Kwanini Wachekeshaji wengi wa kiume wanavaa kama wanawake kwenye kazi zao?

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
88
105
Ni jambo la kushangaza kwamba wachekeshaji wengi wa kiume wanapenda kuvaa mavazi ya kike katika kazi zao. Tena wengine wanavaa mpaka mawigi na wanapaka makeup kabisa

Huenda ikawa wanaona njia hii ya uigizaji inavutia sana watazamaji lakini ukweli ni kwamba huu udhalilishaji, kumdhihaki na kuwaona wanawake kama vichekesho kwenye jamii yetu.

Je, ni kwamba wamekosa mbinu na ubunifu kwa watazamaji ambazo wanaweza kuzitumia kwenye kazi zao?
 
Ni jambo la kushangaza kwamba wachekeshaji wengi wa kiume wanachagua kuvalia mavazi ya kike katika vichekesho vyao. Huenda ikawa wanaona njia hii ya uigizaji inaongeza kicheko kwa watazamaji, lakini kuna swali la msingi kuhusu kwa nini wanahisi hawawezi kuigiza kama wanaume na bado wafanye kazi zao vizuri. Je, hii inaashiria upungufu wa ubunifu au mbinu nyinginezo ambazo wangeweza kuzitumia? Matumizi ya mara kwa mara ya uvaaji wa nguo za jinsia tofauti yanaweza kuonekana kama njia ya kumdhihaki mwanamke, na hii inaweza kudhalilisha na kumfanya mwanamke aonekane kama kichekesho badala ya kuheshimiwa katika jamii.
Mwanamke ni chombo cha starehe, mwanamke ni pambo, mwanamke ni kiumbe dhaifu, na...........................
 
Kuigiza maana yake nini ? Ukishajua hilo nadhani utakuwa umejijibu..., Je Mwanaume akiigiza kama Mwanaume amekuwa anaigiza ?

Nadhani cha maana ni kama Kazi inakuvutia unaangalia kama haikuvutii na huyo mchekeshaji anaweza kujipatia mkate wake wa kila siku ina maana kuna watu anawavutia....

Nadhani Political Correctness has gone Mad...
 
Dishi likiyumba mtu Huwa anasahau jinsia yake mpaka achungulie, Sasa sokoni utachunguliaje unajikuta umeshanunua magauni, ,,,,,Hawa walioyumba madishi ndio wanaoigizwa na wachekeshaji😆😆
 
Sinawahi ona mantiki ya mwanaume kuigiza part ya mwanamke. Kwanini director au anaepanga waigizaji asimpe iyo nafasi mwanamke?
 
Sio mbaya mara chache ila kwa mara nyingi hiyo ni mbaya inamaana sio m-bunifu wa kazi yake
 
Ni project rahisi kuvuta mkwanja kutoka donor countries.... Maana kuna kitu kinapandwa kwenye kizazi cha baadae waone ni sawa tu kwa mwanaume kujifananisha na mwanamke. Ova
 
Back
Top Bottom