Makala: Mfahamu Simba Karatasi wa Umakondeni

Seawhale

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
1,186
1,216
Historia ya kweli kumuhusu Simba karatasi huko umakondeni.

Mnamo miaka ya mwisho ya 80 hadi katikati ya miaka ya 90, huko kusini mwa Tanzania paliwahi kuwepo ndui aliyesumbua kwa kipindi kirefu kwa kuleta hofu kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mtwara.

Historia juu ya asili ya simba huyu ina utata mwingi, ila kubwa kuliko ni tukio la vijana wawili wa kimakonde ambao walikuwa wanagombania mke. Vijana hawa waliishi wilaya ya Newala maeneo ya mpakani na Msumbiji. Ugomvi wao ulikuwa ni wa muda mrefu, kushikana mashati kwao lilikuwa ni jambo la Kila siku, ndipo siku moja mmoja kati yao akaamua kutafuta suluhu ya kumaliza mgogoro moja kwa moja.

Kijana akaona azamie zake pande za Msumbiji kutafuta hiyo suluhu kutoka kwa waganga wa jadi waliojaa maeneo ya huko. Katika kuzunguka na kuulizia ndipo akafanikiwa kumpata bwana mmoja mzee wa makamo, akaelezea shida yake na mganga akamuambia kuwa amefika mahali sahihi na shida yake itatatuliwa kwa sharti kwamba ni lazima alete kitu chochote kinachomuhusu huyo adui wake, yaani iwe kiungo cha mwili, damu au nguo yake. Bwana yule akarudi kijijini kwake kutafuta namna ya kuvipata hivyo vitu, haikuwa kazi ngumu sana kwake kuvipata kutokana na asili ya mgogoro wenyewe.

Zilikuwa zimepita siku kadhaa bila kuonana na adui wake kutokana na jamaa kuwa kwenye shughuli za kilimo cha korosho huko mashambani. Sasa kuna siku alikuwa amerudi na ndipo akamtegea kwa yule mwanamke ili amfumanie. Jamaa kweli akajaa kwenye mtego, siku hiyo zilipigwa haswa na ndipo yule bwana akafanikiwa kumchana kwa kisu adui wake na kufanikiwa kupata damu.

Jamaa bila kuchelewa akafunga safari kuelekea Msumbiji kwa fundi wake, kufika kule akakabidhi ile damu na fundi akaanza kuifanyia kazi ile damu na alipomaliza akaifunga kwenye kitambaa chekundu na kuanza kumpa masharti yule bwana. Akamuelekeza kuwa kile kitambaa akakichimbie mlangoni kwa adui wake ili kusudi liwe kila yule adui anapotoka nje basi atageuka kuwa simba na akirudi ndani basi atabaki kuwa binadamu.

Mswahili yule akafunga zake safari na kurejea kijijini kwake. Kufika akavizia yule ndugu hayupo kwake na akafanikiwa kutekeleza maagizo kwa kukichimbia kile kitambaa chenye damu kwenye mlango wa adui. Jioni yule ndugu aliporejea akazama ndani ajabu alipojaribu kutoka sasa ghafla akageuka kuwa simba, watu waliokawa pale nje kuona vile wakatimua mbio.

Sasa shughuli ikabaki kwa yule simba, lilikuwa ni dume la simba haswa ambalo nalo kwa muda sasa lilishaanza kuhisi njaa na kwa bahati mbaya katika kuwinda akafanikiwa kukamata binadamu, sasa kule kwa mganga, yule bwana aliambiwa kwamba ahakikishe kuwa simba huyu hagusi damu ya mtu na kwa bahati mbaya ndiyo ikawa hivyo, ndui akafanikiwa kuonja damu ya mtu na ndiyo ikawa imeisha hivyo, ndui akatokomea mwituni na kuanza kuwa mwiba kwa wanakijiji.

Usiku mmoja kuna Mjane alishikwa na haja usiku wa manane, akajikokota kutoka nje na kuelekea maliwatoni, ile anakaribia tu ghafla akadakwa na yule simba akarushwa huko, sasa alipotua kile kishindo kikawaamsha majirani ambao nao waliingiwa hofu na kutoka nje kwa kuvizia wakiwa na silaha za jadi. Kuangaza huku na kule kwenye lile giza nene ndipo walifanikiwa kuona damu kuelekea vichakani, katika kuifuatilia ndipo wakakutana na mwili wa yule mjane ukiwe umeharibika vibaya kwa kuchanwa na yule simba.

Katika kushauriana cha kufanya, wakaamua mwili uachwe pale kama chambo maana ni kawaida kwa wanyama wala nyama kuyarudia mawindo yao, wakatengeneza kimnara ama kichanja kwa ajili ya kukaa walenga shabaha. Lengo lao lilifanikiwa kwani kuelekea alfajiri yule simba alionekana maeneo yale na walipojaribu kmfyatulia risasi ama gobole waliamini imempata, walisubiri pambazuko na walipofuatilia waliona watone ya damu kuelekea msituni, kuanzia siku hiyo yule simba hakuonekana tena pale kijijini.

Minong'ono ikaanza kuzunguka pale kijijini juu ya kupotea kwa yule mmakonde na tukio la kuibuka simba wa ajabu pale nyumbani kwake. Wazee wa busara wakaanza kuunganisha matukio na ndipo wakahitimisha kwamba kupotea kwa bwana yule kuna uhusiano wa moja kwa moja na kuibuka kwa simba huyu wa ajabu.

Wakaletwa waganga wa jadi pale kufanya matambiko na ndipo wakagundua uwepo wa kitambaa kilichofukiwa pale mlangoni. Yule bwana mwingine mswahili aliyemfanyia hayo mwenzake kuona mambo yameanza kufunuka akaamua kukimbia pale kijijini, na ndipo wazee wakaamini kwamba yule bwana atakuwa amegeuzwa kuwa simba na huyu mwenzake aliyekuwa anasumbuana naye mara kwa mara.

Baadae baada ya kama mwezi kupita, yule simba akaibukia vijiji vya jirani akiwa na nguvu mpya, hari mpya na kasi mpya. Aliendelea kuleta hofu hadi kupelekea wanavijiji kuanza kutembea kwa makundi huku wakiwa na silaha mbalimbali. Sasa kasi ya yule simba kuua kwa haraka kutoka kijiji kimoja hadi kingine na vile kwamba ukimpiga risasi ama mshale bado anaendelea kuwa hai ilipelekea wamakonde kumpachika jina la simba karatasi.

Kwa kasi yake hii mpya aliyokuja nayo ya kufanya matukio kutoka kijiji hadi kijiji ilifanya iwe ngumu kumuwinda huyo ndui. Aliendeleza ubabe wake maeneo ya Tandahimba hadi Naliendele hali ambayo ilipeleka taharuki maeneo hadi ya mjini kabisa na hapo ndipo askari wa wanyamapori wakajitosa kumsaka ndui huyo.

Walihangaika naye kwa kipindi kirefu na hatimaye katikati ya miaka ya 90 ndipo walifanikiwa kumpata na kumpiga risasi maeneo ya misitu ya Naliendele. Kuuawa kwa simba huyu lilikuwa ni tukio kubwa kwani alipakizwa kwenye 110 ya polisi wakawa wanamzumgusha kumuonesha kwa umma maeneo mbalimbali na huo ndio ukawa mwisho wa simba karatasi.

Nyongeza, nadharia mbalimbali zimekuwepo juu ya uwepo wa simba karatasi. Mosi, masimulizi ya wazee wa maeneo ya mkoa huu, ambapo hadi leo hii ukimkuta mzee mwenyeji wa mkoa wa Mtwara, hiki kisa lazima atakuwa anakikumbuka vizuri. Vilevile kwa vijana wenyeji wa miaka kuanzia 30 kwenda juu, watakuwa wanakifahamu hiki kisa.

Pili, vikundi mbalimbali vya ngoma za asili kutoka Mtwara, vinathibitisha uwepo wa kisa hiki kwani walipenda sana kumuimba huyu simba. Mfano kuna kikundi cha wazee wa kimakonde waliwahi kutoa rekodi ya ngoma waliyoimba wakimuelezea huyu simba namna alivyosumbua, biti lake lilikuwa ni la kugogandisha vyuma huku kiitikio yakisikika maneno, 'simbaa karatasiiii'.

Tatu, chapisho la Bwana B. Z Mkirya katika kitabu chake kilichochapwa na Ndanda Mission Press, kiitwacho 'Simba wa Tunduru', kinatoa ukweli juu ya uwepo wa simba huyu, kwani ndani yake aliweza kumuelezea kwa uchache.

Mwisho, tukio la kuuawa kwa simba huyu na askari wa wanyamapori na kitendo cha kumuonesha kwa umma na kumtaja kuwa ni simba karatasi, kunadhihirisha ukweli juu ya uwepo wa simba huyu.

Hitimisho, maeneo mengi ya mikoa ya kusini kuliwahi kuwa na simba wasumbufu hasa maeneo ya Tunduru, ila linapokuja jina 'simba karatasi', kwa kweli wanakusini wanamkumbuka vyema huyu ndui aliyewahi kueneza hofu hadi kupelekea watu kujifungia ndani mapema. Simba huyu kwa ukorofi na ukatili unaweza mfananisha na yule simba wa Tsavo Kenya. Wenyeji wa Mtwara ambao wapo humu jamvini watathibitisha ukweli zaidi juu ya kisa hiki.

Nawasilisha.
 
Hiki kisa ni cha kweli mkuu, sema kinasimliwa kwa namna tofauti lakini wote wanaishia kuthibitisha uwepo wa Simba wa Karatasi.

Matukio haya ni miongoni mwa sababu zilizopelekea kuzaliwa kwa nadharia isemayo kusini wanakula watu.
 
Ila maeneo ya jirani na Nanguruwe wenyeji wanasema kulikuwa na Pori lenye simba, Je haiwezi kuwa ni Simba halisi waliokuwa wakitoka porini?

Kuna watu walijenga miundombinu ya umeme kutoka Mtwara kwenda Tandahimba wanasema, maeneo ya jirani ya Nanguruwe walikuwa wanafanya kazi kwa tahadhari na masharti ya muda pia kukwepa hatari ya kukumbana na wanyama wakali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom