Muungano: VP na Waziri wa Afya, hili si la Muungano. Msiliingize Kinyemela

MGAO WA FEDHA ZA KODI ZITOKANAZO NA WAFANYAKAZI WA MUUNGANO

Wazanzibar wakieleza malalamiko husemwa ni 'kero za Muungano' Watanganyika inasemwa ni chuki.

Watanganyika wanapoeleza ya moyoni hupuuzwa. Prof Magamba alisema ' wakiyatoa Muungano upo matatizoni'

Kati ya kero za Wazanzibar zilizotatuliwa na awamu ya sita ni fedha za Bajeti 4.5% iliyokuwepo hadi 9% ya Rais SSH kama alivyobainisha mwenezi wa CCM bwana Mbeto.
Pili, kuwa na 21% ya Watumishi wa Muungano- iliyowekwa na Waziri Mchengerwa wakati huo

Haikuwekwa wazi 21% ya nafasi za Muungano zinahusu maeneo gani.
Inafahamika kila lenye jinaTanzania ni la Muungano hivyo ajira 21% zinahusu yasiyo ya Muungano pia

Kutoa 21% kwa Wazanzibar ni 'kuficha ukweli' kwamba ajira zinatolewa Wizara zisizo za Muungano kama TAMISEMI, Afya, Madini, Kilimo, Maji, miundo mbinu, Elimu, Maliasili, Ujenzi , Mawasiliano n.k. na Taasisi kama Tanzania Bureua Standards, Bandari n.k. si sehemu ya 21%.

Utaratibu huo unawanyima Watanganyika fursa kwa kuwapa Wazanzibar 21% na pia 79% za Tanganyika
Kwa utaratibu huu, Wazanzibar wana fursa hizi za ajira
1. Kutoka SMZ ambapo Watanganyika hawaruhusiwi
2. 21% zilizotengwa mahususi kwao na si kwa mkoa mwingine wowote
3. Uwezo wa kuomba kutoka 79% ya Tanganyika wakitumia jina ' Tanzania''

Watumishi wa Muungano wanalipa kodi. Zanzibar ililalamika haipewi kodi za Watumishi hao kama kutoka JMT ambayo ni Tanganyika. Utaratibu umewekwa, kodi za Watumishi wa Muungano sehemu ipewe Zanzibar.

Kisichoelezwa ni Watumishi kutoka wapi.
Kwa maneno mengine kodi za Watumishi wa TAMISEMI, Elimu, Kilimo, Madini, Ufugaji , Ujenzi, Maliasili na Taasisi zisizo za Muungano zinapelekwa Zanzibar kama mgao wa kodi za Watumishi JMT.

21% ya Watumishi wa Muungano kutoka Zanzibar inalipwa na fedha za Tanzania ambazo ni za Tanganyika.
Yaani Zanzibar wanapewa nafasi 21% halafu Tanganyika wanabeba mzigo wa mishahara na mafao yao.

Haijaelezwa mchango wa Zanzibar katika Muungano kutoka Bajeti ya Muungano, au ya Zanzibar
Gavana wa Bank Kuu marehemu Ndulu alisema Zanzibar haijachangia Muungan takribani miaka 40+

Ni Wazanzibar hawa wanaolalamika mambo ya Muungano kuingizwa kinyemea.
Wanapoajiriwa katika taasisi na Wizara zisizo za Muungano , wanakaa kimya. UNAFIKI.

Hitimisho: Wazanzibar wanapata yafuatayo kwa gharama za Tanganyika
1. Hawachangii Muungano na hakuna takwimu zinazoonesha hivyo
2. Wanapata 21% ya ajira za Muungano ambazo pia zinahusu maeneo yasiyo ya Muungano
3. Hawalipi mishahara ya 21% ya watumishi inayopewa kwa jina la Watumishi wa Muungano
4. Wanalipwa kodi zinazotokana na 21% ya watumishi wasiowalipa wao na wanaopatikana maeneo yasiyo ya Muungano.
 
KUELEKEA KILELE CHA MUUNGA

TAASISI ZA MUUNGANO NI ZIPI?

Gazeti la Mwananchi la April 14 limeandika Rais wa Zanzibar Mh Mwinyi kuzindua wa sherehe za Muungano.
Katika uzinduzi huo Mh alitembelea mabanda ya Taasisi za Muungano kujionea shughuli.
Akiongea, Mh alisema serikali zote mbili zinaendelea kutatua kero za Muungano.

Hoja: Kwa kawaida sherehe za Muungano hufanyika uwanja wa Taifa. Pengine katika kuimarisha muungano inaonekana ni muhimu kufanya Zanzibar hata hivy gharama za kusafirisha watu na malipo ni mzigo kwa mlipa kodi

Rais Mwinyi ameongelea kutatua kero za Muungano za Wazanzibar kwasababu wana eneo la kusemea kupitia SMZ. Watanganyika wamefinyangwa kwa jina la Tanzania hawawezi kuwa na kero
Tanzania ambayo Zanzibar imo ndani yake haiwezi kuwa na kero na 'mshirika' wake Zanzibar.

Anachosema Rais Mwinyi kwa tafsiri ya hali ilivyo ni kwamba utatuzi wa kero za Zanzibar unaendelea.
Inaposemwa utatuzi wa kero za serikali mbili ni kuwadanganya Watanganyika. Wao hawana serikali.

Tanganyika haina mwakilishi, kero zake haziwezi kuorodheshwa kwasababu zimewekwa ndani ya Tanzania
Ni kwa msingi huo utatuzi wa kero hauwahusishi Watanganyika ambao ndio walipa kodi pekee wa Muungano.

Pili, kuna hoja ya Taasisi za Muungano. Huu nao ni uongo tu. Huwezi kuwa na Taasisi za Muungano zenye mbadala Zanzibar. Taasisi takribani asilimia 99 zina mbadala Zanzibar. Hizi zinazoitwa za Muungano ni za Tanganyika.

Hizi Taasisi za Muungano zinapelekwa Zanzibar kwenye maonyesho kwasababu rahisi.
Kwamba, zibebe uhalali wa Muungano ingawa zinagharamiwa na Tanganyika kwa 100% na ni za Tanganyika. Zanzibar wana Taasisi zao na wala hawawajibiki na hawajawahi kuhudumia Taasisi za Muungano
Taasisi hizo zinapokelewa kwa mikono miwili Zanzibar si kwababu ya utendaji bali kwa FURSA zinazotokana hasa ajira.

Ikiwa hizi ni taasisi za Muungano, ni muhimu ikaonyeshwa Zanzibar inachangia nini katikakuziendesha
Bila kuonyesha mchango wa Zanzibar, maswali yanajitokeza.
Zile 21% za ajira za Taasisi za Muungano ni za nini ikiwa hakuna asilimia ya mchango kutoka Zanzibar
Je, hili si kuwadhulumu Watanganyika fursa za Taasisi zao zilizopachikwa jina la Tanzania!!

Kuelekea sherehe za Muungano, viongozi wasijidanganye kwamba hali ni shwari.
Haya makongamano na maonyesha huko Zanzibar ni kwa ajili ya kujaza Hotel na kukuza uchumi lakini kero za Muungano si kero tena ni adha.

Kuwatenga Watanganyika kwa kuwafanya mazuzu ni jambo la hatari kwa maana hoja ya Utanganyika ipo mezani.
Mbele ya safari, Watanganyika watakapoitaka Tanganyika yao kwa nguvu hakutakuwa na muda wa kujadili kero.

Prof Palamagamba alisema '' Watanganyika wana yao ya moyoni, wasikilizwe maana siku wakiyatoa itakuwa tatizo''
 
TANGANYIKA ILIPE GHARAMA ZA RAIS MSTAAFU WA ZANZIBAR?

Katika mazingira ya kawaida Mbunge wa Bunge la JMT anatarajiwa kuwa na ufahamu mkubwa na mambo ya serikali kwasababu ana uwezo wa kupata habari kutoka vyanzo bila kukwaza.

Kilichotokea Bungeni kinatia shaka na uelewa wa wawakilishi wetu.

Mbunge Suleiman Haroub kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar anayeingia Bungeni Dodoma ameuliza mipango ya kumsaidia Rais mstaafu wa Zanzibar Salimin Amour nyumba yake inamegwa na mmomonyoko wa ardhi na anaishi katika mazingira magumu.

Amesema pia shule aliyosoma Mh Karume , Rais wa kwanza ipo katika hali mbaya

Hoja ya Mbunge huyo wa Zanzibar akiwa Dodoma ni kutaka JMT ichukue jukumu la kumhudumia Rais wa Zanzibar
na pia kutengeneza shule aliyosoma Rais wa Zanzibar Mh Karume

Akijibu swali hilo Waziri S. Jafo alisema JMT haihudumii Marais wastaafu wa Zanzibar ambao hawakuhudumu katika muungano katika ngazi ya Rais na Makamu wa Rais wa JMT.

Hoja: Inajulikana kwamba Rais au Makamu wa Rais kutoka Zanzibar analipwa mafao na JMT ambayo ni Tanganyika.

Kitendo cha Mbunge kuuliza swali tena akitokea BLW kinaonyesha kodi za Watanganyika zinavyotumika.
Kwamba, kodi zihudumie wastaafu wa Zanzibar kama zinavyohudumia wastaafu wengine wa Zanzibar walioajiriwa Tanganyika ikiwemo Taasisi na Wizara zisizo za Muungano kwa upendeleo maalumu wa 21%

Kwamba licha ya kupata ajira kwa upendeleo wa 21%, mishahara yao inatoka kodi za Tanganyika na wanaposataafu wanalipwa pensheni na mafao kutoka kodi za Tanganyika.

Kwamba Mbunge wa Zanzibar anadhani ni jukumu la kodi za Tanganyika kujenga shule za Zanzibar

Ikiwa Zanzibar inapewa sehemu yake ya misaada, mikopo na kisha 9% ya Bajeti ya Tanganyika na zaidi ikikusanya kodi zake zisizoingia Hazina Dar es Salaam, ikiwa haina mchango mwingine katika fedha za JMT ni kwanini bado Wazanzibar wanadhani wana haki ya kutumia rasilimali za Tanganyika kwa jina la Tanzania hata kwenye mambo rahisi ya kuhudumia viongozi na shule zao!!! .

Je huyu Mbunge kutaka Rais wa Zanzibar ahudumiwe kwa gharama za kodi za Watanganyika na shule zikjengwe kwa gharama za kodi za Tanganyika, huu si Unyemela wakuingiza mambo yasiyo ya Muungano ambao Wazanzibar wanaukataar? Je, si unafki!

Tanganyika haiwezi kufanywa '' cash cow' kwa maana chimbuko la pesa za Zanzibar kila uchao
Kutumia jina la JMT kuchukua rasilimali zake ni jambo litakaloendelea midhali hakuna Tanganyika.

Bila Tanganyika hakuna msimamizi wa Rasilimali za Tanganyika
 
KUELEKEA MIAKA 60YA MUUNGANO
MZEE WARIOBA AHOJI ''KERO ZA UANI'' ASEMA HATA YEYE HAZIJUI

MAKONGAMANO YAFANYIKA ZANZIBAR. WAZANZIBAR WADAI FORMULA ZA KUPEWA BILA KUWAJIBIKA


Kuelekea miaka 60 mengi yanatokea. Juzi Mzee Warioba (Mwanasheria mkuu wa Serikali, Wziri wa Sheria , Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais, Mwenyekiti wa Tume ya Mbadiliko ya Katiba) alizungumza na Gazeti la Mwananchi kama ulivo utaratibu wake wa kuzungumzia masuala ya kitaifa yanapojiri.

Wariona ni mmoja wa ''Vijana'' wa Mwl Nyerere na Mzee miongoni mwa Wazee waliobaki wanaozungumza kwa 'mamlaka' au authority. Unaweza kutofautiana na maoni ya Mzee Warioba, usichoweza kubisha ni uwezo wake wa kutumia Elimu na Uzoefu katika masuala ya kitaifa nakimataifa katika kujenga na kutetea hoja zake

Kumpinga Mzee Warioba si jambo baya au geni lakini kumpinga lazima awaye ajiandae kujibu hoja zenye mantiki za mzee Warioba. Ni kwa muktadha huo, tutajadili hoja zake kuhusu miaka 60 ya Muungano kama alivyozungumzia

Hoja ya kwanza;
Mzee Warioba alikemea viongozi kutumia maneno '' Serikali ya Bara'' wakimaanisha ya JMT au serikali za pande mbili ( si serikali ya nchi moja).

Hoja ya Mzee ina maana kwamba ukisema serikali ya Bara tayari ni serikali ya Tanganyika na unaondoa ya JMT.
Inaposemwa Serikali za pande mbili, swali linakuja ni zipi hizo? Tuna ya Zanzibar na ya pili ya JMT ambaye Zanzibar ni mshirika. Kwa maana kwamba wanaosema serikali ya Bara wanamaanisha ni ya upande wa pili ya JMT.

Hoja ya Pili;
Mzee akasema , sheria ya Zanzibar ya Ukaazi ina matatizo.
Akatoa mfano wa mtu wa Unguja anapokwenda kuishi Pemba akirudi Unguja kabla ya miaka 3 hawezi kupiga kura.

Mzee Warioba akasema lakini Mzanzibar huyo anaweza kujiandikisha eneo lolote la Tanganyika na kupiga kura bila kujali ameishi eneo hilo kwa muda gani. Hoja ya Mzee ni kwamba sheria za Zanzibar zina ubaguzi ndani ya Zanzibar lakini pia katika JMT zikitoa nafasi za Wazanzibar kutumia Muungano wakati huo zikiwabagua Watanganyika.

Tuna mifano mingi ikiwemo wa Rais H.Mwinyi aliyekuwa Mbunge wa Mkurunga na sasa ni Rais wa Zanzibar.
Kwamba ni haki Mzanzibar kugombea nafasi au kuajiriwa Bara lakini kuna sheria zinazbagua kule Zanzibar
Kwamba Wazanzibar wanapewa uoendeleo wa kufanya ubaguzi lakini pia kupewa fursa za Muungano.

Hoja ya Tatu;
Mzee Warioba anahoji kuhusu sheria ya Diaspora akioanisha na ubaguzi uliopo Zanzibar
Anasema wakati Serikali inawapa Diaspora hadhi maalumu, uwepo wa sheria za kibaguzi Zanzibar utazua tatizo.

Na mwisho Mzee Warioba akaongelea kero.
Katika kero Mzee amaeshanga kwamba hazielezwi kwa Wananchi na hata yeye hajui ni zipi.
Anachosikia ni kwamba zimepunguzwa kwa namba lakini haelewi wala Wananchi hawajui ni kero zipi.

Mzee Warioba anaphoji suala kama hili kwa uzoefu na nyadhifa alizowahi kutumikia ni jambo zito sana.

Kwamba hata yeye hajui kero ni zipi na anasikia tu namba za kero zikitajwa na suluhu za kuchapia kama si kubandika

Jukwaa hili umewahi kuieleza hoja ya Mzee Warioba kwa kina.
Kwamba Wazanzibar na Makamu wa Rais wanajifungia kisha tunasikia kero zimetatuliwa.
Kero zinazotatuliwa ni za Wazanzibar tu huelezwa kijuu juu.

Makamu wa Rais ni 'Mteule wa Rais' hivyo hatumikia matakwa ya Boss wake

Historia inatuonyesha kwamba VP Mpango amejikita zaidi kutatua kero za Nchi ya Zanzibar

VP walipita walisimama na kuhoji masuala mazito yanayogusa pande zote ndiyo maana Mzee Warioba anashanga uatatuzi wa kero tusizozijua. VP Mpango amekuwa facilitator wa kero za Wazanzibar akilenga mahesabu ya mbali.

Ni haki kusema, kero zinatatuliwa na Wazanzibar wakisaidiwa na Makamu wa Rais

Katika utatuzi wa kero Tanganyika haina mwakilishi na hapa ndipo tatizo linapoanzia kama alivyoeleza Mzee Warioba

Makamu wa Rais Mpango hajawahi kuuliza kero za Watanganyika kwasababu Tanganyika haipo lakini ni yeye amekuwa msuluhishi wa kero za Muungano. Huu si usuluhishi ni usaidizi wa madai na si kero za Wazanzibar

Ukitaka kuona matatizo ya kero yanayosemwa na Wazanzibar pitia habari hizi mbili hapo chini kwa hisani ya magazeti ya Mwananchi na The citizen.

Tutajadili kinachoitwa kero kama alivyosema Balozi Amina Salum na Hamad Rashid na Wasomi wengine.

Ukiwasikiliza Balozi Amina Salum na Rashid Hamad utajiuliza imaswali mengi juu ya nafasi zao za uongozi.

Balozi Amina na Mh Hamad kama walivyo Wazanzibar wanadhani ni haki ya Zanzibar kupewa tu lakini hakuna haki ya Zanzibar kuwajibika. Wanadhani Muungano upo kuwatumikia lakini wao hawana sababu za kuwajibika

Wahehsimia Amina na Hamad wanadai formula za kupewa hawadai formula za kuchangia au kulipa chochote katika Muungano licha ya ukweli kwamba Zanzibar ni wanaufaika wakubwa wa Muungano

Ni wakati Watanganyika wawaulize Wazanzibar , ikiwa wanadai haki ni wapi wanawajibika katika Muungano!
Wanadhani Muungano ni kuibeba Zanzibar kwa gharama za Watanganyika tena wakidai kama haki!


Tutajadili bandiko lijalo

 
KONGAMANO LA MIAKA 60
YALIYOSEMWA NA WASOMI, WANAZUONI NA WATAALAMU


Gazeti la Mwananchi linaandika kongamano limebainisha maendeleo na faida za kiuchumi na kutokuwepo kwa Tume ya pamoja ya Fedha.

Hoja:
Wasomi wamekuwa waoga kuongelea ukweli wa Muungano, wamekuwa ni 'chawa' licha ya sifa za kitaaluma wakiimba nyimbo za wanasiasa bila tafakuri wakivizia teuzi.

Ukweli ni kwamba maendeleo yapo kwa kila nchi hata bila muungano, hoja ni kuhusu kiasi cha maendeleo.
Hakuna manufaa ya kiuchumi kwa Tanganyika. Zanzibar ina watu takribani 1.5 Milioni na nusu wanaishi Tanganyika. Katika wakati mmoja si zaidi ya watu 700,000 katika visiwa hivyo.. Uchumi wa Zanzibar ni mdogo

Bajeti ya Zanzibar ni Tsh 2.8T kwa 2023/2024 karibia sawa na Bajeti ya Ulinzi ya Tanganyika ambayo ni 2.7T.
Ni Bajeti ya Ulinzi ya Tanganyika 100% ingawa imepewa jina la Muungano ili kuihudumia Zanzibar.

Zanzibar ni soko lisilo na faida, Tanganyika ni soko la watu milioni 60 linalofikika ikiwemo ardhi kwa Wazanzibar .
Tanganyika inatoa rasilimali (10%) ya Bajeti ya JMT kwenda Zanzibar, kiasi kikubwa kuliko Bajeti ya Zanzibar.

Kwa mantiki, Wanazuoni wanalenga kuwapendeza Wazanzibar kwamba ni sehemu ya uchumi wa Tanzania.
Ukweli kwa mantiki na namba, Tanganyika hainufaiki na chochote kiuchumi kwa kuungana na Zanzibar.

Tanganyika inapakana na nchi 8 miongoni ni Burundi na Rwanda zenye watu mililioni 13 na 14 masoko makubwa zaidi ya Zanzibar. Tanganyika kuwekeza miundo mbinu kwenda Burundi/Rwanda itanufaiki kiuchum

Mshiriki wa kongamano mwanasiasa Hamad Rashid amesema changamoto ni kukosekana kwa akaunti ya pamoja ya Fedha na kwamba iwepo ''Formula' ili kuondoa matakwa ya mtu aliyepo madarakani.
Balozi Amina Salum akashadidia akaunti ya pamoja litapata ufumbuzi kwasababu Rais SSH analishughulikia.

Hamad Rashid na Amina Salum hawakufanya utafiti. Anayezuia uwepo wa akaunti ya pamoja ni Wazanzibar
Maneno hayo yamesemwa na Rais wa Zanzibar Mh .Hussein Mwinyi. Mwinyi alisema kuundwa kwa akaunti ya pamoja kutalazimisha Zanzibar ichangie mfuko huko kuendesha mambo ya Muungano. Soma hapa


Balozi na Hamad Rashid waelewe Kwamba Zanzibar utachangia nini ili kuwe na akaunti ya pamoja? Wanachosema Wasomi hao, Zanzibar ichangie sifuri na Tanganyika itoe 10 halafu iwepo Formula ya kugawana ''10 ya fedha za pamoja'' wakidhani Rasilimali za Tanganyika ni za Muungano kwa jina la JMT.

Tanganyika inapobeba gharama za Muungano Wazanzibar wasidhani ni haki yao kubebwa
Pia Balozi Amina na Hamad wameshauri iwepo Formula ya kugawana mapato , misaada na mikopo.

Wasichokijua wasomi hao, kwa miaka zaidi ya 40 kwa mujibu wa Gavana wa BoT marehemu B.Ndulu Zanzibar haijachangia chochote katika Muungano.

Formula wanayoidia Balozi na Hamad ni kugawana mali za Tanganyika.

Watanganyika wana haki ya kuhoji ziko wapi formula hizi'
1. Mchango wa Zanzibar katika Muungano ni upi na iko wapi Formula ya Zanzibar kuchangia
2. Formula ya Zanzibar kupewa mikopo na Formula ya Zanzibar kulipa mikopo hiyo iko wapi
3. Formula ya kugawana misaada na pia Formula iliyotumika kuipa Zanzibar 10% ya Bajeti ya Tanganyika
4. Formula ya ajira ya Watumishi 21% ya Wazanzibar na Formula ya kuwalipa hao 21% kutoka Zanzibar
5. Iko wapi Formula ya kuchangia Taasisi za Muungano

Ni kukosa elimu kudhani Formula ya kugawana inawezekana bila kujua mfuko unagharamiwaje.
Lakini pia Wazanzibar wakaelimishwa kutoongelea kugawana tu, wanatakiwa waongelee pii kuwajibika.

Kwa mfano, Tanganyika inabeba 100% ya Muungano na inatoa misaada mikubwa kwa Zanzibar.
Dar es Slaam inachangia 86% ya Pato la Tanzania, inapewa Rasilimali chache ukilinganisha na Zanzibar (sifuri)

Ndivyo ilivyo kwa mikoa hata michanga kama Geita, Songwe, Njombe ambayo umri wake si zaidi ya miaka 6. Mikoa hiyo inaonekana katika pato la Taifa na mchango wake. lakini inapewa rasilimali kidogo kuliko Nchi ya Zanzibar.

Wakati kongamano linaendelea, ni vema Wasomi na Wataalam wakawaelimisha Wazanzibar, Muungano hauna maana ya KUPEWA, muungano ni kuwajibika.

Kuomba Formula za kupewa bila kuwajibika ni Ujima wa mawazo


Inaendelea
 
KONGAMANO LA MIAKA 60
WASOMI WABWABWAJA BILA HOJA


Bandiko lililotangulia tumeangalia hoja na vioja vya wasomi na Mabalozi wa Zanzibar wakishauri Formula za kugawana rasilimali za Tanganyika kwa jina la Tanzania tena wakilifanya suala hilo kama '' Ni haki ya Wazanzibar''

Tuangalie wasomi wa Tanganyika walisema nini. Dr H.Mwakyembe anasema baada ya Muungano fursa za Wazanzibar kwenda Bara zilipatikana bila ubaguzi

Hoja:
Ni kweli Wazanzibar wanapata fursa bila ubaguzi lakini Dr Mwakyembe hakuzungumzia adha ya ubaguzi wanayokutana nao Watanganyika wakiwa Zanzibar kama ile ya Wamasai kuandamwa na marufuku ya Ndizi

Mhadhiri wa UDSM Dr Idd Mandi alisema Muungano umeleta umoja na kuongeza fursa za uchumi hasa biashara.
Dr Mandi akasema Muungano wa serikali 3 utaongeza gharama, na lipo tatizo la kugawana mapato ya Tanganyika

Hoja:
Msomo Dr Mandi anasema ukweli, Muungano umeongeza fursa za uchumi na biashara kwa Wazanzibar.
Fursa hizo hazina maana kwa Tanganyika kwa kuzingatia ubaguzi, idadi ya watu na uchumi mdogo wa Zanzibar. Kusema kwamba kuna Mtanganyika anafaidika kibiashara ni bla bla za Wasomi zikilenga teuzi za u-DC

Dr Mandi anasema Muungano wa serikali 3 utaongeza gharama bila kuanisha gharama zitaongezeka wapi.
Dr angeeleza ni vipi serikali 2 zinapunguza gharama kwa Mtanganyika aliyebeba mzigo wa serikali 2 peke yake.
Dr Mandi akamalizia kwa kusema kuna matatizo ya kugawana mapato

Hoja:
Dr Mandi anamaanisha mapato yanayotokana na rasilimali za Tanganyika yaliyopewa jina la JMT yanahitaji kugawanwa na Zanzibar. Dr wa UDSM hana habari kwamba Gavana wa BoT alisema Zanzibar haijachangia Muungano kwa miaka 40 wala haelewi gharama za Muungano zmebebwa na Tanganyika peke yake.

Kwamba rasilimali zote za Tanganyika zimegeuzwa za Muungano tena zikigawanywa kwa wingi kwenda Zanzibar kuliko kule zilikotoka ndicho Dr anachosema ni mgogoro wa kugawana mapato

Dr Mandi angefanya utafiti angebaini gesi inatoka Mtwara lakini mapato ya gesi 9% kupitia bajeti ya JMT yanakwenda Zanzibar. Mandi haelewi mkoa wa mchanga wa Songwe una mchango katika pato la Taifa kuliko nchi ya Zanzibar lakini unapata asilimia ndogo sana ya pato la Taifa ukilinganisha na 9% inayokwenda Zanzibar

Dr Mandi aelimishwa kwamba Zanzibar haina Bajeti za mambo makubwa kama Wizara ya Ulinzi.
Ikiwa Zanzibar itatoa 5% ya Bajeti ya Wizara haiyo haitaweza kwa uchumi wake.

Msomi huyu wa Chuo kikongwe alipaswa kuelewa Zanzibar haihitaji kugawana chochote na Tanganyika bali ipewe si kwa stahili bali fadhila kama misaad inayopata sasa ambayo ni mikubwa kuliko Bajeti yake..
Dr Mandi ni mfano wa Wasomi wanaoongea bila takwimu wala ushahidi kama walivyo chawa wengine wa CCM

Msomi mwingine wa UDSM Dr Mbunda alisema watu wenye mitazamo tofauti ya Muungano waalikwe kuelezwa faida za Muungano , akamalizia kwa kusema Dr SSH amemaliza ''kero' na hatarajii kusikia Wazanzibar wakilalamika

Dr Mbunda kama wasomi wengine anashadidia jambo bila kutafuta ukweli.
Hivi Dr Samia kamaliza kero gani za Muungano? Kuwapa Wazanzibar kila wanachotaka zikiwemo rasilimali za Tanganyika ndiyo suluhu ya Muungano?

Mfano Dr SSH alisamehe deni la Tanesco la Tsh 60 Bilioni . Mzigo wa deni hilo unabebwa na mbeba Lumbesa wa Kariakoo na Mama Ntilie wa Igunga au mfugaji wa Tarime. Je hiyo ndio suluhu anayotaka kuiona Dr Mbunda!

Hatudhani wasomi hawa wanayasema kwa bahati mbaya , huenda 'maradhi' ya uchawa yanayoambukiza kwa kasi na kutafuna akili za kizazi cha leo yamewakumba Wasomi huko maktaba na kuzikaimisaha akili zao Lumumba.
 
KONGAMANO LA UVCCM LA MIAKA 60 YA UHURU

STEVEN WASIRA
AWANANGA VILIVYO WAZEE WA CCM WARIOBA, BUTIKU NA SALIM AHMED
APOTOSHA NA KUDANGANYA MAANA YA SERIKALI YA SHIRIKISHO


Tafadhali rejea ;
View: https://www.youtube.com/watch?v=HASebKTjIjQ&t=6041s

Kongamano limefanyika Zanzibar, mengi yameelezwa kama ' video' inavyoonesha hapo juu.
Kuna hoja za Washiriki kwa namna tofauti lakini zote zimelenga kueleza Muungano na Faida zake

Miongoni mwa Wageni maarufu alikuwepo Mzee Steven Wasira aliyehudumu nafasi mbali mbali ndani ya CCM na Serikali zama za Mwalimu Nyerere hadi Rais Kikwete. Mzee Wasira bado anaonekana katika shughuli za CCM akishiriki makongamano, amejikita zaidi katika mambo ya Muungano.

Katika kongamano la jana kuna hoja ilijitokeza ikielekezwa kwa Mzee Wassira.
Hoja ilihusu muundo wa Muungano , kwamba kwanini muundo uwe wa serikali 2 na si vinginevyo.

Katika hali iliyoshangaza jibu la Mzee Wasira lilibeba sura mbili. akiwananga Wazee waliofanya kazi na Nyerere.

Wazee hao ni Dr Salim Ahmed Salim aliyeanza utumishi chini ya Mwl Nyerere akiwa na umri wa miaka 22.
Dr Salim amekuwa balozi katika nchi mbali mbali ikiwemo umoja wa mataifa (UN).

Akiwa UN Dr Salim alifanya mengi ikiwemo kusimamia China kurudishwa katika kiti UN chini ya maelekezo ya Mwalim. Dr Salim alitunukiwa heshima ya juu na nchi ya China kwa mchango wake kwa nchi hiyo

Dr Salim akiwa UN alisimamishwa kugombea Ukatibu mkuu hadi pale nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zilipompiga zengwe kwa kura ya Veto kwasababu tu za kisiasa na si uwezo wake.

Mwl alimrejesha Dr Salim na kumpa nafasi za ndani ya nchi kama Waziri wa Ulinzi na kisha Waziri Mkuu.
Mwl alimteua Dr Salim kuwa Waziri wa mambo ya nje ikiwa ni njia ya kumtambulisha Afrika.

Mwl akampigia chapuo kuwa katibu kuu wa OAU wadhifa alioutumikia kwa miongo kadhaa
Akiwa OAU Dr Salim alishiriki sana katika kutatua migogoro mingi ya Afrika ukiwemo wa Eritrea na Ethiopia.

Inatosha kusema Dr Salim ana uzoefu mkubwa wa masuala ya nchi , Afrika na Dunia.

Mzee Warioba:
Huyu ni miongoni mwa vijana wasomi wa kwanza wakati wa Mwlimu. Joseph aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Sheria, Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais wa JMT.

Moja ya sifa za Mzee Warioba ni ushiriki wake katika serikali ya Mwl na Mzee Mwinyi na utatuzi wa migogoro ikiwemo ule wa Zanzibar. Mzee Warioba ana heshima ya pekee kwa uwezo wake wa kuchambua, kujenga na kutetea hoja.

Mzee Joseph Butiku:
Huyu alikuwa katiba wa Rais Nyerere. Ni mmoja wa watu wanaoijua serikali ya Tanzania kuanzia zama za Tanganyika.
Mzee Butiku ni mtu pekee aliye hai aliyebeba siri nyingi za Mwalimu Nyerere, Serikali na CCM.

Mzee Butiku kama alivyo Mzee Warioba, ni miongoni wa wanaoitwa ''independent minds''

Butiku, Salim na Warioba walichaguliwa katika tume ya katiba mpya inayojulikana kama Tume ya Warioba.
Pamoja na mapungufu ya tume, Wananchi waliikubali tume wakijua kuna watu wazima 'adults in the room' . Wananchi waliamini Tume ya Warioba hata kama ilijaa wanazi , wapenzi au washabiki wa vyama , uwepo wa Wazee hawa watatu haukutiliwa shaka hata kidogo.

Wazee hao walifanya kazi ya kutukuka kwa kusikiliza, kufafanua na kuanisha nini wananchi wanataka.

Hawa ni 'Vijana' wa Mwalimu Nyerere hakuna anayetegemea wangefanya uhayawani hasa katika suala la nchi yaani Muungano. Ni Wazee wanaojua matatizo ya nchi za dunia hawapo tayari kuona nchi inatumbukia katika matatizo. Ni wazee walioweka masilahi ya nchi mbele kuliko matumbo yao.

Dr Salim, Mzee Butiku na Mzee Warioba ni wastaafu na hawakuwa na interest nyingine zaidi ya interest ya nchi.

Tumeeleza Wasifu wa wazee hao makusudi kabisa kwasababu ukitazana video hapao juu, katika dakika ya 15:20 na kuendelea, Mzee Wasira kwa makusudi kabisa aliamua kuwadhalilisha akina Butiku , Salim na Warioba mbele ya Watoto. Kauli za Wasira zimesikitisha, hakupaswa kuwananga na kuwadhalilisha wazee kiasi hicho!

Wasira kasema nini? Itaendelea
 
Mzee Wasira aidhalilisha Tume ya kukusanya maoni ya Jaji Warioba mbele ya watoto wa UVCCM

Katika video ya bandiko#27 Mzee Wasira alianza kuongea
Dakika 15.20 anaombwa kutoa ufafanuzi kwanini Serikali 2 na si vinginevyo

Dakika 17: 40 Wasira anasema katika Bunge la Katiba wapo waliotaka Serikali(S), S2 ,S3 na mkataba.
Anasema haelewi mkataba ni wa nin.

Dakika 18:17 Mzee Wasira anasema waliotaka mfumo wa Serikali 3 au mkataba walilenga Kuuvunja Muungano..
Hoja:
Kwa maneno mengi ile Tume ya Warioba iliyokuwa na Wajumbe wazito akina Jaji Warioba, Salim Ahmed Salim, na Joseph Butiku tuliwaeleza hapo juu kwa sifa zao eti eti walitaka kuvunja Muungano.
Mzee Wasira anaituhumu Tume ya kukusanya maoni ya Mzee Warioba kwa kutaka kuvunja Muungano.
Hakuna maeno mengine mbadala bali ni 'tusi' kwa wazee na vijana watiifu wa Mwalimu Nyerere ambao jamii ya Watanzania inawaheshimu kwa maono, nidhamu na utumishi wao.

Mzee Wasira ana haki ya kuwa na msimamo wake wa Serikali 2, ana haki ya kuutetea msimamo huo.
Hata hivyo Wasira hana haki ya kutoa tuhuma zisizo na uthibitisho. Kutuhumu kwamba Tume ya Jaji Warioba ililenga kuvunja Muungano bila ushahidi ni uzushi na majungu. Ikiwa ana ushahidi Mzee Wasira alipaswa kuuweka wazi, hakuweka! Wasira hakuwatendea wajumbe wa tuma na hasa Wazee wenzake haki.
Salim Ahmed, Butiku na Warioba ni wastaafu wa Umma, Waisira anataka umma uamini walikuwa na agenda nyuma ya Tume. Ikiwa anaamini hivyo Wasira anapaswa kutoa ushahidi wa tuhuma zake.

Dakika 18: 44 Wasira adai utajiri wa Tanganyika wa madini utavunja Muungano

Inaendelea
 


Mh Wasira alivyowabagaza akina Jaji Warioba na Wenzake mbele ya watoto wa UVCCM


Dakika 18: 44 Wasira anasema Serikali 3 zitaifanya Tanganyika iwe na nguvu za kiuchumi kuliko Zanzibar au Serikali kuu. akaendelea kusema Tanganyika ina Wanajeshi wengi na itakuwa na nguvu za kijeshi.
Mzee Wasira akatoa mfano wa iliyokuwa Soviet Union akisema Yetsin Boris aliita Wanajeshi kutoka majimbo yaliyokuwa Urusi ya zamani warejee Russia. Mzee Wasira akasema ndivyo itakavyokuwa katika Serikali 3 kwasababu Rais wa Tanganyika atakuwa na Jeshi na Rais wa Zanzibar atakuwa na Jeshi na kila mmoja anaweza kuita Wanajeshi wake na kumwacha Rais wa Muungano bila Jeshi.

Hoja
Kwa Taarifa ni kweli Tanganyika ina nguvu kubwa sana za kiuchumi kuliko Zanzibar.
Ina rasilimali yakiwemo madini n.k. Rasilimali za Tanganyika zimegeuzwa za Muungano na watu kama Wasira wanadhani hilo linaficha hoja za Watanganyika.
Mzee Wasira aelewe Watanganyika wanachosema ni kwamba Wazanzibar wasidhani rasilimali za Muungano wana shea au wana haki nazo. Hawana kwasababu hawachangii chochote. Hivyo wanachipewa ni hisani tu si haki.
Kutumia rasilimali nyingi za Tanganyika kwa eneo lisilo na manufaa si busara.

Kwanini tunasema ni 'eneo lisilo na maana' ? Ni kwasababu rasilimali fedha zinatumika kuwapendeza Wazanzibar kwa matrilioni bila Zanzibar kuwa na mchango wowote kwa ustawi wa Tanganyika.Kwanini tuwekeze eneo lisilo na 'return au dividend' badala ya kuwekeza maeneo machanga yenye tija kama Songwe, Geita, Simiyu n.k.

Kwanini rasilimali kama madini alizosema Mzee Warioba zitumike kwa Muungano na za Zanzibar ziwe zao.
Mfano ni suala la mafuta na gesi waliyoondoa!

Pili, Mzee Wasira ima hajui au kwa makusudi anapotosha. Kuvunjika kwa iliyokuwa USSR kulikuwa na mkono wa CIA na mageuzi ya Perostrika ya Gobachev yalichagiza zaidi. ZIilizokuwa ''states' zilianza kujitoa Russia ikawa anguko la USSR. Mzee Wasira anapaswa kulielewa hili

Pili, Tume ya Jaji Warioba ilipendekeza uwepo wa Serikali ya Muungano ukiyaacha mambo makuu chini ya Rais wa Muungano. Mambo hayo ni Ulinzi na Usalama(Jeshi), Mambo ya ndani , Mambo ya nje, Usajili wa vyama, Fedha n.k. Kwa mantiki kwamba kiongozi wa Tanganyika hana jeshi wala kiongozi wa Zanzibar hana jeshi.
Kusema kiongozi wa Tanganyika au Zanzibar wataita wanajeshi makwao ni upotishaji na uzushi usio na maana

Nchi kama USA, Canada, India , Brazil, Australia , Nigeria , zinatumia mfumo wa shirikisho na hakuna jimbo lenye askari wake kama anavyopotosha Mzee Wasira.

Kuangalia eneo la USSR kwa kupotosha kunaeleza bila shaka Mzee Wasira hakuwa na jibu japo la kubabaisha, akaona ni Vijana wadogo anaweza kuwadanganya bila kujua ataonekana duniani na kuwa kicheko cha siku.

Badala ya kujenga hoja kwanini S2, Mzee Wasira anawatia hofu Vijana! Hofu isiyokuwa na msingi wala mantiki.

Hofu aliyolenga kwa watoto UVCCM ni sawa na ile aliyotumia kuibagaza Tume ya Warioba mbele ya watoto hao.
Ni kwanini Mzee Wasira anaingia katika siasa za chini kiwango hiki!


Wasira apotosha kuhusu kuundwa kwa JWTZ

Inaendelea
 
Mzee Wasira na JWTZ !

1. Dakika 20:16 Mzee Wasira amesisitiza '' waliotaka Tanganyika iwepo shabaha yao ni kuvunja Muungano.'
Wasira anasema Muungano utavunjika kwasababu Tanganyika ina madini na inatengeneza sehemu kubwa ya Jeshi

2. Dakika 21:36 Wasira anaeleza maasi ya Jeshi ya 1964 na kusema Nyerere alivunja Tanganyika Riffles na kuunda JWTZ kutoka Vijana wa TANU na ASP Youth League

3.Dakika 24:06 anasema Muungano wa Serikali Mbili una faida kwasababu Zanzibar siyo Mkoa

4. Dakika 26: 20 Mzee Wasira anasema Tanganyika haihitaji upendeleo kama Zanzibar , ni kubwa haiwezi kumezwa4.

5. Dakika 27;12 Wasira anasema Mapato ya nchi Mbili yanaedesha Muungano

Hoja:
Tuzipite hoja za Mzee Wasira moja baada ya nyingine kuona ukweli au upotoshaji wake

1. Si kweli kwamba waliotaka Serikali 3 walilenga kuvunja Muungano. Maoni ya Watanzania ndio yalikuwa kioo cha Tume ya Warioba. Kusema Watanzania walitaka kuvunja Muungano si kweli, ni upotoshaji na ukosefu wa hoja.
Haieleweki uwepo wa madini unawezaje kuvunja Muungano. Hadi sasa madini ya Tanganyika ni ya Muungano sijui ni kwanini iwe madini na si kodi au Utalii. Ni kweli sehemu kubwa ya Jeshi ni la Tanganyika lakini pia Mzee wetu auone ukubwa wa Tanganyika na wingi wa mipaka yake. Jeshi haliwajawahi kuwa tatizo la Muungano kama anavyotaka Umma uelewe au alivyodhamiria kubabaisha watoto wa UVCCM

2. Ni kweli kulikuwa na maasi ya Jeshi ya 1964 kama anavyosema Wasira na ni kweli kulikuwa na na Jeshi lililojulikana kama Tanganyika Riffles. Kilichotokea ni kukidhi matakwa ya Wanajeshi waliotaka '' Africanization' ili nao wapate vyeo na kuongoza Jeshi na si wakoloni. Baada ya maasi Mwl alibadili jina na kuita TPDF ili kuleta sura ya Uzalendo wanajeshi wakiwa wale wale. Kwamba walitoka TANU na ASP ni uzushi na upotoshaji wa Mzee Wasira.

3. Kwa mtazamo wake Muungano wa S2 una faida kwasababu Zanzibar si Mkoa. Mzee Wasira atambue kwamba Zanzibar anayosema si mkoa ni Mkoa uliopewa upendeleo maalumu. Zanzibar haina utambulisho kimataifa kama ilivyo Songwe au Simiyu.

4. Mzee Wasira anasema Tanganyika haihitaji upendeleo ndani ya Muungano. Wasira anakubaliana na wengi kwamba Zanzibar inapewa upendeleo. Hata hivyo, Wazanzibar hawakubaliani na Wasira, wanasema zilizoungana ni nchi mbili huru na sawa. Ikiwa ni hivyo, kusema wanahitaji upendeleo ni kuwatukana.

Mzee Wasira haelewi hoja za Watanganyika ya kutotaka upendeleo wala kuidhulumu Zanzibar.

Watanganyika wanasema ndani ya Muungano Zanzibar imekuwa mzigo, tofauti na mkoa wa Songwe au Kiwira tunakoweza kuona mchango wao. Zanzibar haiwajibiki kwa Taasisi za Muungano lakini inapelekewa sehemu kubwa ya mapato . Mfano, Rais SSH aliamua Zanzibar ipewe 9% ya Bajeti ya Tanganyika inayoitwa ya Muungano.

Madeni ya Zanzibar kama umeme yakabebwa na Tanganyika. Mikopo ya Zanzibar ikalipwa na Tanganyika

5. Mzee Wasira anasema mapato ya nchi mbili yanachangia Muungano.
Kwanza, Mzee haelewi Muungano siyo Nchi iliyoungana na Zanzibar bali kuna nchi ya Tanganyika
Mzee anaposema kuna nchi ya Tanzania na Zanzibar inatia shaka hasa tukizingatia umri
Kusema nchi mbili ni kutoelewa au upotoshaji tu.

Pili, Mzee Wasira haelewi Zanzibar haichangii muungano kwa mujibu wa Gavana wa BoT marhumu Ndulu
Tatu, hata hicho kidogo inachopata hakiingii Muungano, tuna mifano ya kutosha
Nne, Bajeti ya Ulinzi ni sawa na ya Zanzibar, na makusanyo yao ni takribani bilioni 60.
Bila kuondoa gharama za SMZ kiasi hicho hakihudumia Wizara ya Ulinzi kwa mwezi, wana nini cha kuchangia?

Mzee Wasira hana habari Watanganyika wanataka Nchi ya Tanganyika wawe na uwezo wa kuamua mambo yao bila kuingiliwa . Mfano, Wabunge wa Zanzibar wanafanya nini Dodoma kwa miezi na miezi?
Kwanini wawe na kura kwa mambo yasiyo wahusu.

Mzee Wasira aelewe Watanganyika hawataki kuvaa koti la Muungano wala kuwadhulumu Wazanzibar.

Muundo wa sasa unawafanya Wazanzibar waamini kuna mambo ya Muungano yasiyopaswa kuwa ya Muungano.
Ili kuyaondoa nje ya Muungano Tanganyika yenye uongozi wake itakayosimamia masilahi yake lazima iwepo.

Mambo yaliyoingizwa Muungano kinyemela na yasiyo ya Muungano yaondolewe ili kuwatendea haki Wazanzibar.

Tuhitimishe video hapo juu kwakusema kwamba, Mzee alitambua anaongea na vilaza na alitumiamwanya kudanganya na kupotosha k uhusu suala la Muungano ambalo Mze hana hoja hata za kubahatisha.

Mzee hawezi kueleza Muungano kwanini upo, una faida na unaweza kulindwa vipi.

Unapokuwa na Wazee kama Wasira, siku watakapoondoka hakutakuwa na replacement yake, hakuna anayeweza kubeba upotofu na ubabaishaji kama wake, mwisho wa siku vijana wa kizazi hawatakuwa na majibu sahihi na Muungano utafikia hatma kama glass iliyodondoka mkononi.


Bandiko lijalo :
Uchechefu, udwanzi na upuuzi wa Mbunge kutoka Konde Zanzibar pale Dodoma (Paasport)
 
Duh Nguruvi3, umenikumbusha zama zile JF ikiwa JF kabla ya kuvamiwa na chawa na vidudu. Kwa hizi nondo, hongera sana! Nazifuatilia kwa karibu sana na nasubiri kwa hamu bandiko lako litakalofuatia.
 
Duh Nguruvi3, umenikumbusha zama zile JF ikiwa JF kabla ya kuvamiwa na chawa na vidudu. Kwa hizi nondo, hongera sana! Nazifuatilia kwa karibu sana na nasubiri kwa hamu bandiko lako litakalofuatia.
Mkubwa nashukuru sana kwa endorsement. Tutajitahidi kuweka kidogo tulicho nacho kadri ya mjaaliwa

Kama ulivyosema, chawa, wadudu kunguni n.k. wamevamia jamvi lililokuwa kisima cha maarifa, wazee wakapotea!!
Tuna wa miss sana ninyi mlioyaona mengine kwa macho yenu na mliosaidia sana kunyoosha hoja hapa JF.

Ahsante mkuu
 
WIKI ILIYOJAA MAUZA UZA YA MUUNGANO

MBUNGE ATAKA WATANGANYIKA WAENDE ZANZIBAR NA PASSPORT

Mh TUNDU LISSU ATIBUA NYONGO , AJADILIWA NA SI KUJADILI HOJA ALIYO TOA


View: https://www.youtube.com/watch?v=UBzxqVKvpUs

Link hapo juu inamuonyesha Mh Mohamed Issa Mbunge wa Chama cha ACT Wazalendo akizungumzia suala lililoibua mjadala mzito katika mitandao ya jamii na duru za siasa nchini.

Mohamed Issa ni Mbunge wa chama cha ACT Wazalendo aliyeshinda kwa kura 2,391 jimbo la wapiga kura 3,338.

Akichangia wizara ya Muungano na mazingira , Mohamed anasema Watanganyika kuingie Zanzibar kwa passport kwasababu wamejaa hakuna sehemu ya kuishi, ardhi ya Zanzibar lazima ilindwe na shughuli za Utalii na Hoteli zimechukuliwa na 'Watanganyika

Mohamed ameibua hisia lakini alichokisema si jambo geni kwa maana mbili.

Kwanza, utaratibu wa kuingia visiwani kwa passport ulikuwepo hadi nyakati za Rais Mwinyi.
Katikakati ya fukuto la G55 Wabunge wa Tanganyika walitaka Wazanzibar waje kwa passport.

Baraza la Mpainduzi liliondoa sharti la Passport haraka kwa ukweli, ni Wazanzibar wanaohitaji kuingia Tanganyika

Pili, Mohamed Issa amewakilisha mawazo ya chama ACT Wazalendo chenye sera ya kuvunja Muungano.
Licha ya dharau dhidi ya Watanganyika, ACT Wazalendo wapo kimyaa! ishara ya kubariki kauli ya Mohamed Issa wa Jimbo la Konde

Tatu, wanaharakati kama mwanasheria Fatma Karume ambaye ni 'vocal' katika masuala ya Muungano alikaa kimya kama ilivyo kwa wana CCM wa Zanzibar ikiashiria Wazanzibar kukubali kauli ya Mbunge wa Konde .

Rejea bandiko#33 kuna link ya kongamano la Vijana wa UVCCM kuhusu Muungano.
Dakika 12:15 Prof Makame wa Zanzibar anabainisha Sensa ya Taifa ya 2020 Wazanzibar 1.3 Milioni wanaishi Tanganyika. Wazanzibar wanapata huduma zote kama Mtanzania mwingine popote pale iwe shuleni au Hospitali, chuoni au sokoni , mtaani n.k. kwa gharama za kodi za Waanganyika bila kubaguliwa

Mbunge Mohamed anaposema 'Watanganyika wamejaa Zanzibar, na wanafanya kazi za utalii na hoteli na hivyo wadhibitiwe kwa passport'' ni tusi la kukera na kuudhi kwa Watanganyika.

Wazanzibar 1.3Milioni waliopo Tanganyika wanapata fursa na haki zote, hakuna anayelalamikia ujazo wao

Mbunge Issa na ACT na Wazanzibar, mbegu waliyopanda ya UBAGUZI ni mbaya kwa Wazanzibar .
Wazanzibar wanaoishi Tanganyika wanaangaliwa kwa jicho lile lie la ubaguzi

Alichozungumza Mohamed hakihitaji elimu ya darsa lolote wala busara ya busati bali upuuzi tu

Akiwa Dodoma, Mohamed Issa analipwa mafao na mshahara wake na kodi za Watanganyika.
Maji na umeme na mkewe anaotumia Dodoma na Zanzibar zinalipwa na kodi za Watanganyika.

Idadi ya waliomchagua kuwa Mbunge ni ndogo kuliko ' Ndaki' au Faculty ya Chuo kimoja cha Tanganyika.
Pesa za mfuko wa jimbo la Konde anazopata ni kodi za Watanganyika

Mbunge Mohamed ni mzigo kwa Tanganyika, kusema wanajaza Zanzibar ni ukosefu wa Elimu na maarifa.

Mbunge Mohamed Issa anaueleza kero ya Muungano! . Unapokuwa na Mbunge anayechaguliwa na watu sawa na Faculty moja ya UDSM akiongoza watu wachache kuliko kiongozi wa DARUSO pale Chuo kikuu, uwezekano wa kumpata Mbunge mwenye busara na akili ni mdogo sana

Hoja ya Mohamed Issa wa ACT Wazalendo, Wamasai kutandikwa viboko na Watanganyika kuzuiliwa biashara za ndizi, ubaguzi wa Wazanzibar umetibua nyongo za Watanganyika.

Kama Mohamed Issa alitumwa ili kutibua Watanganyika, amefanikiwa, asubiri 'reactions'

Watanganyika hawana shida yoyote kuingia Zanzibar na passport, wengi huenda kujivinjari na si kuishi.
Ni vema na haki kurudisha utaratibu wa passport na wao waje na passport huku bara.

Jambo la kustaabisha, UBAGUZI kama wa Mohamed unanyamaziwa na Rais SSH na Rais Mwinyi.
Picha inayopatikana katika jamii ni kwamba 'huenda' nao wanaunga mkono hoja za ACT na Mohamed

Ukimya wa viongozi kutokemea hoja ya Mohamed , yale ya ndizi na Wamasai kufurushwa kumezaa ' reaction'. Watanganyika wanahisi ukiwa na upwekei na wanaliona ombwe! wanadai nchi yao!

Bandiko lijalo tutaangalia kauli ya Tundu Lissu na hamaki itokanayo
 
TUNDU LISSU ASHAMBULIWA BINAFSI NA SI HOJA ALIYO TOA

Tumejadili fyongo ya Mbunge wa ACT Wazalendo kuhusu Watanganyika kuingia na passport Zanzibar

Kwa namna ya aibu waziri Wizara ya muungano aliijibu kwa utani tu alisema '' Ndg yetu Mohamed anaturudisha nyuma...' hakumkemea Mohamed Issa (MB) wala hatukusikia kelele za meza. Ilikuwa ''business as usual''

Ghafla tukaona mawaziri wakilaani kauli za Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bw Tundu Lissu kwa ghadhabu kali

Ilikuwa kana kwamba Mh Lissu kafumua misumari inayoshikilia anga la Tanzania, na huenda likaanguka.
Waziri habari alisema Taifa lisigawanywe kwa misingi ya wapi kiongozi anatoka, ana jinsia gani , dini n.k.

Wakati Mh Waziri akimlaani Tundu Lissu kwa ''kuligawa'' Taifa, ndani ya wiki hiyo tulisikia upuuzi wa Pasport.
Tulisikia mgogoro wa ndizi Zanzibar, Rais wa SMZ na marufuku Mtanganyika kupewa ardhi Zanzibar, Wanamasai kule kufurushwa n.k. Yote hayakuonekana tatizo kwasababu yalifanywa na Wazanzibar

Wazanzibar wamepewa haki ya kuhoji , kuutukana na kuudhihaki Muungano bila kukemewa.
Kwa mfano, Rais Mwinyi anapowapiga marufuku Watanganyika kumiliki ardhi, na Mbunge kutoka Zanzibar anapodai Passport katika nchi moja kuna ubaguzi gani uliozidi huo? Tulimsikia nani akikemea?

Mh Mbowe aliposema suala la DP World linajenga hisia mbaya na Rais aliangalie, alishambuliwa Bungeni.
Alichokisema Mh Tundu Lissu ni kile alicho onya Mbowe na kukemewa badala ya kusikilizwa

Maneno ya TL si mageni lakini utamaduni wa Wazanzibar kupewa haki za kusema lolote unayafanya maneno kuwa ni maneno makali. Ukweli. TL ameazima maneno kutoka kwa Wazanzibar.

Walioliamsha jina la Tanganyika ni Wazanzibar tena wakiwatukana Watanganyika.

Wanaotumia neno Uzanzibar ni Wazanzibar, Katiba ya Zanzibar inawatambua kwa Uzanzibar wao.
Wenye vitambulisho vya Uzanzibar ni Wazanzibar na ndivyo vinatumika kuwabagua Watanganyika.

Hakuna Tanzania bila Zanzibar ! kuitenga Zanzibar nje ya Tanzania kitakachobaki ni Tanganyika.

Rais SSH ni Mzanzibar akitambuliwa na katiba na kitambulisho cha Uzanzibar ukaazi.
Kitambulisho cha ukaazi kilimpa nafasi ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa JMT.
.
Kumtambua kwa Uzanzibar wake linakuwaje tatizo? Kwanini maneno ya Tundu yaligawe Taifa na si kitambulisho cha Uzanzibar ukaazi anachomiliki Rais SSH?

TL allisema kuwafurusha Wamasai Ngongoro kumefanywa na Rais ambaye ni Mzanzibar huku Tanganyika.
Kwanza, Uzanzibar wa Rais SSH upo katika katiba ya Zanzibar, TL amekosea nini?

Pili Rais SSH alikuwa makamu wa Rais kwasababu alitokea Zanzibar. KaTiba inasema hivyo!
Kuingia kwake madarakani ni zao la Uzanzibar kwa mujibu wa Kaiba. Kwahiyo kuwa Mzanzibar si kosa.

Hoja ya TL kuhusu bandari n.k. ni kweli na hapo ndipo Mbowe apongezwe kwa kuliona tatizo mapema .

TL alichokisema ndicho kinasemwa na Watanganyika tena wakiwemo wa CCM nyuma ya pazia.
Kwamba kuuza kwa bandari kulihusisha za Tanganyika tu, kwanini haikuwa Zanzibar?

Suala la Bandari lilishadidiwa na akina Jusa, Othaman (VP) na Babu Duni.
Wakati wa sakata la DP walisema '' ....Watanganyika wanalalamika kwasababu Rais ni Mzanzibar na hilo ni la kwao wahangaike nalo wenyewe''.

Utetezi kwa Rais SSH kwa Uzanzibar wake na si hoja, hawakujua mbegu waliyopanda.
Wazanzibar hawakumbuki usemi kwamba ''Mwiba hutoka ulipoingilia''.

Utetezi wa Rais SSH ulijengwa na Wazanzibar kwa Uzanzibar wa SSH na si Urais. Bandari za Tanganyika ziliajwa na Wazanzibar na si za Tanzania. Leo Rais SSH anapohojiwa kuhusu bandari na Ngororo kwa Uzanzibar wake na mali za Tanganyika , kimebadilika nini?

Kwanini utetezi kutoka kwa Wazanzibar haukuwa tatizo, leo ni tatizo TL akisema waliyosema akina Duni, Jusa na Othaman! TL alipaswa ku 'acknowledge'' kutumia maneno ya akina Jussa, OMO na Duni.

Wakati akina Jussa, OMO na Duni wanaongea hatukusikia wakikemewa ! TL kakosea kipi kigeni?

Inaendelea...
View: https://www.youtube.com/watch?v=ZdRPMylxhsI
 
BAADA YA TUNDU LISSU ''KUTIBUA VUMBI'' MENGI YAANZA KUJITOKEZA

Katika hoja alizotoa Mh Tundu Lissu (TL) ni kuhusu Idadi ya Wabunge wa Zanzibar

TL anasema mkoa wa Dodoma ina Wabunge 11 ukilinganisha na Wabunge zaidi ya 80 kutoka Zanzibar
TL anatoa takwimu za wapiga kura wa mkoa wa Dodoma ambao ni takribani 1.3 Milioni, Zanzibar ni 500,000

Hoja ya Mh TL inachagizwa na ukweli wa Jimbo la Temeke lenye wapigakura 400,000 na Mbunge mmoja, wakati Jimbo la Konde Zanzibar lina wapiga kura 3,338 sawa na Wananchi wa mtaa mmoja wa Jimbo la Temeke.

Kwa taarifa , jimbo la Konde ndilo anatoka Mzanzibar Mohamed Issa anayeshauri Watanganyika waingie kwa pasport

Alichoonge TL ni ukweli unaoudhi wahafidhina wa CCM kwasababu ni ukweli mtupu ''naked truth''

Mkoa wa Dar es Salaam, kitovu cha uchumi una watu milioni 6 na Wabunge 10 kwa wastani wa watu 600,000 kwa mbunge idadi kubwa kuliko jumla ya wapiga kura wote wa Nchi ya Zanzibar 2020.

Athari kubwa za Wabunge wa Zanzibar ni uwezo wa kuzuia au kuamua mambo ya Tanganyika.

Mathalan, ikiwa kuna kura katika Wizara ya Elimu, Mifugo, Utalii, Viwanda, Maliasili , Nishati n.k. ambazo si za Muungano, Wabunge wa Zanzibar takribani 80 wana nguvu ya kubadili maamuzi yanayohusu Tanganyika kwa kura.

Kutokana na tatizo hilo kuna mambo yanayoweza kufanyiwa marekebisho haraka na Wazanzibar kama hawana UNAFIKI inabidi wayaafiki kwa muda huu tukisubiri katiba mpya

1. Wabunge wa Zanzibar wajadili mambo ya muungano kisha waondoke ili kupunguza gharama kwa mlipa kodi wa Tanganyika. Wabunge hao hawahitajiki katika maamuzi yasiyohusu Zanzibar na hivyo wakae pembeni.

Uwepo wa Wabunge wa Zanzibar kujadili ya Tanganyika ni ulafi na uroho wa pesa. Ni unyemela wanaoukataa lakini wanautaka kwasababu ya matumbo tu. Watanganyika wanasema hawahiaji mchango wao! wapunguze gharama

2. SMZ ilipie Wabunge wake na idadi ya 80 inawezakena kwa mambo ya Muungano kisha wanaondoka Dodoma .

Kwa hoja hii, alichokisema TL ni sahihi na ukweli mtupu. Mtu aliyechaguliwa na watu 3,000 kufanya maamuzi kwa kura sawa na aliyechaguliwa na watu 600,000 si sawa , ni upendeleo usio na maana wala mantiki.

Mkoa wa Mwanza una idadi kubwa ya watu kuliko Zanzibar, unachangia pato la Taifa kwa wingi na una rasilimali nyingi. Mkoa huo unahitaji Wabunge wengi na si Zanzibar wanaochaguliwa na watu 3,000

Hoja ya TL imechokoza fikra kwa wanaofikiri. Jumatatu saa 2 usiku kulikuwa na mjadala unaoendeshwa na Mwanaharakati Mmoja (space). Watanganyika walionyesha kuchukizwa na mfumo wa Muungano wakibeba na kuugharamia peke yao, Wazanzibar wakisubiri kugawiwa au Formula ya kupewa na si kuwajibika.

Mchangiaji mmoja alibomoa hoja ya Wazanzibar kuhusu ardhi, alisema '' ikiwa ardhi ya Zanzibar ni ndogo na tumeunga hakuna sababu za Muungano''.
Aliendelea kusema Muungano una maana moja kubwa ya kile alichokisema tunaungana ''whaT do you have to offer''

Hoja ya mchangiaji huyo ilikuwa na mantiki sana kwamba ikiwa Zanzibar hawawataki WaTanganyika kwa udogo wa ardhi yao tunakuwa na muungano wa kitu gani?

Yaani Zanzibar wana offer nini ambacho Tanganyika itavutika kusema naam! Tuungane.
Ikiwa hawataki ardhi, basi tunaweza kukutana EAC hatuhitaji Muungano.

Muungano ni kwa ''mutual benefit'' kila upande unafaike. Kwa sasa Watanganyika hawaoni nini wananufaika zaidi ya kupoteza.

Wimbi la kuidai Tanganyika linavuma na kuzizima, ikiwa wapo wanaoutaka muungano huu uendelee basi wafuate ushauri wa Prof Kabudi, Watanganyika wapewe Tanganyika yao kabla ya kuidai kwasababu wana ya moyoni.

Hali ikiachwa kama ilivyo, udanganyifu unafika kikomo na Muungano utavunjika kwa chuki, Zanzibar watataabika! Waswahili husema udongo uwahi ungali maji.
 
ALIYEDAI PASSPORT, AUKANA UTANZANIA
SLOGAN YA ' KILA MZANZIBAR NI MTANZANIA, LAKINI SI KILA MTANZANIA NI MZANZIBAR

Mbunge wa Zanzibar Bw Mohamed Issa aliyetaka wa Bara waingie Zanzibar kwa passport amezua jingine.
Ndani ya Bunge la JMT Issa alikana yeye si Mtanzania ni Mzanzibar

Kauli ya Issa ilileta mshtuko ndani ya Bunge lakini kwavile ni ACT Wazalendo yenye ubia na CCM, suala lilionekana jepesi likiwekewa mwongozo wa Spika kisha kikao kuendelea kama kawaida.
Laiti kauli hiyo ingetolewa na Mtanganyika hasa wa upinzani kuta za Ukumbi wa Bunge zingevunjika kwa laana

Kudai passport ni ubaguzi na ushenzi (kukosa ustaarabu) kuliko kaul iliyotolewa kwa mtazamo wa Muungano.

Spika na Bunge akaiacha! . Kauli ya Kuukana Utanzania ndani ya Bunge ni ya kibaguzi Spika, Waziri Mkuu na Bunge wakakakaa kimya! Hatukuwasikia Wabunge waliofura wakati wa kauli za Mbowe na Lissu, Wabunge waliufyata.

Ni kawaida, Wazanzibar wana haki ya kusema lolote bila kuchukuliwa hatua, ni '' raia daraja la I ''

Kuukana Utanzania ndani ya Bunge ni tusi. Issa na Wabunge wa Zanzibar wamo ndani ya Bunge wakijadili yasiyowahusu kwa 90 %. Yupo mwenyekiti wa Bunge Mzanzibar anayesimamia mijadala ya mambo ya Tanganyika. Wazanzibar wanalipwa stahiki zao na pesa za majimbo kutoka hazina ya Tanganyika '' wasiyoitambua ''

Mbunge Issa wa Zanzibar anapata wapi uthubutu na jeuri ya kusema anayosema?
Je ana baraka za ACT Wazalendo ambao wamekaa kimya na tukijua sera zao ni kuvunja Muungano!

Yuko wapi Spika wa Bunge la JMT? Yuko wapi Waziri Mkuu wa JMT? viongozi wa JMT na SMZ wako wapi?

Muungano unapita nyakati ngumu, kauli za maudhia na kadhia za Wazanzibar zinachochea hasira na hisia.
Hisia zinazojengeka ni kwamba Wazanzibar ni raia daraja la I.

Katika muendelezo wa hayo, Makamu wa pili wa Rais na mmoja wa Waziri katika ofisi yake kutoka SMZ anayeshughulikia Muungano wamenukuliwa katika Televisheni wakisema '' Kila Mzanzibar ni Mtanzania lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar'' ., Ni kauli inayotumiwa na CCM Zanzibar kutetea na hoja za kibaguzi.

Kwa mfano wakiulizwa kwanini ardhi , ajira na yasiyo ya Muungano Wazanzibar wanashiriki, jibu lao ni hilo

Bungeni, wanapojadili ya Tanganyika ni katika '' uhalali'' ni Watanzania, lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar.

Kwa kauli ya Issa kuna kila sababu za kuamini ni masilahi tu , Wazanzibar hawana uchungu wala kujivunia Utanzania, kama alivyowahi kusema Jussa kuhusu DP na Bandari au Ali Salehe na Bandari ya Bagamoyo.

Jussa alisema hla bandari ni lao wenyewe akimaanisha Watanganyika ingawa mapato ya bandari yanagawanywa sehemu kwenda Zanzibar

Ali Salehe alisema '' nasikia bandari ya Bagamoyo imefeli, na afadhali ifeli kabisa'' Ali Salehe ni Bunge na pesa za Ubunge na Jimbo lake zinatoka Taganyika. Wote hawana uchungu na Tanganyika licha ya kuwalea

Kauli ya CCM Zanzibar kwamba ' Kila Mzanzibar ni Mtanzania na si kila Mtanzania ni Mzanzibar'' ina ukweli.
Tatizo, katika nchi moja hatuwezi kusema '' Kila Mkigoma ni Mtanzania lakini si kila Mtanzania ni Mkigoma''
Sisi ni Watanzania na Taifa moja na tunaishi popote hatuhitaji passport kama wanavyodai Wazanzibar.

Hatari ya kauli ya '' Kila Mzanzibar ni Mtanzania na si kila Mtanzania ni Mzanzibar' ni ushahidi kwamba kila kilicho cha Tanganyika ni cha wote na cha Zanzibar ni chao.

Watanganyika wanaliona hili kama ''abuse' ya Muungano na linachochea hasira!
Wazanzibar watafakari matumizi ya maneno hayo, kwasababu yanawafanya Watanganyika watafakari '' chetu ni cha wote kwasababu hakina mlezi , chao ni chao'' '
 
ZIPO NYAKATI SAA MBOVU INASEMA UKWELI MARA 2 KWA SIKU
TUNACHOKISEMA KILA SIKU WAZANZIBAR WAMETHIBITISHA


Ni kwa hisani ya gazeti la Mwananchi, shukran

Kuna msemo ''saa mbovu husema ukweli mara 2 kwa siku'' ,
kwa maana pale iliposimama muda ule ukifika itasomeka kweli. Hilo halifanyi saa mbovu iwe nzima

Katika mkutano wa ACT Wazalendo uliofanyika viongozi wawili waandamizi wa chama wameongea.
Kwa minajili ya mjadala tutaongelea kauli za Mwenyekiti wa ACT bw Masoud Othman (OMO)

OMO amenukuliwa '' mbele kuna giza, ni wakati Wazanzibar washikamane kupigania masilahi ya Zanzibar''
Kauli ya OMO haina matatizo, chama chake ni cha Wazanzibar akiwausia wapiganie masilahi ya Zanzibar.

Tatizo ni pale kauli ingetolewa na Mtanganyika! ingaliitwa ya kibaguzi kwasababu inawataja Wazanzibar kama ilivyosemwa kwa Rais SSH ili hali mwenyewe amethibitisha mara nyingi kwamba ni Mzanzibar.
Kuna Mbunge kasema yeye ni Mzanzibar na kuukana Utanzania. Kwanini yote haya hayaonekani!

OMO anaendelea '' Harakati za kupigania Zanzibar kupata mamlaka ni sasa kwasababu mbele kuna giza''
Mwenyekiti OMO anataka mamlaka kamili ambayo ni lugha laini ikimaanisha '' kuvunja Muungano'
Ni mantiki hiyo kwasababu hata katika ndoa za binadamu hakuna mwenye mamlaka kamili hadi ajitoe.
ACT Wazalendo wanaposema mamlaka kamili wana maana moja '' Vunja Muungano''

OMO akasema '' 54% ya mapato ya uchumi wa Zanzibar yanatoka katika vyanzo vya Muungano, akitokea akaja kiongozi mwingine akavichukua Zanzibar haitabaki na kitu kwasababu ni hisani''
OMO anathibitisha wasi wasi kwamba akitokea kiongozi asiye Mzanzibar mapato hayo yanaweza kuchukuliwa.

Pili, OMO anathibitisha kauli zetu za kila siku kwamba Zanzibar inabebwa na Tanganyika kwa jina la Muungano.
Na OMO anasema ukweli kwamba rasilimali za Tanganyika zimepachikwa jina la Muungano

Makamu wa kwanza wa Rais bw OMO anakiri kwamba ushuru wa forodha, Bandari, mafuta na gesi na Uhamiaji ni mambo ya Muungano lakini kwasasa yameondolewa.
Wasi wasi wa OMO, akija kiongozi mwingine (kwa maana asiye Mzanzibar) anaweza kuyarudisha katika Muungano.

Kwa aya hiyo hapo juu OMO na Wazanzibar wajilaumu wenyewe. OMO ni Mwanasheria na anafahamu katiba ya JMT inasema nini kuhusu Mambo ya Muungano na 2/3 ya Wazanzibar Bungeni ina maana gani.

Ni katika wakati akiwa Mwanasheria, OMO kwa chuki na ghadhabu akawaongoza Wazanzibar wayaondoe katika Muungano bila kujadiliana na JMT. Kitendo hicho kimewaudhi Watanganyika kwani ni dharau dhidi ya Katiba ya JMT

Miaka 10 na ushee OMO anabaini kwamba kilichofanyika ni 'cosmetic changes' na kwamba mambo hayo yanaweza kurudishwa bila hata kuijulisha Zanzibar kwaababu yaliondolewa kinyume na sheria kwa kukosa elimu tu.
Katiba ni ''sheria' na huwezi kuondoa au kufuta sheria bila kufuata taratibu zilizoainishwa. OMO kama mwanasheria alishindwaje kuliona hilo akiwa AG! Hili halihitaji elimu ya sheria, pengine ni chuku tu iliwaongoza Wazanzibar

OMO amethibitisha kwamba malalamiko ya Watanganyika kwamba Rais SSH ametoa bandari za Tanganyika kwa DP na kuziacha za Zanzibar ni ya kweli kwasababu Bandari ni suala la Muungano hata OMO amethibitisha.

Siri nyingine aliyoitoa Mh OMO ni kuhusu Uhamiaji. Katika mabandiko hapa JF tulielezamapato ya Uhamiaji Zanzibar yanachukuliwa na SMZ na si JMT ingawa ni jambo la Muungano.

Tulieleza pia kwamba Watumishi na gharama za uendeshaji wa Idara ya Uhamiaji yakiwemo mafunzo, majengo , na mishahara ya Wafanyakazi yanatoka JMT ambayo ni Tanganyika.
Kwa maneno mengine Watumishi wanalipwa na Tanganyika ili wakusanye mapato kwa ajili ya SMZ.
OMO amethibitisha unyonyaji huo unaofanyika mchana kweupe.

Lakini pia kuna swali la kujiuliza, ikiwa Uraia ni wa nchi moja tunawezaje kudhibiti ''Passport' tukiwa na Idara ya Uhamiaji ya JMT na kisha idara ya Uhamiaji Zanzibar?

Kuna tatizo kwasababu kuondoa 'Uhamiaji' kinyemela kutoka mambo ya Muungano ni kuhatarisha usalama wa Taifa.
Haiwezekani kuwa na 'system 2' zinazo control passport moja

Tunakumbuka hatari iliyowahi kutokea kwa mtindo huo wa ''double control' . Kimataifa Tanzania ni mwanachana wa IMO (International Maritime Organization) kupitia Tanzania Maritime Organization( TMO) na ndiyo inalipa ada za Uanachama. Zanzibar wana ZMO (Zanzibar Maritime Organization) ikifanya kazi tofauti na TMO.

ZMO ilisajili meli na kuzipata idhini ya kutumia bendera za Tanzania. Meli hizo zilitumiwa na Iran ikiwa chini ya vikwazo. Tatizo lilipokuwa la Kimataifa, Waziri wa mambo ya nje ndiye alihusika kutatua na ilikuwa issue ya Tanzania si Zanzibar. Wazanzibar walichukua pesa na ''msala' wakawaachia Tanzania a.k.a Tanganyika wahangaike nao

Hili la Uhamiaji kuondolewa na Zanzibar katika mambo ya Muungano kwa siri lina hatari kwa usalama wa Tanzania.
Tunarudia tena katika nchi moja hatuwezi kuwa na mifumo miwili inayo '''Passport control'' na Uhamiaji.

OMO ametoboa siri nyingine ya Uhamiaji iliyochanganya watu na sasa tuna majibu! tutaijadili bandiko lijalo

Itaendelea
 
KUHUSU UHAMIAJI
MAKAMU WA RAIS 'ANENA NENO TUSILOLIJUA''. ATUKUBUSHA URAIA ULIOTOLEWA ZANZIBAR


Makamu wa Rais wa SMZ Bw Othman Masoud (OMO) ambaye ni mwenyekiti wa ACT Wazalendo amenukuliwa na gazeti la Mwananchi (Bandiko#38) akisema akitaja mambo yaliyoondolewa katika Muungano lakini ni kwa ''hisani'.

OMO aliyeshiriki kuyaondoa bila kujali katiba ya JMT ameonyesha wasi wasi ikiwa atatokea ''kiongozi mwingine' na kuyarudisha katika Muungano. Ameyataja kama Ushuru wa Forodha, Mafuta na Gesi , Bandari ,Uhamiaji.

Matatu ya mwanzo yaliondolewa na Zanzibar kwa katiba ya 1984 toleo 2010 lililoitambua Zanzibar kama nchi na kujipa ukuu zaidi ya ile ya JMT. Zanzibar wana '' haki'' watajadiliana na nani ikiwa wao pia ni sehemu ya JMT?
Ombwe la kukosekana kwa Serikali ya Tangayika linaonekana , ni hoja inayofikirisha ikihitaji kufanyiwa kazi.

Kubwa kati ya aliyosema OMO ni Uhamiaji. Watatanganyika isipokuwa SMZ na Wazanzibar hawakujua Uhamiaji imeondolewa kinyemela kutoka Muungano. Kisichojulikana, imeondolewaje kwa utaratibu gani na chini ya Rais gani.

Mwaka jana Rais SSH akifunga mafunzo ya Uhamiaji alisema '' ... Zanzibar ni ndogo tunafahamiana kwahiyo ni vema Watumishi kutoka Bara wakapelekwa Zanzibar na wa Zanzibar wakaletwa Bara, hili ni jambo la Muungano''

Makamu wa Rais Bw OMO anaposema Uhamiaji imeondolewa katika Muunga inalofikirisha.

Je tumwamini Rais SSH au Makamu wa Rais Bw OMO. Ni swali la kijinga lakini kwa wanaofikiri kuna kitu hakipo sawa. Kwa mujibu wa OMO hatujui ni kipi kimeondolewa katika Uhamiaji ?

Lakini pia suala la Uhamiaji linalohusiana na Uraia linaweza kufanywaje nusu nusu.
Ikiwa anachosema OMO ni sahihi kuna jambo halipo sawa, au linafumbiwa macho, au linapewa usaidizi.!

Maswali yanazidi kuongezeka tukikumbuka tangu Uhuru na tangu Muungano uundwe hatujasikia kiongozi mwingine zaidi ya Rais wa JMT akitoa Uraia. Kuna uwezekano zipo taratibu za kukasimu madaraka hayo kisheria, tunachofahamu Uraia haujawahi kutolewa na kiongozi mwingine zaidi ya Rais wa JMT.

Miezi 8 iliyopita Rais wa Zanzibar alitoa hadhi ya Uraia kwa raia wa Kigeni.
Rais wa Zanzibar anachaguliwa na Wazanzibar na ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri la JMT.
Ukiacha mialiko ya shughuli za kawaida za kijamii, kisheria Rais wa Zanzibar hana mamlaka katika JMT.
Rais wa Zanzibar anapotoa Uraia wa Tanzania ni kwa mamlaka kutoka Ibara gani ya Katiba ya JMT!

Lakini pia kwa kufuata katiba ya Zanzibar toleo la 2010 Zanzibar ni nchi. Kuna uwezekano Rais wa Zanzibar alitoa Uraia kwa wageni kuwa ''raia'' wa Zanzibar! Lakini suala la Uraia ni la Muungano tukitumia passport moja ya JMT

Bw OMO anaweza kuwa sahihi kutuambia Uhamiaji imeondolewa katika Muungano, na pengine kupitia kuondolewa huko Rais wa Zanzibar akapewa uwezo wa kutoa Uraia kwa Wageni.
Swali ni moja tu Uraia uliotolewa ni wa Zanzibar au JMT? Ikiwa ni wa JMT, Rais wa SMZ ana mamlaka gani kikatiba?

Kichefu chefu ni pale Raia wa kigeni wanapopewa Uraia Zanz,ibar tukijua Uraia ni suala la Muungano.
Kwa maneno mengine Raia hao wanaweza kuvuka bahari kuja Tanganyika kwa kauli ya '' Kila Mzanzibar ni Mtanzania lakini si Kila Mtanzania ni Mzanzibar'' wakitumia passport ya JMT inayowapa haki ya kila kitu Tanganyika.

Kuingia kwa watu hao bila ''vetting' wakipewa Uraia wa ''Zanzibar' kupitia kitambulisho cha Ukaazi lakini passport ni za Tanzania kuna tatizo kiusalama hasa kwa upande wa Tanganyika

Makamu wa kwanza wa Rais Bw OMO ametufumbua macho! hili la uhamiaji kuondolewa kinyemela lakini gharama za majengo na mishahara zinatoka Tanganyika! na Uraia unakuwa na uatata

Lakini nani atahoji ? Tanganyika ambayo ni 'victim' haina structure! Rasilimali zake hazina msimamizi ni za wote

Tanganyika kulalamika JMT ni sawa na kesi ya Ngedere kula mahindi kesi ikapelekwa kwa Nyani kama Hakimu!
 
Back
Top Bottom