangazi yake na mpenzi wangu alikuwa anajua kuwa mtoto wa marehemu kaka yake alikuwa mgonjwa(kama nilivyosimuliwa na jamaa yangu kuwa shangazi kasema MDOGO WENU HUWA NI MGONJWA HIVYO TUNAMSOGEZA KWENYE HUDUMA), na kwa kuwa mpenzi wangu nilipomuuliza siku ile aliporudi kuniaga rasimi kabla ya kuondoka KAMA ANAUGUA UGONJWA WOWOTE AKANIKATALIA, NIKAWA NIMEPATA HITIMISHO KICHWANI KUWA MPENZI WANGU ALIZALIWA NA UKIMWI NA YEYE KAMA MTOTO ASINGEAMBIWA NA ASINGEWEZA KUJUA.

LIFUATALO NDIO SWALI NILILOMUULIZA MTOA USHAURI KUTOKANA NA NILICHOKUWA NIMEKIWAZA.

MIMI: JE MTOTO AKIZALIWA NA UKIMWI ANAWEZA KUISHI MPAKA UMRI GANI?

ANGAZA(mshauri): Inategemea, anaweza hata kufika miaka mitano,wakati mwingine anaweza hata kufika darasa la saba, wengine wanasoma mpaka wanamaliza o olevel.

MAJIBU YA MSHAURI YALIZIDI KUNITESA AKILI, kwa sababu akili yangu yote ilikuwa ina hisia kuwa huenda mpenzi wangu alizaliwa na ukimwi basi jibu la mshauri lilizidisha hofu yangu na kuzidi kuongeza ushahidi kuwa atakuwa alizaliwa na ukimwi maana nilitegemea mshauri angeniambia labda hawafikishi miaka mitano kidogo ningejipa matumaini.

KWA HARAKA NIKAWA NAFIKIRIA KUISHIA FORM SIX NISIENDELEE NA CHUO HATA KAMA NIKIFAULU MTIHANI ILI NIKAFUNDISHE SHULE ZA KATA WALAU NIWASAIDIE WADOGO ZANGU KWA KIPINDI KIFUPI AMBACHO KILIKUWA KIMEBAKI KWA UHAI WANGU, NILIHISI NIMEWAKOSEA SANA WAZAZI KWA KUWA WALINITEGEMEA SANA NA MIMI NDIYE NILIKUWA WA KWANZA KUSOMA HUKU WADOGO ZANGU WAKITUMAINIA MSAADA WANGU MAANA WALIJUA NIKAMILIZA MASOMO NITAKUWA MSAADA KWAO.

ILIKUWA KAMA MSHAURI AMESHAJUA NINAWAZA NINI KICHWANI.

akaendelea kutoa ushauri kutokana na swali langu, akasema" UKIMWI hau-ui maana mtu ukishagundulika mapema unaweza kuishi miaka mingine mingi,hata ishirini mpaka therathini, wewe kama unasoma endelea kusoma hata mpaka chuo kikuu, kama una mipango mingine endelea kufanya wala usiwe na wasiwasi"

duuuuuuuuuuh , nilihisi kama mshauri anajua kila kitu kuhusu mimi japo hiyo angaza yenyewe ilikuwa kilomita zaidi ya 80 toka kwetu.

BAADA YA MAJIBU NA MAELEZO YAKE HAKUKUWA NA SWALI TENA.

IKAWA MUDA WA KWENDA KUCHUKUA KIPIMO.
ilipofika zamu yangu , nikaitwa , nikaingia chumbani kutolewa damu.

ndani nikamkuta yule yule mshauri, akaniuliza ninafanya nini, nikamwambia ninasoma form five na nikifungua naenda kuanza form six.

alishangaa sana maana nilionekana mdogo sana kwa mimi kuwa advance, akasema hongera sana baada ya kuniuliza masomo nayochukua.

akanichoma na kuchukua damu tayari kwa kuipima.

NIKARUDI KUSUBIRIA MAJIBU ILI WENGINE WAKATOE DAMU PIA.

WAKATI WA HOFU KUBWA KULIKO WAKATI WOWOTE IKAWA KUYASUBIRI HAYO MAJIBU.

kila mtu alizidiwa na hofu kiasi kwamba baadhi yetu wakataka kuyakimbia majibu hata kabla hayajatoka.

wakati huo hata mimi ujasiri wa kuyasubiria majibu yangu unazidi kupungua na nikawa naona ingekuwa vyema kama nisingeyachukua.

kwenye wengi haliharibiki jambo, akajitokeza mmoja kati yetu akatutia moyo na kutuambia tujikaze tu tusiyakimbie majibu maana tulienda pale tukitaka kujua hali zetu.

nikakumbuka kuwa nilifika pale nikiwa na ujasiri mkubwa na nilishaamini tayari nina ukimwi, nikaona liwalo na liwe.

nikayasubiri majibu.

MARA MSHAURI HUYU. wote tunamkodolea macho tukiwa tunatia huruma huku wote hatujui hatima yetu.

akasema atatuita mmoja mmoja kwenda kuchukua majibu.

zamu yangu ikafika.

nikaingia chumba maalumu cha kutolea majibu.

mshauri:karibu

mimi: kimyaaaaaa nikiwa nimejaa hofu.

mshauri:una mpenzi?

mimi:ndiyo

mshauri: wangapi?

mimi:mmoja.

mshauri:vipimo tayari vimeshatoa majibu na majibu ninayo hapa(aliongea huku akiniangalia.
)akaendelea "je upo tayari kupoke majibu yako?"

mimi:ndiyo(niliitikia kwa hofu na unyonge)

mshauri:je kama utakuwa umeathirika utajisikiaje?

mimi: nitajikubali na kuishi kawaida.(mapigo ya moyo yalikuwa yamepanda)

mshauri:je kama hautakuwa umeathirika utajisikiaje?

mimi:nitajilinda

mshauri: kwa leo hatujaona, you have to undergo total abstinence(mshauri aliongeza maneno hayo kwa kimombo akinitaka niachane kabisa na mapenzi)

mimi: ahsante( sikumbuki tena mule chumbani niliondokaje na sijui kama niliaga, ila nachokumbuka ni kwamba kwa kiasi fulani mawazo yalipungua.)

JE MAJIBU YA ANGAZA KUWA NILIKUWA SALAMA YALISAIDIA AMA HAPANA BAADA YA HAPO? tuendelee na stori kujua nini kiliendelea.

kimsingi majibu ya ANGAZA sikuyaamini kabisa kwa kuwa tayari nilikuwa nimejenga hisia na kuamini nilikuwa nimeathirika na hivyo majibu yale hayakuweza kunirudisha katika hali ya kawaida kama ambavyo kila msomaji angetegemea maana nilifikiria huenda angaza wameamua kunipa moyo ili niendelee na masomo yangu na pengine CD4 zangu waliona zingeweza kunisogezasogeza.

SIKU MOJA TU BAADA YA SHULE KUFUNGULIWA NIKAPATA TAARIFA MBAYA KUHUSU SHULE YANGU.

mzee alinipigia simu(wakati huu nilikuwa nina simu), nakumbuka ilikuwa mida ya saa moja jioni.
akaniuliza kama nina taarifa yoyote kuhusu shule yangu. nikamwambia sina taarifa yoyote, akaniambia "muda mfupi imetangazwa kuwa shule yangu imechomwa moto baada ya wanafunzi kugoma na kuichoma moto"

ilikuwa ni taarifa nyingine mbaya kwangu tuliyekuwa tunasoma nae advance , nikampigia simu rafiki yangu kama naye alikuwa na taarifa zozote, akaniambia ndio shule yetu imechomwa moto na hatima haijulikani itakuwaje.

STAY TUNED:
masikio yangu yote nikawa nataka kujua nini kitaendelea shuleni.

kesho yake naibu waziri wa elimu wakati ule akiwa MWANTUMU MAHIZA, alifika shuleni kwetu na kutangaza kuifunga shule kwa muda wa mwaka mzima ili kupisha ukarabati na ikatangazwa bungeni kuwa shule imefungwa mwaka mzima.

baadae nikataarifiwa kuwa O LEVEL wote watarudishwa shule za kata na form five watahamishiwa shule zingine ila sisi form six hakukutolewa maelezo yoyote maana ilionekana ndio tulikuwa tatizo na kifupi tulikuwa tumeachwa kabisa.

TUKIO HILI LA KUCHOMWA KWA SHULE LIKANIFANYA NIENDELEE KUKAA NYUMBANI KWA MUDA USIOJULIKANA MPAKA HAPO HATIMA YETU ITAKAPOAMULIWA NA SERIKALI.

nilikaa mpaka mwezi wa tano ambapo shule yangu ya o level nayo ikafunga na wanafunzi wakawa likizo.

wakati huu wote , hali yangu ikiwa haijaimalika maana bado siamini kama sina ukimwi.

nilikuwa na rafiki yangu mwingine aliyekuwa anasoma shule ile niliyosoma o level(kumbuka ni eneo hilohilo tunapokaa).

huyu hakuwa rafiki yangu sana maana urafiki wetu ulitokana na mimi kumpenda kwa sababu alikuwa mzuri sana darasani wakati huo nilipokuwa nasoma o level, na yeye aliniona kama kaka yake hasa kwa kuwa na mimi nilikuwa nafanya vizuri darasani wakati nilipokuwa pale.

KWA NINI HUYU ANAINGIA KWENYE STORI HII.?

endelea ili uone kilichokuwa kimejificha nyuma ya pazia.

mpaka muda huu sikuwa namfahamu jamaa aliyenichukulia demu wangu zaidi ya kumsikia jina tu.

huyu rafiki yangu alikuwa na urafiki wa karibu sana na vijana wengine wawili, kati ya hao rafiki zake wawili mmoja wao ndiye aliyekuwa amemmiliki demu wangu baada ya mimi kuondoka kwenda kusoma mbali.

kwa kuwa sikumfahamu kabisa huyo jamaa ,nilijikuta nimekutanishwa naye kupitia huyu rafiki yangu bila kujua kama ni yeye maana hata hatukuwahi kuzungumzia mambo ya wasichana na jamaa yangu, hivyo hata mimi sikujua kama rafiki yangu alijua chochote juu yangu wala msichana wangu.

kwa kuwa tuliendelea kuwa pamoja muda mwingi na jamaa yangu, tulijikuta urafiki unakuwa mkubwa zaidi na tukawa tunatembea wote karibu muda wote maana mimi sikuwa na jambo lolote la kufanya baada ya shule kukosa mwelekeo.

IKATOKEA SIKU MOJA TUKAENDA KUTEMBEA MBALI VICHAKANI KWA MIGUU NIKAANZA KUMSIMULIA HUYO RAFIKI YANGU HABARI ZA DEMU WANGU.

tofauti kabisa na nilivyokuwa nafikiria, kumbe jamaa yangu alikuwa anajua kuwa yule ni msichana wangu na akaniambia, "BWANA YULE DEMU WAKO ALIKUWA ANAKUPENDA SANA" (kumbuka wakati huo demu wangu alishaondoka kimoja toka mwezi wa pili na hapo ilikuwa mwezi wa sita, hivyo haikuwa na maana sana zaidi ya stori kwa kuwa hata sikuwa na matumaini ya kumuona tena)

baada ya jamaa kuniambia yule demu wangu alikuwa ananipenda sana, nikataka kujua kwa sababu ipi maana nilikuwa najua demu mwenyewe nilipoondoka tu alimilikiwa na wajanja.

jamaa akaniambia yule demu wako alikuwa mwaminifu sana sijapata kuona.

nikamwambia, mbona demu mwenyewe nilipoondoka tu akawa anachukuliwa na jamaa anaitwa QQQ,

Jamaa yangu alicheka sana, mimi nikawa namshangaa iweje acheke baada ya kusikia vile.

akasema ni uongo , QQQ hajawahi kumchukua yule demu wala hakuwahi kukubaliwa.

mmmmmmmmh, niliguna na kustaajabu, nikashawishika kujua zaidi habari hizo zilizokuwa zinanihusu na kumhusu demu wangu na yule jamaa.

nikamwambia anieleze baada ya kunihakikishia kuwa anajua A-Z kuhusu stori zote za demu wangu na jamaa wote waliokuwa wanamtongoza baada ya mimi kwenda mbali kusoma.

HII NDIYO ILIKUWA SIMULIZI YA JAMAA YANGU

" kwa mara ya kwanza ilikuwa likizo ya mwezi wa nane mwaka jana, yule demu wako alikuja mashineni kusaga unga, pale pembeni yake na mashine ndo alikuwa akiishi QQQ ,alipomuona yule demu wako akamfata na kumwambia kuwa alikuwa na barua ambayo ilikuwa ni ya mjomba wake na demu wangu, hivyo akamwambia akimaliza kusaga akaichukue barua na alimwelekeza ni chumba kipi alimokuwa, yule demu baada tu ya kumaliza kusaga mashineni akaenda ndani kwa jamaa, demu wako alipoingia tu ndani jamaa akafunga mlango ili asex na demu wangu bila hata kumtongoza, sisi tulienda dirishani kusikilizia, yule demu baada ya kuona mule ndani hakukuwa na barua yoyote ya kupeleka kwa mjomba wake na wakati huo jamaa anamlazimisha kusex, demu alimwambia amwache na akawa ametishia kupiga kelele anabakwa, baada ya jamaa kuona vile ikabidi amfungulie demu akatoka bila kufanya chochote"

SJUI MSOMAJI UMEPATA PICHA GANI MPAKA SASA, LAKINI MIMI KIDOGO NIKAWA NIMEANZA KUPATA MWANGA KUHUSU STORI AMBAZO NILIKUWA NIMESIMULIWA KABLA KUHUSU DEMU WANGU.

Jamaa aliendelea "baada ya siku ile demu wako na QQQ wakawa wamekosana kabisa, baada ya likizo demu wako alienda kupanga chumba kwa MR.LLL, na QQQ naye akahamia na kupanga kwa MR.LLL, hivyo wakawa pale wote huku wakiwa wamekosana kabisa,taratibu QQQ alijenga urafiki na demu wako mpaka ikafikia kipindi wakawa marafiki hasa, wakawa wanatembea wote mtaani, baada ya hali ile kuwa vile QQQ alipata matumaini kuwa huenda ndio ulikuwa wakati muafaka wa kumpata demu, alimtongoza tena, lakini tofauti na matarajio yake demu alikataa, ikabidi rafiki zake wengine wamsaidie, na kwa harakaharaka waliona ingekuwa rahisi kumpata kama wangemtongoza kwanza rafiki yake ili amshawishi, wakafanya hivyo lakini bado haikuwezekana"

MWISHO ILIKUWAJE? endelea kusoma maelezo kama nilivyosimuliwa pia.

"wapambe wa jamaa walizidisha harakati za kumshawishi demu wangu, ikatokea siku moja demu akakubali, kwa kuwa demu na QQQ walikuwa wamepanga nyumba moja, demu akamwambia mmoja kati ya wapambe kuwa amekubali baada ya mazungumzo maraefu ila akaomba apewe dakika tano za kujiandaa ndio QQQ aje ndani"

HUKU NAENDELEA KUMSIKILIZA JAMAA YANGU AKINISIMULIA TENA KWA MAKINI SANA BILA HATA KUMUULIZA SWALI NILISHANGAA KUONA DEMU WANGU KUMBE ALIKUBALI.

anyway endelea kusoma uone nini kilitokea baada ya jamaa kuingia ndani.

"QQQ alipelekewa taarifa kuwa demu ameshakubali ila anapaswa kusubiri dakika tano tu alafu aende ndani kwa demu, QQQ alifurahi sana na kuziona dakika tano zilikuwa ndefu sawa na mwaka mzima maana alimpenda sana yule demu, hatimaye saa ikahesabu dakika ya tano na QQQ akaingia ndani huku akiwa na furaha isiyoelezeka moyoni, sisi kama kawaida yetu tukazunguka dirishani ili tushudie kinachoendelea baada ya jamaa kumsotea demu kwa muda mrefu, alipoingia tu ndani akakutana na mazingira ambayo yalimshangaza na hakuyategemea na alipigwa na butwaa"

NINI ALIKUTA? ENDELEA KUSOMA.

"alipotazama mezani hata kabla hajakaa aliona kwa mara ya kwanza meza yote IMEPAMBWA KWA KADI NYINGI ZA MAPENZI NA UPENDO NA BARUA NYINGI ZIKIWA ZIMEZAGAA MEZANI, huku demu anamkaribisha ndani, QQQ alishindwa kujikaza na kuamua kuuliza zile kadi zote ni za nani wakati yeye alishawahi kutuma kadi moja tu? demu wangu alimwambia ni za mpenzi wake anayempenda sana, QQQ aliishiwa nguvu na kumuuliza demu ni nani mwenye hizo kadi, japo alikuwa anajua? demu akamwambia azifungue mwenyewe atasoma jina limo kwenye kila kadi na kila barua,QQQ hakutaka hata kufungua asome maana alijua ni za nani, kwa mara nyingine ikadhihirika kuwa hakukuwa na namna ya kumpata yule demu kwa kuwa alikuwa anakupenda sana"

MSOMAJI, HAPA NIKAWA NIMESAHAU KWA MUDA HABARI ZA UKIMWI NA KUAMINI KABISA KUWA KUMBE NI KWELI DEMU WANGU ALIKUWA ANANIPENDA SANA KAMA JAMAA YANGU ALIVYOKUWA ANADAI.

LAKINI HAPO HAIKUWA MWISHO WA STORI YENYE UTATA NA MIKASA MINGI JUU YA QQQ.

endelea kusoma maelezo ya jamaa.

"baada ya zoezi la kumpata kushindikana QQQ aliendelea kuwa rafiki mkubwa kwa demu, huku wakiendelea kutembea wote mtaani kila jioni baada ya shule, QQQ hakukata tamaa, ilikuwa siku moja ambapo aliamua kuingia ndani katika chumba cha demu wako na kuzima taa mara tu alipoingia ndani akitaka kutekeleza adhima yake ya kusex na demu, demu alishituka na kuamua kupiga kelele anataka kubakwa,maana alishangaa kuona kitendo cha mwanzo kinajirudia na hakuamini kama ingekuja kutokea tena kwa kuw QQQ alishaomba msamaha na kutumua kadi ya kuomba msamaha baada ya jaribio la awali la kumbaka kushindikana, hapo ndo QQQ na demu wakawa wamekosana kimoja, lakini kwa kuwa tayari QQQ alikuwa ameshatangaza kuwa yule ni demu wake na tukio lile limewakosanisha na hawatembei tena pamoja basi akamzuishia kuwa ana HIV ili akiulizwa kwa nini wameachana ama amemuacha ajibu vile ili kujiokoa na aibu kuwa ameachwa japo hakuwahi kummiliki"

aaaaaaaaaaah, HAPO NDIPO NIKARUDISHA HISIA ZANGU NA KUMBUKUMBU NYUMA NA UKWELI ULIOKUWA UMEJIFICHA NYUMA YA PAZIA UKAJULIKANA.

kwanza niliionaga ile kadi ya kuomba msamaha-kumbe aliituma baada ya jaribio la kumbaka kushindikana ili kuweka mambo sawa,

pili niliambiwa jamaa anammiliki demu-kumbe alijitangazia tu kutaka sifa kisa alikuwa karibu nae.

tatu niliambiwa ana ukimwi- kumbe alimzuishia baada ya jaribio la pili kutaka kumbaka kuwakosanisha moja kwa moja.

HAPO NDIPO HOFU YA KUWA NINA UKIMWI IKAWA IMEONDOKA KABISA NA MAJIBU YA ANGAZA NIKAYAAMINI KUWA YALIKUWA SAHIHI.

Jamaa yangu aliendelea kunisimulia stori za kusikitisha alizokumbana nazo demu juu ya wavulana wengine waliokuwa wamemtongoza, ili kunidhihirishia ni jinsi gani demu wangu alikuwa ananipenda na mwaminifu.

jamaa aliendelea

"kuna jamaa mwingine anaitwa DDD, naye alimfatilia sana mpaka siku moja alikuja geto akawa amekaa mpaka usiku sana saa tano saa sitahivi ndipo naye akataka kumlazimisha wasex, ilikuwa vurugu demu akatoka nje kuja kutafuta msaada baada ya kuona jamaa hataki kuondoka anang'ang'ania kulala huku akiwa ameshamkataa, ndipo mwenye nyumba MR.LLL alipoona na kuja kumtimua"

BAADA YA STORI ZILE ZOTE, HAKUNA HATA CHEMBE YA MAELEZO AMBAYO NILIHISI JAMAA YANGU AMEDANGANYA.

lakini nilijifunza somo kubwa sana juu ya tabia ya mpenzi wangu , kuwa pamoja na kwamba alikuwa mpole sana lakini hakuwa na uwezo wa kutoa maelezo mengi zaidi ya kuniambia haikuwa kweli na kila nilipomuuliza maswali mengi aliishia kulia tu.

PAMOJA NA KWAMBA DEMU WANGU ALISHAONDOKA LAKINI NILIZIDI KUMPENDA ZAIDI BAADA YA KUONA ALIVYOKUWA ANANIPENDA JAPO SIKUJUA KAMA ANGEWEZA KUWA MWAMINIFU KIASI KILE.

(kufupisha stori, niliweza pia kuongea na QQQ maana naye tayari alikuwa ameshakuwa rafiki yangu pamoja na rafiki yake yake, wote walieleza ukweli na kuyadhibisha maneno yote niliyosimuliwa, ila nilipowafata sikuwaambia kama nilisimuliwa na rafiki yao, hivyo baada ya kumwambia QQQ kuwa nilikuwa najua kila kitu, aliamini kuwa ni kweli ninajua na akajua demu wangu ndiye aliyenisimulia, hivyo naye akaeleza sehemu ndogo ya tukio la kukuta zile kadi zimewekwa na maelezo hayakutofautiana, hata walionieleza mwanzo habari za demu wangu nao niliwauliza wakasema jamaa ndiye aliyezusha uongo)

NIKIWA NIMEKOLEA NA MAISHA YA MTAANI , NIKAPATA TAARIFA NYINGINE YA FARAJA KUBWA BAADA YA ILE YA KUJUA UKWELI JUU YA DEMU WANGU.

IPI HIYO?
taarifa ikawa ni kwamba shule yetu imefunguliwa na form six tunatakiwa kuripoti ndani ya siku chache sana.

SASA NAELEKEA SHULENI FORM SIX NIKIWA MZIMA, NIKIJUA MPENZI WANGU ALIKUWA ANANIPENDA SANA NA NIKIWA NIMEJAWA NA SHAUKU YA KUMTAFUTA MPAKA NIMPATE KWA VYOVYOTE VILE MAANA ILIKUWA LAZIMA NIFIKIE DAR KABLA YA KUFIKA RASIMI SHULENI.

LAKINI NIKIWA SIJUI ANAPOISHI, JAPO ALISHANIDOKEZEA TU, ILA DAR NI KUBWA SANA KUMPATA MTU KAMA HUNA MAWASILIANO NAYE.

JE NILIMPATA AMA SIKUMPATA NA ILIKUWAJE? nitaendelea siku nyingine kama itawapendeza.
but the story is always interesting.

NARUDIA TENA HII NI STORY YA KWELI.

MSOMAJI KAMA UMEFIKA MPAKA HAPA POLE NA HONGERA LAKINI KWA KIASI KIKUBWA UTAKUWA UMEJIFUNZA KITU.

Kitabu cha Obama same strory
 
Hii story ina element nyingi za uhalisia. Hii shule iliyochomwa ikafungwa kama naikumbuka hivi....sio Kibiti secondary kweli?
 
Mshinga mbona haijaisha!??

niliogopa kuiandika yote, na kimsingi ni ndefu sana na matukio ni mengi sana na nikawa nahisi kuchosha wasomaji.

Nitaimalizia kwa kuongeza vipande viwili tena ama kimoja kama inaweza kuwa sumarized.
 
Last edited by a moderator:
Hii story ina element nyingi za uhalisia. Hii shule iliyochomwa ikafungwa kama naikumbuka hivi....sio Kibiti secondary kweli?

ha ha ha ha ha ha ha, ndio mana najitahidi sana kuweka encryption ili kuzuia wahusika kujulikana wote humu, ni kweli that is the school, hujakosea.KILA KITU HAPA NI UHALISIA KWA 100%,nikuhakikishie hilo ila story kuna sehemu nimeikata kuipunguza ila sijaongeza chumvi hata
 
ha ha ha ha ha ha ha, ndio mana najitahidi sana kuweka encryption ili kuzuia wahusika kujulikana wote humu, ni kweli that is the school, hujakosea.

Hah inabidi unishukuru, niliplay part flani kulinda maslahi yenu.
 
have you recognized me? I dont think so. Ila ni rahisi kuijua shule kwa identification niliyotoa.

Wahusika wote wakiona hii watajua tu ila nina uhakika wewe si kati ya hao. Te te te
 
ha ha ha ha relax mkuu nlikuwa nakuchemsha! naikumbuka shule nilikuwepo kwenye kamati ya Mwantumu ya kuchunguza chanzo cha vurugu.
 
Moyo wa mtu ni kichaka: Twanga pepeta.

Interesting story
 
kuandika story nacho ni kipaji, kama mwenzangu na mimi ulikuwa unapa sifuri kwenye "insha" usitegemee miujiza ukubwani!

moyo wa mtu ni kichaka: Twanga pepeta.

congrats, una uandishi usiochosha

sent from my blackberry 9300 using jamiiforums

na subscribe, na uendeleze kwenye sredi hii hii.:cool::cool::cool:

moyo wa mtu ni kiza kinene.........endelea kaka

leta mwendelezo hapahapa mkuu

wooooow, ikopouwa sana.......mwendelezo plz!!

imenivutia

uhh,nmesoma mwanzo mwisho..mapenzi hayaa...kwa mujibu wa kichwa cha habari inasikitisha u guys parted ways wakati mnapenda that much..

wow umefikia wapi sasa? Naye amejua hana ukimwi au? So kusema kuachwa solemba ndio utasema baadae?

Haya wai kabla hatujasahau una story hii.

nashukuru kuwa mmoja wa waliokupa moyo wa kuiendeleza story hii. Tupo wote mwanzo mwisho

sent from my blackberry 9300 using jamiiforums

very interesting story...

kitabu cha obama same strory

mshinga mbona haijaisha!??

hii story ina element nyingi za uhalisia. Hii shule iliyochomwa ikafungwa kama naikumbuka hivi....sio kibiti secondary kweli?

afadhali wewe umesema

interesting story
nimeiendeleza tena, i hope nitaweza kuandika sehemu ya mwisho hata kama itakuwa ndefu ila nitaiandika yote. Posibly kesho kutwa. Ama kesho nikiweza.
 
Back
Top Bottom