Kuna watu ustaarabu ni sifuri, unakaribishwa chakula Una agiza zaidi ya aliyekukaribisha

Ungemuita muhudumu umuambie "mletee chips kavu huyu jamaa" mbona easy tu..?
Mkuu bill yake alipewa mi nililetewa yangu ya chips yai na Fanta tu.
Akasukuma kwangu,hela hiyo ilikuwepo.
Tatizo sio rafiki yangu kivilee,
Sikutegemea kumkuta pale.
Usiku huo nilikua naondoka sikutaka ujinga mdogo mdogo.
Nikalipa ili tuondoke tu.
Badae anaomba hela tena.
 
Mada za kibahiri na umasikini.
Kama huna hela usikaribishe watu
Bora uwe umkaribishe, mtu hamjaonana 15 years.
Sio hata mtu wa karibu yako.
Umemkuta tu mahali anaagiza mavitu hovyo.
We unajua ana hela zake atalipa kumbe hana.
Sasa ni nini hicho.
Mwingine tumeenda out kaita mjimama wake.
Ukaja na mishangingi mingine minne.
Yanakula kama yanafukuzwa yanakunywa haswa 300000 ikaenda pale.
Weka top up 3 ingine nikabaki na chenji tu.
Toka siku hiyo yule mshkaji nikapiga chini.
 
Ulikua sahihi Ilipaswa uwe mkweli pia.Mwanangu karibu agiza Nina hela kadhaa hapa zitatutosha yeye angejiongeza kama mwana.Kuliko kutoa alafu unakuja kulialia huku.Unakosa baraka bure mchizi.
 
Haha, umenikumbusha mbali sana.
Kuna kipindi rafiki yangu alikuwa anataka kugombea ubunge Jimbo X, tukaambiwa tutafute wazee wa muda mrefu wa chama chake kwenye lile jimbo ili wamsaidie kuongea na wajumbe watakaompitisha kwenye kura za maoni. Basi tukakutana nao, maongezi yakaenda vizuri na wakataka kiasi chao ambacho walipewa bila shida. Mchana ile tunaondoka tukasema tupite sehemu tupige lunch, wale wazee sasa tukawa tumewapa lift, kufika sehemu ya msosi, tumeagiza menu za kawaida tu maana tushatoboka vya kutosha alafu wale wazee bila aibu wakaanza kuagiza Makange ya mbuzi na Makange ya Kuku, hapo sisi tunapiga wali nyama. Niliwaona wasenge sana wale wazee kiukweli. Na from there nilijua kabisa kwamba wale wazee hawatatusaidia tushinde wala nini na kweli hatukushinda na 20M yetu ikateketea kwenye kuhonga wajumbe. Wajumbe sio watu kabisa.
 
Kama huna hela usimwambie, ama lah muelekeze kikubwa, mfano bajeti yako ni elfu 10, unampanga kikubwa(mzee kuna 10k hapa agiza msosi) we ukisema agiza tu mtu anajua mambo yamenyooka mfuko una ruhusu
 
Kuna watu ustaarabu sifuri mtu kakukuta unakula mgahawani akaja kukaa kwenye meza yako ukaona utumie ustaarabu kumwambia na yeye aagize chakula maana sio vizuri kula huko mtu anakutazama usoni , unashangaa anaagiza vitu vizito vizito ! Tena zaidi hata unavyokula , halafu anamwambia muhudumu ongeza 😀 , ama kweli kuna watu mishipa ya aibu hawana
Siku nyingine kama hauna hela nyingi ya ziada uwe unamuagizia kabisa, mfano unamwambia mhudumu mpe mishkaki 5 na chips na sio kujitutumua kumwambia aagize kumbe unampigia hesabu anachoagiza
 
Kuna watu ustaarabu sifuri mtu kakukuta unakula mgahawani akaja kukaa kwenye meza yako ukaona utumie ustaarabu kumwambia na yeye aagize chakula maana sio vizuri kula huko mtu anakutazama usoni , unashangaa anaagiza vitu vizito vizito ! Tena zaidi hata unavyokula , halafu anamwambia muhudumu ongeza 😀 , ama kweli kuna watu mishipa ya aibu hawana
Usimwambie mtu aagize ikiwa hajakuomba na hukumualika.
Hii dunia wajanja wachache na wajinga wanazaliwa kila siku hawaishi.
 
Back
Top Bottom