Mliokopa salio la kawaida kwenye Airtel mmekutana na hiki kitu kwenye kulipa?

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,824
2,204
Salamu wadau.

Kifupi sio kulipa labda niseme utaratibu wao mpya sio mzuri.

Juzi kwa dharura nimekopa salio la kawaida nimpigie jamaa nikafanikiwa sasa kesho yake nimeenda kwa wakala niweke hela nashangaa ghafla napigwa na kitu kwamba salio lako ulilokopa limekatwa deni lako na hela iliyobaki imepelekwa kwenye salio lako la kawaida.!!

NIKABAKI kushangaa tu nimetoa macho kama nimebanwa kwenye bawabu za mlango wa mbao.Najiuliza huu utaratibu umeanza lini mbona hawasemi kwanini wasitujuze kama wavotumaga sms zao za matangazo?

Halafu kitu kingine mimi nimekopa salio la kawaida inakuwaje nyinyi mnakata kwenye airtel money? Kama umekutana na hii kitu hebu lete mrejesho kama nado jaribu na wewe kidogo halafu uone.
 
Ndo maana nikasema jaribuni
Hakuna ujanja ujanja siku hizi. Mfumo upoo tangu mwaka Jana si Voda Sio Airtel. Hata kama unge tafuta mtu mwingine akurushie Salio. Wanakata deni lao kwanza. Ukijifanya kuweka Hela Airtel money ununue Salio Airtel money,Wanakata deni kwanza halafu ndo unaendelea na mambo Yako.

Ka mfumo kazurii sana. Kanahamasisha kusaka mkwanja
 
So sad, hauna sifa ya kukopesheka benki tena
Usimtishe mwenzako. Mimi timiza wananidai 29000 huu mwaka wa wa pili na kila mwez nakopa NMB pesa fasta, sasa hv nshafika viwango vya kukopa hadi laki moja na ushee nkitaka.
Na mind you mimi sio mtumish wa serikali
 
Alichosema mleta mada;

1.Alikopa salio/muda was maongezi

2.Ameweka hela Airtel Money na kiasi kilichobaki kwe airtel money ya wamembadilisha kuwa salio LA kawaida wakati yeye may be kuna sehemu alitaka kutuma hiyo hela
 
Back
Top Bottom