Mbunge furaha matondo ataka kujua ni lini Bima ya Afya kwa wote kuanza

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,033
974

Mbunge Furaha Matondo Ataka Kujua ni Lini Bima ya Afya kwa Wote Kuanza

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote itatangazwa kuanza kutumika kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Aprili kwa tarehe itakayotajwa.

Dkt. Mollel amebainisha hayo Aprili 3, 2024 Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Furaha Matondo aliyetaka kujua ni lini Bima ya Afya kwa Watu Wote itaanza kutumika.

“Baadhi ya vifungu ambavyo vinaweka mifumo imara ya kutekeleza Bima ya Afya kwa Wote vimeshaainishwa na kuwasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sheria itatangazwa kuanza kutumika kabla ya mwisho wa mwezi wa nne mwaka 2024 kwa tarehe itakayotajwa,” ameeleza Dkt. Mollel.

Dkt. Mollel amesema kuwa serikali imeshaainisha vyanzo vitakavyohudumia watu wasio na uwezo wakiwemo wajane na watoto wa mitaani.

Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ilipitishwa na Bunge Novemba 1, 2023 na Rais Samia Suluhu Hassan aliidhinisha sheria hiyo Novemba 19, 2023 na tayari imechapishwa katika gazeti la Serikali la Desemba 1, 2023.

maxresdefaultaqwsdcf.jpg
GKOtBJgXwAARN4z.jpg
 
Back
Top Bottom