Madhara ya Vinywaji vya kuongeza nguvu (Energy Drinks) kwa afya

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
575
2,560
Energy drinks hutangazwa kama vinywaji vinavyoweza kuongeza nguvu na kuamsha ubongo.

Matumizi ya bidhaa hii yameongezeka sana siku za hivi karibuni jambo lilaloongeza hamu ya kujifunza na kufahamu madhara yake kwa sasa na baadae.

Wingi wa kemikali za caffeine huathiri utendaji kazi wa moyo na mishipa ya damu. Hii huongeza nafasi ya kuugua magonjwa ya moyo na shinikizo la damu.

Vinywaji hivi huharibu pia mpangilio wa saa ya ndani ya mwili wa binadamu inayoongoza mzunguko wa usingizi, huufanya mwili upoteze kiasi kikubwa cha maji, hupunguza uoni wa macho pamoja na kufanya baadhi ya watu wapatwe na hali ya kuweweseka.

Aidha, kopo moja dogo lenye ujazo wa 16 oz ( 470 mls) huwa na nyongeza ya sukari inayofikia hadi gramu 54-62. Kiwango hiki kinazidi mahitaji ya kawaida ya kila siku ya mwili hivyo huongeza nafasi ya kuugua ugonjwa wa kisukari, kuongezeka kwa uzito pamoja na kuoza kwa meno.

Watu wenye magonjwa sugu, wanawake wajawazito pamoja na watoto ni makundi matatu yasiyoshauriwa kutumia kinywaji hiki.

Kama ilivyo kwa vitu vingine, madhara yake huonekana pale kinapotumika kwa kiasi kikubwa. Kunywa kwa kiasi.

Chanzo: NIH
 
Energy drinks hutangazwa kama vinywaji vinavyoweza kuongeza nguvu na kuamsha ubongo.

Matumizi ya bidhaa hii yameongezeka sana siku za hivi karibuni jambo lilaloongeza hamu ya kujifunza na kufahamu madhara yake kwa sasa na baadae.

Wingi wa kemikali za caffeine huathiri utendaji kazi wa moyo na mishipa ya damu. Hii huongeza nafasi ya kuugua magonjwa ya moyo na shinikizo la damu.

Vinywaji hivi huharibu pia mpangilio wa saa ya ndani ya mwili wa binadamu inayoongoza mzunguko wa usingizi, huufanya mwili upoteze kiasi kikubwa cha maji, hupunguza uoni wa macho pamoja na kufanya baadhi ya watu wapatwe na hali ya kuweweseka.

Aidha, kopo moja dogo lenye ujazo wa 16 Oz ( 470 mls) huwa na nyongeza ya sukari inayofikia hadi gramu 54-62. Kiwango hiki kinazidi mahitaji ya kawaida ya kila siku ya mwili hivyo huongeza nafasi ya kuugua ugonjwa wa kisukari, kuongezeka kwa uzito pamoja na kuoza kwa meno.
authority?
 
Hamna kunywa kiasi

Ni kutokunywa kabisa

Nilikuwa mnywaji mzuri sana lakini sasa kinywaji changu pendwa ni maji.
 
Back
Top Bottom