Matumizi ya N-card Kivukoni Kigamboni siyo shirikishi; yanafyeka salio la wananchi kimya kimya. Fanyeni hivi kuondoa tatizo

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,295
21,435
Matumizi ya Card kwenye vivuko ni mazuri lakini yamekuja na changamoto ya kuibia wananchi pesa zao kielektronikia!

Nauli ya kivuko ni tsh 200 kwa watembea kwa miguu, na elfu 1500 au 2000 hata zaidi kwa magari!

Pesa hiyo hukatwa unapochanja (scan)!
ZIFUATZO NI BAADHI YA CHANGAMOTO

1. Yapo makosa ya kibinadamu kwa watumiaji wageni kukatwa pesa mara mbili au zaidi kutokana na kuchanja kwa makosa ya ufaham (Hill linatatuliwa kwa elimu)!

2. Yapo makosa ya kimfumo wa mashine kukata salio la mtumiaji pasipo kufungua njia ( Hili tatizo linaweza kufyeka salio hata mara mbili, tatu au kukomba salio lote na mteja asielewe salio lake limekatwaje (mult error functional). HUU NI WIZI MKUBWA

3. Yapo makosa ya makusudi ya kiufundi! Badala ya mashine kukata kiwango sitahiki huwa inakata kiwango kikubwa zaidi mfano 300 au zaidi kimya kimya ! Huu ni wizi wa kimtandao!

SULUHISHO!
Temesa na TTCL wanaoendesha huo mfumo wa N-card pale kivuko waboreshe kwa kutoa taarifa mtu anapochanja (Notification message kwa mtumiaji)

Mitandao ya simu, bank na matumizi yote ya makato kwa njia ya kadi ni lazima yawe wazi kwa mlaji kwa njia ya meseji ili ajue kakatwa tsh ngapi.

Msipofanya hivyo basi huo wizi wa kuaminika mnaofanya unawalipa na sisi wajumbe tutakuja kuwanyoosha kwenye kura za maoni 2025! Harafu mambo ya kufungia watu kwenye mabanda kama ng'ombe muache achaneni na vivuko vikubwa vya kizamani.

Bajeti ya kununua vivuko vikubwa au kurekebisha vivuko vikubwa itumieni kununua SEA TAX NYINGI 8 ambazo zitakuwa zinasubiria abiria wajae level seat nakuondoka chapu.

Sea tax zikiwepo za kutosha kunakuwa hakuna haja tena ya kufungia watu kama ng'ombe wakati wanaakili zao timamu.

Kivuko cha magari kikibakia kimoja kinatosha kuvusha gari mhimu kwa bei kubwa! Anaeshindwa kulipia azunguke darajani.
 
Kwakweli ni changamoto sana hizo kadi, unaweza kuweka salio la 1000 wakati unaenda, wakati wa kurudi ukiweka kadi inakataa eti salio hakuna.

Huenda hiyo ya kupewa sms pindi ukichanja inaweza ikasaidia. Mimi sasa hivi nimeshaacha hata kutumia kadi zao, naenda na 200 yangu nampatia mwenye kadi anichanjie.
 
Kwakweli ni changamoto sana hizo kadi, unaweza kuweka salio la 1000 wakati unaenda, wakati wa kurudi ukiweka kadi inakataa eti salio hakuna...
Ni wizi wa kuaminika! Akumbukwe sana wakili msomi mtikila kesi za taasisi kwa uzembe na wizi kama huu alilala Nazo mbele!

Walitakiwa wafunguliwe kesi za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu
 
Yapo makosa ya kimfumo wa mashine kukata salio la mtumiaji pasipo kufungua njia ( Hili tatizo linaweza kufyeka salio hata mara mbili, tatu au kukomba salio lote na mteja asielewe salio lake limekatwaje (mult error functional). HUU NI WIZI MKUBWA
Nishawahi kukatwa halafu mlango haujafunguka, ikabidi nihamie njia nyingine
 
Back
Top Bottom