Manabii wa uongo waanza kuumbuka!

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
10,010
20,242
Tukisema, ukristo umevamiwa na manabii na mitume wa uongo, watu tuwe tunaelewa. Hawa wameletwa makusudi na shetani, wamepewa nguvu za miujiza na shetani, na kujivika vazi la “ulokole” wakati wao sio walokole, ili kuchafua image yote ya ulokole/wokovu watu waamini miujiza na motivational speeches badala ya Neno la Mungu.

Hii imedhihirika majuzi, mmoja wao alipotangaza wazi kwamba Yesu Kristo, sio Mungu, alikuwa mwanadamu wa kawaida tu. Lakini bado anashika Biblia ileile inayosema Yesu Kristo ni Mungu. Shetani alishaona, kuzuia wokovu toka nje ni nguvu, akaamua kuingia ndani, kwenye ukristo, ndio maana ukiona mchungaji yeyote anajali pesa, anavaa nguo za kumeremeta kama sharobaro, anapenda kuabudiwa na waumini, kuna wengine anafunguliwa hadi mlango wakati mikono anayo, anatandikiwa kanga akanyage, analindwa na mabaunsa rundo, ana kiburi kama kile cha jamaa wa arusha anayejiita mkuu, kiburi cha pesa za sadaka anaziita zake kumbe za wale anaowaringishia, kiburi kama kile cha kuhani pale kimara temboni, kiburi kama cha yule anayetaka watu walete nywele za utosi na kucha za kidole kidogo, kiburi kama cha muuza mafuta, maji, keki na chumvi za upako mwamposa, jua tu hapo hakuna mtumishi wa Mungu, ni ajenti wa shetani.

Maneno yao yamejaa hekima ya kibinadamu na sio Nguvu za Roho Mtakatifu, hayagusi nafsi wala kuponya roho, ila yanaonyesha miujiza, as if wanafikiri hatujui kama shetani naye anaweza kufanya miujiza. Kwa msiojua, siku Musa alipoambiwa na Mungu atupe chini fimbo aliyoshika, alitupa ikageuka nyoka, Farao naye aliita wachawi na waganga wa Misri wakatupa fimbo zao zikageuka nyoka, lakini yule nyoka wa Musa alimeza vinyoka vyote vya wachawi wa farao. Uchawi upo, uganga upo, miujiza ya kichawi ipo, shetani hajafa, anaweza kuhadaa wanadamu kwa kutumia wanadamu wengine kufanya miujiza ili wapoteze muda badala ya kuokoka waamini miujiza kumbe wanaamini shetani.

Sio mara ya kwanza mtu huyu kujianika. Tunakumbuka kipindi kile amelewa konyagi anatishia kuua watu, na siku ingine alikuja kuhojiwa akasema yeye ni mnywaji wa pombe ni kweli. Akaringa mbele ya tv kwamba yeye ana pesa, kawe ana nyumba kama 8. Amezijengaje? Kwa sadaka za watu wanaokopa nauli kwenda kwenye kusanyiko lake. Hii inaumiza moyo kwa kweli. Mwingine huyo anayezunguka akipotosha watu na miujiza ya mafuta kajenga hoteli mbalizi mbeya, ni mfanyabiashara mzuri tu, wala si mhubiri wa injili. Mnachotakiwa kujua, wewe ukitoa sadaka kusukuma injili, inatakiwa kwenda kuhudumia usukumaji injili, sio kujenga hoteli za mchungaji na watoto wake. Watu wapo vipofu. Hao sio watu wa Mungu, na hata kama pengine tungewapa benefit of doubt kwamba ni watu wake kweli ili ninyi wafuasi wao mridhike, mbona Yesu alisema mmepata bure toeni bure,wao wanauza, na wengine mnaingia kwao kwa consultation kwa fee kama mnaenda kwa daktari, wagonjwa ambao hawana hela watahudumiwa na nani kama hayo yangekuwa ndiyo mapenzi ya Mungu? Kwahiyo injili ni kwa wenye pesa tu.

Cha kumshukuru Mungu ni kwamba, huwa hawafiki mwisho mzuri, nyoka wa farao hata kama walimshangaza Musa aliyekuwa anafikiri Mungu wake tu ndio anaweza kufanya muujiza, mwisho wa siku walimezwa na nyoka wa Musa. Hata hawa manabii, historia inaonyesha huwa wanavumaaa ila inafika kipindi wanaaibika na kufedheheka na kabla hawajamrudia Mungu kwa kuacha uchawi wao na mikataba yao na mashetani, wanavunwa na moja kwa moja wanaenda motoni, kwasababu wamepoteza roho nyingi sana za watu. Kuweni makini, ninyi wapambe wao, kwasababu kikombe wanachostahili ninyi pia mtakinywea pamoja nao, Naamu hakika itakuwa hivyo!
 
Mchungaji kakutoa pangoni. Huenda imekuumiza sanaaa, ila huo ndio ukweli. Kumbuka sio wakristo wote wanaosali kwa kusema: "kwa jina la baba, mwana na roho mtakatifu" Jiulize kwanini?

Unaandika: " Kwahiyo injili ni kwa wenye pesa tu" Ndio swali zuri sana hilo. Kuna watu nimewasikia wakisema- ukitaka kuwa tajiri jiunge na ukristo. Sikuwaelewa wakati huo, ila hawa wachungaji wameweka mambo yote bayana kuwa Ukristo na pesa ni mapacha.

Nukuu: "Sio mara ya kwanza mtu huyu kujianika. Tunakumbuka kipindi kile amelewa konyagi.......... na siku ingine alikuja kuhojiwa akasema yeye ni mnywaji wa pombe ni kweli." Akaringa mbele ya tv kwamba yeye ana pesa"
Hivi ni mistari gani ndani ya Biblia imekataza kunywa pombe? Mbona unajichanganya! kwa maana mvinyo ni kinywaji cha kawaida kanisani.
 
Ole wao waamukao asubuhi na kufata kileo.........
 
Siku hizi hakuna kanisa ambalo halizingatii pesa mkuu.

Anayetoa michango ndo muumini kuliko wasiotoa (hata kama hawana)
 
Tukisema, ukristo umevamiwa na manabii na mitume wa uongo, watu tuwe tunaelewa. Hawa wameletwa makusudi na shetani, wamepewa nguvu za miujiza na shetani, na kujivika vazi la “ulokole” wakati wao sio walokole, ili kuchafua image yote ya ulokole/wokovu watu waamini miujiza na motivational speeches badala ya Neno la Mungu.

Hii imedhihirika majuzi, mmoja wao alipotangaza wazi kwamba Yesu Kristo, sio Mungu, alikuwa mwanadamu wa kawaida tu. Lakini bado anashika Biblia ileile inayosema Yesu Kristo ni Mungu. Shetani alishaona, kuzuia wokovu toka nje ni nguvu, akaamua kuingia ndani, kwenye ukristo, ndio maana ukiona mchungaji yeyote anajali pesa, anavaa nguo za kumeremeta kama sharobaro, anapenda kuabudiwa na waumini, kuna wengine anafunguliwa hadi mlango wakati mikono anayo, anatandikiwa kanga akanyage, analindwa na mabaunsa rundo, ana kiburi kama kile cha jamaa wa arusha anayejiita mkuu, kiburi cha pesa za sadaka anaziita zake kumbe za wale anaowaringishia, kiburi kama kile cha kuhani pale kimara temboni, kiburi kama cha yule anayetaka watu walete nywele za utosi na kucha za kidole kidogo, kiburi kama cha muuza mafuta, maji, keki na chumvi za upako mwamposa, jua tu hapo hakuna mtumishi wa Mungu, ni ajenti wa shetani.

Maneno yao yamejaa hekima ya kibinadamu na sio Nguvu za Roho Mtakatifu, hayagusi nafsi wala kuponya roho, ila yanaonyesha miujiza, as if wanafikiri hatujui kama shetani naye anaweza kufanya miujiza. Kwa msiojua, siku Musa alipoambiwa na Mungu atupe chini fimbo aliyoshika, alitupa ikageuka nyoka, Farao naye aliita wachawi na waganga wa Misri wakatupa fimbo zao zikageuka nyoka, lakini yule nyoka wa Musa alimeza vinyoka vyote vya wachawi wa farao. Uchawi upo, uganga upo, miujiza ya kichawi ipo, shetani hajafa, anaweza kuhadaa wanadamu kwa kutumia wanadamu wengine kufanya miujiza ili wapoteze muda badala ya kuokoka waamini miujiza kumbe wanaamini shetani.

Sio mara ya kwanza mtu huyu kujianika. Tunakumbuka kipindi kile amelewa konyagi anatishia kuua watu, na siku ingine alikuja kuhojiwa akasema yeye ni mnywaji wa pombe ni kweli. Akaringa mbele ya tv kwamba yeye ana pesa, kawe ana nyumba kama 8. Amezijengaje? Kwa sadaka za watu wanaokopa nauli kwenda kwenye kusanyiko lake. Hii inaumiza moyo kwa kweli. Mwingine huyo anayezunguka akipotosha watu na miujiza ya mafuta kajenga hoteli mbalizi mbeya, ni mfanyabiashara mzuri tu, wala si mhubiri wa injili. Mnachotakiwa kujua, wewe ukitoa sadaka kusukuma injili, inatakiwa kwenda kuhudumia usukumaji injili, sio kujenga hoteli za mchungaji na watoto wake. Watu wapo vipofu. Hao sio watu wa Mungu, na hata kama pengine tungewapa benefit of doubt kwamba ni watu wake kweli ili ninyi wafuasi wao mridhike, mbona Yesu alisema mmepata bure toeni bure,wao wanauza, na wengine mnaingia kwao kwa consultation kwa fee kama mnaenda kwa daktari, wagonjwa ambao hawana hela watahudumiwa na nani kama hayo yangekuwa ndiyo mapenzi ya Mungu? Kwahiyo injili ni kwa wenye pesa tu.

Cha kumshukuru Mungu ni kwamba, huwa hawafiki mwisho mzuri, nyoka wa farao hata kama walimshangaza Musa aliyekuwa anafikiri Mungu wake tu ndio anaweza kufanya muujiza, mwisho wa siku walimezwa na nyoka wa Musa. Hata hawa manabii, historia inaonyesha huwa wanavumaaa ila inafika kipindi wanaaibika na kufedheheka na kabla hawajamrudia Mungu kwa kuacha uchawi wao na mikataba yao na mashetani, wanavunwa na moja kwa moja wanaenda motoni, kwasababu wamepoteza roho nyingi sana za watu. Kuweni makini, ninyi wapambe wao, kwasababu kikombe wanachostahili ninyi pia mtakinywea pamoja nao, Naamu hakika itakuwa hivyo!
Dini zimevamiwa, sasa huyu akikuhubiria si upako wote unayeyuka kila ukikumbuka vivuzi vyake kwenye ile connection yake?
 
Attachments

  • IMG-20240516-WA0026.jpg
    IMG-20240516-WA0026.jpg
    55.4 KB · Views: 4
Hawa waabudu mashetani watakokota wengi kuzimu. Watu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa Hosea 4 :6.
 
Back
Top Bottom