Meneja CoLtd
Member
- Mar 6, 2021
- 58
- 55
Vijana wengi wamekua wakishindwa kuchagua ni binti yupi anafaa kuolewa, hivyo hivyo wanawake nao wameshindwa kutambua ni mwanaume mwenye vigezo vipi anafaa kukubaliwa kuolewa nae.
Mambo mnne muhimu ya kuzingatia kabla haujafanya maamuzi ni;
1. HOFU YA MUNGU (DINI)
Hiki ni kigezo muhimu sana cha kuzingatia, kwani mume au mke mwenye hofu ya mungu kuna asilimia nyingi atakua mkweli na kukupenda kwa dhati kama mafundisho yanavyotaka
2.CHIMBUKO AU ASILI YAO
Unatakiwa kuchunguza historia au asili ya yule unaetaka kuoa au kuolewa nae.
3. TABIA NA UZURI WAKE
Ili usije juta kutamani wanawake au wanaume wengine baada ya ndoa inapaswa uoe au kuolewa na mtu mwenye Tabia na uzuri unaoutaka. Hapa msisitizo ni TABIA maana Uzuri na muonekano hubadilika mda na mda.
4. MALI
Mwisho kabisa tutaangalia mali, duniani hamna anayetaka kuishi maisha magumu yeye wala familia yake, sasa kama akitokea mtu mwenye sifa kuu tatu za juu na ana mali (Mwanamme/Mwanamme) Basi huyo ndo mtu sahihi kwako.

NB: HAPA TUNAANGALIA ASILI NASIO KABILAWahenga wamesema mtu hawezi kuacha asili yake; ikiwa na maana kama ukoo wao ni wawatu wenye maadili mabaya kuna asilimia kubwa nayeye akawa hivyo au watoto wenu wakawa hivyo
Pia wahenga wamesema malipo hapahapa duniani; hapa unaweza jikuta unapata watoto wenye tabia mbaya wasumbufu ikawa ni kama malipo ya tabia mbaya alizofanya mke/Mme kwa wazazi wake. Au urithi wa tabia mbaya za babu zao.