Chekechea na Primary nimesoma english medium private.
Sekondari Form 1 hadi 6 nimesoma Boarding private, Msosi Pilau kila J5 na J2, Ugali ni nadra sana.
Chuo kikuu sikupata mkopo ila si haba sikuwahi kupata changamoto za kiuchumi.
Rasmi na mimi nikawa baba, nikaanza kuwaza watoto waje kusoma KAYUMBA wakati mimi sijasoma huko ?
Hali yangu ni tofauti na waliowahi kusoma kayumba wao hata wakiwa matajiri wanaweza kusomesha watoto kayumba kwa uhuru, wana uzoefu na hizo shule kwahiyo wanaweza kuwasaidia watoto mawazo na ushauri, sasa mimi sijasoma kayumba wala siyajui mazingira yapoje nitamshauri nini mtoto ?
Natoa mfano mwepesi hata kama umesoma kayumba lakini ulipambaniwa ule milo mitatu, ni kwamba na wewe ukiwa mzazi kuna msukumo unakuingia upambane watoto wale milo mitatu, ukikutana na mzazi aliekulia maisha ya milo miwili nae analisha watoto mara mbili, akikupa ushauri kwamba ulishe watoto mara mbili ni ngumu kumuelewa hata kama watoto wake wana nguvu na afya kuzidi wako.
Ndivyo ilivyo kwa upande wangu, nilipambaniwa ili maisha yangu ya shule yawe mepesi ni ngumu mimi kuwapeleka watoto Kayumba, pia hata wazazi watanichukuliaje ? wamenipambania nisome kwa raha kisha waje kuona wajukuu wanaenda kayumba ?
Kwa sasa nina watoto watatu nawapambania wasije pitia maisha ambayo mimi sikupitia,
Suala la kufaulu wapo wanafunzi wanaokalia ndoo wanapasua vibaya mno, Kusomesha private kumelenga zaidi kumrahishia mtoto maisha ya shuleni
Ninajua zipo shule za bei rahisi mfano kuna shule za serikali za englsh medium, shule za sekondari za jumuia ya wazazi, n.k. kwa research yangu zimetofautiana kidogo na Kayumba.
Kwa sasa nina miaka 36 kiuchumi bado najibana sana hasa kwasababu bado najenga ili nihamie kwangu, imenibidi nitembelea IST ili kupunguza gharama za usafiri, Simu yangu ina miaka mitatu sijabadili, wife nae nashukuru anajua tunayopitia nae kapunguza vizinga

- First yupo form 1 boarding, ada milioni 2 na nusu kwa mwaka
- wa pili yupo Primary day ada laki 9.
- Huyu mwengine nae soon anaanza shule hio ya laki 9
- Sina mpango wa kuongeza mtoto wa ziada labda uchumi ukae sawa
Suala la kufaulu wapo wanafunzi wanaokalia ndoo wanapasua vibaya mno, Kusomesha private kumelenga zaidi kumrahishia mtoto maisha ya shuleni
- Vyoo visafi kila siku vinasafishwa
- Chakula kizuri shuleni
- Mazingira tulivu
- Usafiri shuleni hadi nyumbani
- kutumia kiingereza kwenye masomo tangu shule ya msingi
- Kila mwanafunzi ana kiti na dawati lake
- Hakuna kujazana darasani
- kujifunza computer utotoni
- Library
- masomo ya kupika, kushona, kuchora, n.k.
- watoto wengi hutokea familia zinazojali malezi na maadili.
- wanafunzi wengi hufika elimu ya juu (shule ya msingi 80% niliosoma nao tuna degree, kuna msukumo unaupata usiachwe sana na wenzako kielimu)
- n.k.