Kielelezo kinatakiwa kusomwa kwa sauti Mahakamani

Apr 26, 2022
69
104
Nyaraka ikishapokelewa kama kielelezo Mahakamani, inatakiwa yule shahidi aliyeleta hicho kielelezo asome kwa sauti kilichomo ndani ya hicho kielelezo mbele ya Mahakama, ili upande wa pili kwenye kesi uweze kuelewa yaliyomo kwenye kielelezo na kuweka pingamizi kama anataka kupinga. Kama kuna pingamizi Mahakama itasikiliza na kutoa uamuzi mdogo (Ruling) kuhusu kukubaliwa kwa hicho kielelezo.

Kushindwa kumpa nafasi shahidi asome yaliyomo ndani ya kielelezo ni kosa lisilorekebishika kisheria (ni fatal) na inaweza hata kubatilisha mwenendo wa kesi nzima hasa ikiwa kielelezo hicho ndo ulitegemea sana kuthibitisha madai yako, kwa sababu kitaondolewa kwenye ushahidi alafu Mahakama itaangalia kama ushahidi wa maneno au nyaraka zingine uliobaki unatosha kusimama peke yake na kuthibitisha kesi yako?

Hii ni kwa mujibu wa maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi ya Selemani Selemani Mkwavila Vs Agatha Athuman, Land Appeal No. 5 of 2022.

Mahakama ya Rufani ambayo ni Mahakama ya juu kabisa nchini Tanzania pia inaunga mkono utaratibu huo huo, ambapo inasema, haijalishi ni kesi ya madai au jinai, (Mahakama ya Rufaa inasema) nyaraka ikishapokelewa kama kielelezo Mahakamani inatakiwa isomwe kilichomo ili upande wa pili ajue aina ya ushahidi uliotolewa dhidi yake ndani ya hiyo nyaraka.

Kushindwa kusoma kilichomo kwenye kielelezo ni kosa lisilotibika (ni fatal) na nyaraka ambayo haikusomwa Mahakamani inatakiwa kuondolewa kwenye rekodi (kumbukumbu) za Mahakama haitakiwi kabisa kuzingatiwa kama sehemu ya Ushahidi.

Hii ni kwa mujibu wa maamuzi ya Mahakama ya Rufani kwenye kesi ya Bulungu Nzungu dhidi ya Jamhuri, iliyosikilizwa Shinyanga kwenye Rufaa ya Jinai namba 39 ya mwaka 2018.

Hapo chini nimekuwekea screenshot ya kurasa za maamuzi hayo. Maamuzi full yanapatikana mtandaoni kwenye website ya Tanzlii.
 

Attachments

  • FB_IMG_1714575968722.jpg
    FB_IMG_1714575968722.jpg
    161.3 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1714575963160.jpg
    FB_IMG_1714575963160.jpg
    147.3 KB · Views: 3
  • FB_IMG_1714576659784.jpg
    FB_IMG_1714576659784.jpg
    126.9 KB · Views: 3
Back
Top Bottom