Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,212
- 4,158
Ripoti ya THBUB inasema April 27 asubuhi Nusura alisafiri kwa basi la Manning Nice kutoka Dodoma hadi Babati. Kisha akapanda Coaster hadi Arusha, kabla ya kumalizia safari kwa basi la Ibra Line hadi Moshi. Lakini taarifa ya VC UDOM (Soma hapa Chuo Kikuu cha Dodoma chatoa taarifa kufuatia kifo cha Nusura) inasema April 27 Nusura alionekana chuoni akiendelea na masomo kama kawaida, pigia mstari neno KUONEKANA. That means alikuwepo na watu wakamuona. Je, inawezekanaje Nusura awe chuoni na safarini kwa wakati mmoja? Kati ya THBUB na UDOM kuna mmoja kapotosha. Je ni nani? Na kwa malengo gani?
1. Taarifa ya THBUB inasema Nusura alifariki tar. 1 May 2023 lakini taarifa ya UDOM inasema alifariki April 29. Mtu mmoja anawezaje kufa mara mbili? Kati ya THBUB na UDOM kuna mmoja kapotosha. Je ni nani? Na kwa malengo gani?
2. Taarifa ya THBUB inasema mara ya mwisho Nusura alifanya mawasiliano na rafiki yake anayesoma nae UDOM tar.1 May 2023, lakini taarifa ya UDOM inaeleza alifariki tar.29 April. Mtu aliyefariki anawezaje kufanya mawasiliano kwa simu? Kati ya THBUB na UDOM kuna mmoja kapotosha. Je ni nani? Na kwa malengo gani?
THBUB imeenda Moshi, Iramba alipozikwa, UDOM na kwa mkemia mkuu wa serikali. Kote huko imewahoji watu mbalimbali. Lakini nadhani management ya UDOM haikuhojiwa vizuri.
Kama THBUB imejiridhisha kuwa Nusura alisafiri tar.27 April kwenda Moshi, ilitakiwa wawaulize UDOM huyo Nusura aliyekua chuoni April 27 akiendelea na masomo ni yupi? Kama UDOM walikosea tarehe waombe radhi na kufuta kauli.
Pia kama THBUB imejiridhisha kuwa Nusura alifariki tar.1 May ilitakiwa wawaulize UDOM huyo Nusura aliyefariki tar.29 April ni yupi? Kama UDOM walikosea tarehe waombe radhi na kufuta kauli. Hii ingesaidia kupunguza doubts.
Lakini taarifa ya THBUB na UDOM kupingana kunaongeza mkanganyiko kuhusu kifo cha huyu binti. Halafu mwisho wa siku mtawalaumu wananchi kwamba wanapotosha, wakati ninyi wenyewe ndio mnawatengenezea mazingira ya upotoshaji kwa kushindwa kujipanga. Plz redo your homework.!
3. Tume inasema Nusura alipanda bus la Manning Nice April 27 hadi Babati, kisha akapanda Coaster hadi Arusha, kabla ya kumalizia safari yake kwa Ibra Line hadi Moshi. Lakini hakuna bus la Manning Nice linaloanzia safari asubuhi kutoka Dodoma. Basi hilo huanzia safari Dar kwenda Babati na hupita Dodoma mchana. Hili alilopanda Nusura asubuhi lilitoka wapi?
4. Tume inasema walipeleka matapishi ya Nusura kwa mkemia mkuu wa serikali kujua kama kuna viashiria vya sumu kwenye chakula alichokula. Kumbuka Nusura anadaiwa kutapika akiwa nyumbani kwa Mchumba wake, kabla hajakimbizwa hospitali. Je Mchumba wake aliwezaje kutunza matapishi badala ya kuyafukia? Alijuaje Nusura atakufa na matapishi yake yatahitajika kwa ajili ya vipimo?
5. Nusura alifikia kwa mchumba wake Moshi mjini, lakini eti alipotapika alipelekwa Faraja Dispensary iliyopo Himo. Kwanini hawakumpeleka KCMC, Mawenzi au hospitali kubwa zilizopo Moshi mjini, badala ya kumpeleka Zahanati iliyopo 35Kms nje ya mji?
6. THBUB imeanzishwa chini ya Ibara ya 129(1) ya Katiba ya Jamhuri. Kifungu cha 15 (1) cha Sheria ya haki za binadamu na utawala bora sura ya 391 kimeipa tume mamlaka ya kuanzisha uchunguzi wa malalamiko yanayoashiria uvunjifu wa haki za binadamu. Tume imetumia mamlaka haya ya kisheria kuanzisha uchunguzi wa kifo cha Nusura.
Lakini je kuna matukio mangapi ya uvunjifu wa haki za binadamu Tume haijajishughulisha nayo? Wakati wa Magufuli watu walitekwa na kupotea lakini Tume haikufanya uchunguzi. Maiti ziliokotwa ufukweni kwenye sandarusi lakini Tume ilikaa kimya.
Akina Ben Saanane, Azory Gwanda na wengine walipotea, na mpaka leo hata mifupa yao haijaonekana. Familia zao zina maumivu makali lakini Tume haisikii kilio chao. Lissu na Aquilina walipigwa risasi mchana kweupe, lakini Tume haijafanya uchunguzi wowote.
Sabaya alimkata mtu sikio, akavunja miguu watu wa familia moja na matukio mengine ya kikatili Tume haikutoa tamko. Makonda alivamia Clouds na bunduki Tume ikaufyata. Hata leo bado kuna matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu, lakini Tume haiyaoni. Lakini tukio la Nusura, Tume imejitosa haraka kufanya uchunguzi na kutoa tamko. Je kwanini Nusura na si matukio mengine?
MyTake
Watu walitarajia ripoti ya THBUB ingemaliza mkanganyiko uliokuwepo, lakini ni kama vile mkanganyiko umezidi kuongezeka.
Pia soma:
- Tume ya Haki za Binadamu yatoa ripoti ya kifo cha Nusura Hassan Abdallah, chasema hakuna uhusiano na ajali ya Waziri Dkt. Festo Dugange
- Polisi yatoa taarifa rasmi juu ya kifo cha Mwanafunzi wa UDOM, Nusura Hassan Abdallah
Credit: Malisa GJ