Trueman m
JF-Expert Member
- Nov 26, 2014
- 292
- 299
Hapo kwa akili yako onesha huo ukweli aliosema.N
Fikiri watanzania wengi na watumishi wa umma wengi ndio wana uelewa mdogo wa kupembua mambo. Hapo mnachokifanya ni mashambulizi binafsi kwa mkuu wa mkoa ambayo hayawezi kamwe kubadiri maisha yenu.
Kikokotoo kimepitoshwa bungeni ambao kila mmoja wenu ana mwakilishi wake uwe ulimchagu au hukumchagua. Kuna vyama vya wafanyakazi pia. Mkiitwa kwenye maandamano na CHADEMA kupaza sauti hamjitokezi mnajidai hamtaki kukosana na mwajiri wenu.
Ni lini vyama vya wafanyakazi vimeitisha maandamao au mgomo kupinga kikokotoo? Kama hawakipendi mbona hawakipingi hadharani? Mnategemea mtu kujificha huku jamii forum na kutukana mtu binafsi?
Ni lini watumishi kwa ummoja wenu mmeingia barabarani kupinga uamuzi wa bunge? Kazi kudandia mada. Wengine wanadhani kikokotoo kimepitoshwa juzi. Kweli tangu 2018 leo hii ndo midhipa inawatoka?
Nani umemsikia akigoma kwenda kazini kisa kikokotoo.
Watanzania wasipoambiwa maneno machungu hawaamki. Ni umbea, majingu na takataka zote.
Mtu kusema ukweli ndo tumshambulie. Na baada ya kumshambulia tumepata nini? Lazima tujitambue hasa watumishi.
Hii inaonyesha dhahiri hata watumishi hawajui kikokotoo kimetoka wapi, kimeletwa na nani na wakitaka kiondoke wafanyeje. Hawa wengine tunawaonea tu.
Mshambulizi haya yangetolewa hadhari kwa aliyeleta kikokotoo. Kwa taarifa yako kikokotoo kabla hakijaletwa bungeni, kinaandaliwa na watumishi walioko kwenye ofisi zinazihusika. Lazima watumishi wajue mbaya wao kwanza.
Jamii forum inatakiwa kuwa na watu wajenga hoja na sio personal attack. Kwa hiyo Mtaka akiwa sio mkuu wa mkoa ndo kikokotoo kimeondoka?