Kwa kukereka na mwendo wa taratibu wa Mabasi ya Mikoani naomba ombi langu likubaliwe

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,115
110,509
Kuwe na Mabasi Maalum ya Waoga wa Kufa ( yaendayo taratibu ) kama sasa na pia kuwe na Mabasi Maalum ya Tusio Waoga wa Kufa ( yaendayo kasi ) ili tusichoshane humu Barabarani.

Haiwezekani kutoka Dar hadi Moro zamani ukipanda Abood Dereva akiwa Dula Bedui ( sasa Marehemu ) unatumia dakika 90 au Saa Mbili lakini hivi sasa unatumia Saa 5 kufika.

Zamani ulikuwa ukipanda Allys au Zubery unatoka Dar Saa 12 Alfajiri na unafika Nyegezi Mwanza Saa 1 Jioni ila kwa sasa unafika ama Saa 6 au Saa 7 usiku.

Ombi langu hili likubaliwe haraka.
 
Hahahaha wale wenye stress, madeni na tuliyochoka maisha tuwe na gari zetu special pia
 
Vipi umesafiri niñi Leo. Maana saivi Dar unatoka saa12 moro unafika saa5.
KISBO imepunguza mwendo pia?! maana hiyó ndo ikuwa inakufaa Roho mkononi.
 
Mabasi yamefungwa mfumo, ukifika tu 80, king'ora Cha warning kinapiga! Ukiendelea kukaza basi taarifa inatumwa na ukifika stand kwenye ukaguzi unaonyeshwa muda na eneo ulipooverspeed!

Mfumo ni mzuri ila 80 ni ndogo aisee!
 
Samahani ndugu wajumbe,hapa mwandishi aliandika akiwa ameranduka.Uhai hauna spare.
 
Mabasi yanachosha mno. Nilikja napanda hakuna kulala kutoka mbeya to dar ila nazo saivi zimepigwa ban, wanataka pesa ndefu ili isafiri ama lah usafiri kwa lorry.

Speed ndogo inachosha sana kwakweli.
 
Kuwe na Mabasi Maalum ya Waoga wa Kufa ( yaendayo taratibu ) kama sasa na pia kuwe na Mabasi Maalum ya Tusio Waoga wa Kufa ( yaendayo kasi ) ili tusichoshane humu Barabarani...
Mkuu Kwa Nini uhangaike na mabasi ,panda ndege , hata kama ni ya kukodi sawa kama ukiwa na haraka sana.

Maana serekali haipo tayari kupoteza nguvu kazi Kwa mawazo ya mtu mmoja
 
80km/h ni speed ndogo sana ila ajali nazo zinatisha.

Dual carriage ndo dawa ya hii changamoto ila hii ni long term solution.
 
Mkuu Genta zamani enzi za kina Bedui (RIP) magari hayakuwa mengi Kama sasa.

Sass hivi kutoka Dar hadi Moro kuna jam kila sehemu.

Mimi naona serikali wakati inajenga barababra ya njia nne kutoka pale ilipoishia kibaha Hadi Moro ningeomba ijenge pia free way ambayo mtu anaruhusiwa kumaliza kisahani akipenda.
 
Changamoto ni barabara zisizijitosheleza. Tumechagua SGR. Tusubiri kwanza. Anyway, next year wataanza ujenzi. Eneo la hovyo zaidi ni kibaha to Mlandizi.
 
Back
Top Bottom