Mhimili mmoja umeweka roboti, mihimili mwingine mnasubiri nini?

Mzalendo120

JF-Expert Member
Jul 2, 2022
1,601
2,091
Kuna lidude limewekwa bungeni nimeona hata wabunge wenyewe wanashangaa.
Zaidi ya upigaji kwa aliyelileta je roboti lile MDEBWEDO linamanufaa gani kwa bunge?
Kama manufaa yapo basi Serikali iwekwe roboti Ikulu na mhimili wa mahakama uweke lakwake

Mhimili wakusimamia rasilimali za nchi umekua kielelezo cha ufujaji. Nimeona hata baadhi ya mawaziri wanashangaa. Unaweza ukakuta hata wao hawajui nani amepeleka hilo toy bungeni.
Hii ni aibu kubwa. Spika aibu yako kwa niaba ya bunge. Umeudhalilisha mhimili. Kama kunajambo ambalo limekitia doa nihuo mdoli uliouweka hapo.

Aliyependekeza liwekwe pale au auziwe akaweke kwake limsaidie na familia yake.
 
Tunaomba utaratibu ulio tumika kuninua hilo Toy.

2. Tunaomba kujulisha dhamani yake na limenunuliwa kupitia budget ipi

3. Ni nini matumizi yake kulingana na dhamani yake.

4. Bunge likiisha linapelekwa wapinna kufanya kazi Gani.

5. Lengo la kulileta hapa bungeni ni nini
 
Tuna Vibinti Vibichi Vimemaliza Masomo yao havina ajira, Virembo balaa...!

Vipo tayari hata malipo ya Posho kama hamtavipa Mshahara. Halafu Watu wanaleta Robot..!

Hii dharau kwa Kodi zetu.! DHARAU TOZO ZA KWENYE SIMU mnazovuna bila ridhaa yetu..... Mnatukumbusha machungu
 
Tuna Vibinti Vibichi Vimemaliza Masomo yao havina ajira, Virembo balaa...!

Vipo tayari hata malipo ya Posho kama hamtavipa Mshahara. Halafu Watu wanaleta Robot..!

Hii dharau kwa Kodi zetu.! DHARAU TOZO ZA KWENYE SIMU mnazovuna bila ridhaa yetu..... Mnatukumbusha machungu
Niwabinafsi sana. Sasa wanaona wakae na matoy bungeni kuliko watanzania wenzao. Aibu kwa spika
 
Kwanza tujue limenunuliwa wapi, japan, amerika, china, india au korea na je likiharibika wataalamu wa kulitengeneza wapo, au litapelekwa nchi lilikotengenezwa likakarabatiwe huko au litaletwa jingine? Kama nchi tuache ushamba na ulimbukeni wa kufakamia teknolojia na kuzitumia mahali pasipostahili tutonekana ni majuha
 
Back
Top Bottom